Mawaziri Wetu Wanaifanyia Nini Nchi Yetu

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
409
31
Wakuu,

Lini hasa tutawaweka KITIMOTO Mawaziri wetu ili watueleze wanaifanyia nini nchi yetu na tutegemee nini zaidi toka kwao. Utaratibu wa kila wiki kwa Mawaziri angalau wawili kuongea na Watanzania kupitia redio na televisheni kwa angalau saa tatu naamini unaweza kutusaidia.

Pia ni muhimu sana tukaanzisha utaratibu kwa Baraza la Mawaziri kuongea na Watanzania angalau mara moja kila robo mwaka kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
 
Anza na rais anaifanyia nini nchi hii, ukipata jibu huna haja ya kwenda mbali,Unawaonea bure mawaziri wa watu. waacha wamalize honeymoon yao ya miaka 5. kila kitu wamelipiwa na JK!

Nwachukia wote mnaomkwepa JK na kuanza kuuliza uliza mawaziri, RAIS AKIWA SMART system yote inakuwa smart!

Sasa Pinda naye utauliza anafanya nini, wakati JK kamweka makusudi aakijua hatafanya lolote, hatampita kwa umaarufu, sanamu tu,haya ukiona PM zero hao mawaziri wa nini for God sake!waacheni watanue.wengine wanatamba kabisa kamuulize aliyetuchagua!!!
 
Sabi Sanda unachojaribu kukisema ni sawa. Ila kila nisomapo mijadala kama hii ninakumbuka alichosemaga kiongozi mmoja aliekua na upeo na busara.. si mwengine bali JFK pale aliposema...

"And so, my fellow Americans: ask not what your country can do for you - ask what you can do for your country"

Je unadhani sisi Watanzania tukichuka hili fundisho na kufanya kivitendo, Tanzania itakua ni nchi ya aina gani. Tuache kua walalamishi kila mara....
 
Ni kweli tujenge utamaduni wa kufanya kazi ila hata hivyo siasa zinatuangusha big time. Imefika mahali sasa tuanze kuonyesha kwa vitendo nini tunachokitaka.Na ndo ushauri anaoutoa mkubwa hapo juu, mijadala nao wako kwenye wizara kufanya nini
 
Waberoya,

Nashukuru kwa mchango wako. Wazo langu halimkwepi Rais. Na ndo maana umeona nimependekeza Baraza la Mawaziri chini ya uwenyeketi wa Rais liwe linaongea na wananchi moja kwa moja kila robo mwaka. Na kama alivyosema Ndahani ni muhimu tukawa na utaratibu huu ili tuwaeleze Mawaziri wetu na Rais nini tunataka na wao watueleze nini tutegemee toka kwao. Pia nakubaliana na wewe asilimia 100 kuwa Rais akiwa Smart nchi itasonga mbele kwa kasi kubwa. Ila hili liweze kutokea ni muhimu pia Wizara zikaongozwa na Mawaziri, PSs na Wakurugenzi waadilifu na wanaochapa kazi.
 
Back
Top Bottom