Mawazo kwa serikali kwa ufupi

Mawazo kwa serikali kwa ufupi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,828
Reaction score
15,607
1. Punguza kodi na kodi zijulikane wazi: Mlipa kodi yeyote hatakiwi kusubiri mpaka mzigo ufike bandarini kujua ni kodi gani alipe. Hii inapunguza biashara, inapunguza idadai ya watu kuleta vitu n ahata inapunguza upelekaji wa vitu nje. Kodi inabidi ziwe rahisi sana kujulikana na kusiwe na tabia ya makisio ya kodi. Kodi itokane na receipt kama wenzetu hii inaongeza ushindani kama nimepata gari kwa bei rahisi haina maana wote tena tulipe kodi sawa maana kodi inatakiwa kutokana na kiasi nilicholipa. Hii inachochoe ushindani. Vilevile kodi zipo juu sana hivyo angalieni vitu ambavyo vina add value mfano gari ikiingia moja kuna kodi nyingine nyingi itachangia mafuta, matairi, spare, road tax….. hivyo kupunguza kodi ya magari inafaida kubwa kwa miaka mingi kuliko kukosa kodi au kupata mara moja kubwa kwa magari machache

2. Rahisisha kufungua biashara. Haitakiwi mtu anafungua biashara kwa pesa yake na serikali inafanya tena iwe ngumu kufungua na iwe na bei. Pesa inatakiwa kwenye kwenye biashara.

3. Punguza kodi au ondoa kabiasa kwenye vifaa vya ujenzi kama mbao. Kama tunataka kuweka mazingira yetu sawa na tusikate miti tutoe kodi kwenye mbao ambazo ziko juu sana.

4. Rahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi kuwa rahisi

5. Ingiza technologia kwenye masomo. Technologia ikitumika vizuri inaweza kufanya watoto wetu waweze kusoma zaidi kwa bei nafuu yaani kuna vitabu vingi sana vya bure lakini unahitaji mtandao. Hii ni sababu kubwa sana watoto wetu wako nyuma kielimu.

6. Shughulikia swala la umeme rahisi na wa uhakika

7. Achana na upinzani haisaidii nchi kulumbana kuhusu mikutano yeyote aongee chochote . Watu mwishoni watajali maendeleo maneno mazuri yawe ya CCM au CUF hayasaidii ni maendeleo tu. Mfano wa Zanzibar kwasababu maendeleo hayakuweko kila uchanguzi kwa miaka 15 Seif amekuwa akishinda… issue ni maendeleo tu. Kugombana na upinzani kumepunguza sana sifa yaserikali bila kuongeza chochote cha msingi. Vyombo vyetu wa sheria haviheshimiki kama zamani tena. Kutoka moyoni tunaomba haya muache hayasaidii kabisa

8. Kwenye Afya anzisheni mobile medical: Yaani team ya Dr mbalimbali wanatembea kwenye magari maalumu na kupima, kutoa matibabu mbalimbali. Hatutaweza kujenga Medical Center kila mahali na kuwa na Dr kila mahali kwenye nchi kubwa kama Tanzania. Tusiige Europe wana mazingira tofauti. Kuna mpaka mobile CT, Xrays….., kama ni lazima. Wana set camp kwa muda vijijini. Tujue magojwa mengi ni elimu, chanjo na dawa tu hasa za kisukari na pressure…

9. Ajirini watu wenye ujuzi kuliko wenye elimu. Kuna watu wengi serikalini wana elimu lakini hawana ujuzi. Unaweka wakuu wa TRA kwenye kodi za biashara wakati hawajawahi kufanya biashara, hawajui uchungu wa wafanyabiashara na hali halisi. Ni vizuri mtafute watu ambao ndiyo wawe wasomi lakini hasa wawe wafanyabiashara watawasaidia kuongeza ukusanyaji na urekebishaji wa kodi. Hawa mara nyingi watawapa mpaka mawazo ya ushindani wa nje

10. Bank ni tatizo. Mikopo iko juu sana kwenye riba. Serikali iweke gurantee kupunguza gharama za mikopo, serikali iache kukopa ndani. Lakini wekeni system ya credit rating, vitambulisho vya taifa etc kukuza uhakiki wa watu ili kupunguza risk za bank.

Ardhi/Land: Tuanche sheria za kisifa yaani mfano sasa hivi ukienda kununua shamba pori bagamoyo halafu ukasafisha na kuanza kulima ndiyo uvamizi na wanakijiji wanataka sehemu yako. Wanasiasa kwa sifa wanaweza kuchukua sehemu yako wakati kuna vichaka kibao. Hii
 
wachumia tumbo wamevimbiwa na madaraka, itachukua muda kuelewa ulichoandika.
 
2018 Je yapi yamefanyiwa kazi
Zitto
 
Back
Top Bottom