mawaziri wababaishaji na wavivu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mawaziri wababaishaji na wavivu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Mar 21, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WIKI hii kuliibuka jambo ambalo liliwashtua watu ambalo ni taarifa za kujiuzulu kwa Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, kwa kile kilichodaiwa kuwa ameamu kuchukua hatua hiyo kutokana na kitendo cha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumzuia kuendelea na utaratibu wa kubomoa nyumba za watu waliojenga katika hifadhi ya barabara nchini kote.

  Taarifa ya kujiuzulu kwa Magufuli ilisambaa haraka kama moto nyikani jijini Dar es Salaam, lakini baadaye ikakosa uthibitisho na siku moja baadaye Serikali ikatoa maelezo kuwa waziri huyo hajajiuzulu.

  Lakini kwa ujumla tukio la Waziri Mkuu Pinda kumzuia Magufuli kuendelea na bomoabomoa linatoa taswira nyingi kwetu sisi wananchi.

  Labda wasomaji wangu niwakumbushe kwanza Waziri Mkuu Pinda alichosema akiwa katika mkutano wa hadhara akiwa nyumbani kwa Magufuli eneo la Chato, mkoani Kagera hivi karibuni.Alimwagiza Magufuli kuacha mara moja zoezi la bomoabomoa linaloendelea nchi nzima mpaka Serikali itakapotafakari upya mbinu gani itumike.

  Alisema Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa hawakupatiwa elimu ya kutosha juu ya zoezi hilo na kwamba likiendelea linaweza kuibua migogoro isiyokuwa ya lazima.Alisema kasi aliyokuja nayo Waziri Magufuli imekuwa kali sana, kwa hiyo hata watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) wamekuwa wakipata malalamiko mengi lakini, wanashindwa kumueleza ukweli kutokana na kasi yake hiyo.

  Alisema suala hilo linarudishwa Serikalini ili Baraza la Mawaziri likae na kulitafutia ufumbuzi na badala yake lipelekwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na kupatikana mwafaka.

  Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa maelezo hayo ya Waziri Mkuu Pinda kwa Magufuli ni yanatoa tafsiri nyingi mno.Tafsiri ya kwanza ni kwamba Serikali sasa haihitaji staili ya utumishi wenye kufuata Sheria anaoutumia Magufuli. Serikali inaona sasa Magufuli ndiyo adui wake kwa sababu anaikosanisha na wananchi.

  Kosa la Magufuli ni kasi aliyokuja nayo katika kutekeleza majukumu yake na huenda kauli yake aliyoitoa kwamba mtu yoyote aliyejenga katika hifadhi ya barabara hata ikiwa ni majengo ya CCM atayabomoa, ndiyo iliyomponza.

  Serikali ya awamu ya nne, haihitaji mawaziri wachapakazi inahitaji mawaziri wavivu, mabingwa wa kuzungumza na kumdanganya Rais, huku wakishirikiana na mafisadi kuhujumu nchi.

  Serikali imezoe kuwa na mawaziri wababaishaji ambao wanaidaganya kila ma kuwa wanafanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kukamilisha mradi iliyoko chini ya wizara zao, kumbe hakuna kitu.

  Rais Kikwete alipotembelea Wizara Elimu juzi nilishangaa kusikia kuwa wizara hiyo imeshindwa kutumia Sh30 bilioni wakati wanafunzi wengi bado wanakaa chini, walimu wapya hawajalipwa mishahara na kuna matatizo lukuki lakini, sikumsikia Rais akitaka maelezo ya kina kuhusu jambo hilo.

  Tamko hili la Pinda linatupa picha kwamba Serikali inakubali kusalimu amri kwa watu ambao wamevunja sheria kwa sababu ya kuhofia kunyimwa kura katika uchaguzi mkuu ujao, au sababu nyingine wanazozijua.

  Tafsiri ya pili tunayoipata ni kwamba, kasi ya utendaji wa Magufuli imeaanza kuwatisha baadhi ya mawaziri ndani ya Serikali ya Rais Kikwete, kiasi kwamba wanaanza kuhofia nafasi zao.

  Picha tunayoipata katika jambo hili ni kwamba huenda mtoto wa mkulima anahofia cheo chake baada ya kumwona Magufuli akifanya mambo ambayo mawaziri wengi hawawezi kuyafanya.

  Waziri Mkuu ni binadamu kama wengine naye anaweza kuwa na hofu hiyo kama aliyepo chini yake atamwona anahatarisha nafasi zake yake.Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Pinda kumuumbua Magufuli hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa wakati akiwa Waziri wa Tamisemi, alipotoa tamko la kumpinga waziri mwenzie huyo juu ya hatua yake ya kuzuia Uwanja wa Nyamgana mjini Mwanza kubadilishwa matumizi yake.

  Pinda alitaka uwanja huo ugeuzwe matumizi, lakini Magufuli aliapa kuwa hautageuzwa matumizi akiwa bado Waziri wa Ardhi na Makazi. Na kweli uwanja huo haujageuzwa matumizi mpaka leo baada ya kuwepo shinikizo kubwa la wananchi kuzuia mpango huo wa Serikali.

  Kwa ujumla ni kwamba uamuzi wa Pinda haukisaidii chama au Serikali kupendwa na wananchi, bali unaanika udhaifu wake kwamba haina uwezo wa kusimamia mambo yake.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  professionally pinda ni mwanasheria ... ?
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  alisoma sheria ila sikumbuki ni level gani lakini nimekwisha wahi kuona kwa cv yake kwa mba alisoma sheria!
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hivi serikali ilikuwa wapi wakati watu wanajenga kwenye hifadhi ya barabara? Sheria haikuwepo? Mnataka kutiana umaskini tu!! Mtu amejikusuru amajenga kakibanda kake huku akiwa na hati ya kiwanja kutoka serikali hiyohiyo leo unataka kukurupuka na kumvunjia bila malipo, aaaah wapi? Serikali ikae ione njia bora ya kulimaliza hili tatizo. Kuna watu wamepewa viwanja na wana hati halali za kumiliki viwanja na wamejenga nyumba ila ndani ya hifadhi ya barabara, kwa nini uwahukumu hao kwa kuwavunjia nyumba ili hali waliotoa viwanja wapo? Kuna sheria zinakinzana; moja ya mipango miji na nyingine ya barabara kwa hiyo hizo sheria zinatakiwa ziwe harmonized na siyo kukurupuka kuvunja nyumba.
   
Loading...