Mawazo yenu tafadhali

pondiboy

Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
81
Reaction score
29
Wakuu nisaidieni, mimi ni kijana mwenye miaka 27.

Nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulidumu kwa miaka mitatu, nilimpenda mno mwisho wa siku alinitenda, niliumia mno, nilichanganyikiwa kwa ujumla, nilikuwa mwaminifu saana kwake wala sikuwahi kumsaliti.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kwamba kwa sasa nimepata shida nadhani ni la psychology, nimejikuta nawatongoza wasichana nikikaa wiki moja naanza kumchukia natafuta njia ya kumwacha!

Katika kipindi cha January to April nimeshawatongoza wasichana 5. Japo sijawahi ku do nao! Siipendi hii kabisa hali nisaidieni nifanyeje niondokewe na hii hali?

Natamani nipate msichana ambaye angeweza kurudisha hisia zangu za kimapenzi!
 
Tulia kwanza upone hayo majeraha then ndo uingie kwenye uhusiano mwingine!
Only time can heal a broken heart!
 
Kweli wewe ni mwaminifu na nimeamini...
yani from January to April only 5 girls?
aliekutenda hana huruma, ningekuwa single ningekuchukua....
 
Ebu rudi kwa hao mabinti watano na gegedana nao wote..then rudi hapa uchukue councelling
 
Ebu rudi kwa hao mabinti watano na gegedana nao wote..then rudi hapa uchukue councelling

We Papupi em acha kumpoteza kijana mwenzio jamani. Si bure jina lako linafanana na papu..hi, lol. Kaka ushauri umeshatosha. Ni kwamba hujawa tayari kuanza mahusiano mapya. Acha muda upite majeraha yapone. We uambie tu moyo kwamba ulipenda mtu asiye sahihi na ushukuru kaondoka, jisamehe, msamehe, basi. Kaa peke yako mpaka uone unahitaji mwanamke kwa sababu umempenda na si kwa sababu unatafuta faraja au kisasi.
 
Jitahidi uwe unaweza kuyamaliza maswala yako binafsi wewe mwenyewe achana na hii ya kumtegemea mtaalamu, wewe mwafrika uhitaji mwanasaikolojia kuendesha maisha yako.

Waachie wamagharibi
 
Jitahidi uwe unaweza kuyamaliza maswala yako binafsi wewe mwenyewe achana na hii ya kumtegemea mtaalamu, wewe mwafrika uhitaji mwanasaikolojia kuendesha maisha yako.

Waachie wamagharibi

Huu ushauri wako hatari, hata zamani counselors walikuwepo, wazee waliaminika kuwa na busara na vijana walienda kwao wakashauriwa.
Sasa hivi mfumo wa maisha umebadilika, hao wazee wanaishia Chalinze. So usitake mwenzio apate uchizi, kuna wakati mtu anakuwa hana la kufanya na anahitaji ushauri. Kaka mtoa mada tafuta Counselor akusaidie, soma majarida ya psychology yanaweza kukusaidia kukujengea self esteem. Pia usisahau kumuomba Mungu akupe aliye mwema.
Nakutakia kila la heri
 
Nimekupata kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…