Mawazo ya Dr. Kigwangala yana walakini

Mawazo ya Dr. Kigwangala yana walakini

JAPUONY

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Posts
383
Reaction score
186
Ndugu wana bodi,

nimependa niwape tu machache juu ya kwanini Khamisi Kigwangala anapendekeza RC Mtwara pamoja na DC wake wang'olewe au watolewe kafara.

Katika fukunyungu za kisiasa Simbakalia amekuwa akiombwa muda mrefu na Wananzega ( ambako ndo kwao)kuwa agombee Ubunge wa Jimbo la Nzega suala ambalo amekuwa akilikataa kwa sababu kuwa siasa za Nzega zimejaa ufitini na yeye hahitaji siasa za kufitiniana.

Dr? Kigwangala amekuwa akimhofia Simbakalia kwa muda mrefu sana juu ya uwezekano wa kuja kuwa mpinzani wake ndani ya CCM kwa jimbo la NZEGA. Hvyo, Kigwangala kupendekeza RC Mtwara aondolewe ni mbinu za kutaka kummaliza nguvu Mzee Simbakalia. Anaimani kuwa kama ndugu Simbakalia ataondolewa katika nafasi yake ya sasa ya Ukuu wa Mkoa atakuwa amepungua nguvu na hivyo kuwa na uwezo mdogo wa kuja kuwa Mpinzani wake Mkuu kwa siasa za 2015.

Lazima mkumbuke pia kuwa pale NZEGA yupo pia Hussein BASHE ambaye pia ni threat kwa Kigwangala na amekuwa akitumia mbinu chafu za kuhakikisha wawili hao wanakwisha nguvu za kisiasa ili awe na uwanja mpana na huru kwa 2015.

so, watch out guys maamuzi ya Wanasiasa siyo ya kuwaamini kabisa.

Bado naamini kuwa kumfukuza RC na DC siyo suluhisho la mgogoro wa Mtwara kwa mambo yafuatayo:-

1. Siyo signatories katika mkataba wa gesi
2. Siyo wahusika wa kuwapa elimu wana Ntwara juu ya mkataba wa gesi na watakavyofaidika, ni kazi ya Wizara na Waziri aliyesaini mkataba huo
3. RC huyu na DC wake wamehamishiwa katika mkoa huo hivi karibuni kukiwa hayo mambo ya gesi yamesha anza muda mrefu pale Mtwara na Wizarani!!!
4. RC na DC hawana mamlaka za kisheria za kuagiza JWTZ, POLISI toka nje ya Mtwara kuja kupiga wanamtwara, ni IGP na Mkuu wa JWTZ.
p​

Tuwe makini na wanasiasa!
 
Watu mnakera sana.... Ni chuki tu kila kona, halafu mnajidai mnamtumainia mungu
 
Aiseee inaonekana kuna kaharufu ka ukweli hapa, by the way acha waparurane makamanda mbele kwa mbele.
 
Back
Top Bottom