mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,223
- 4,681
Wanasema ukitaka kujua uhondo wa ngoma basi ingia uicheze. Na wengine wanasema mpira unakuwa mrahisi sana ukiwa nje ya uwanja, ishu inakuja ukipewa jezi uonyeshe uwezo wako..
Mawazo yangu ni kuhusu serikali ya Magufuli. Magufuli kama Magufuli hana shaka anajulikana uwezo wake kiutendaji na kufatilia mambo. PM Kassim Majaliwa na yeye moto wake unaonekana ni mfuatiliaji wa mambo na mpiganaji wa kweli.
Ishu ipo kwa mawaziri wa Magufuli. Kiukweli wengi mimi bado hawajanivutia wala kunishawishi. Wameshindwa kabisa kukata kiu ya matarajio yetu kwao.
Najua wengine watajitetea kwamba wanakosa bajeti labda tusubirie bajeti au wana visingizio lukuki lakini kwa kweli kuna vitu haviitaji bajeti wala mabadiliko ya kisera.
Mfano Prof Ndalichako mpaka sasa sijaona alichofanya kikubwa kusimamia elimu yetu especially elimu ya msingi na secondary. Nchi bado ipo kwenye mataifa mawili ya kielimu ilihali mtaala ni mmoja. Kuna shule zina term tatu na kila term ina ada yake na kuna shule zina term mbili kwa mwaka. Kuna shule zina walimu hawana ata cheti kimoja, kuna shule zipo sebuleni, kuna shule wanaajiri walimu wa mpaka wa civics kutoka nje ya nchi. Waziri yupo idara ya ukaguzi ipo. Hakuna jipya.
Waziri wa kilimo Mwigulu naona anapiga ziara tu mkoa baada ya mkoa. Matatizo ya kilimo bado hayana majawabu. Kuna vitu kama connection za masoko kwa wakulima haviitaji kusubiri bajeti kuu Waziri angeweza kuanza na hili kama kuna vingine anasubiri.
Wizara ya kazi, ata Waziri nimesahau tayari. Hizo recruitment agencies bado zinatesa waajiriwa huko kuna unyonyaji wa hatari na Waziri yupo tu anafanya ziara. Hakuna kulinda ajira za wazawa yalifanyika maigizo ya wiki mbili kiwanda cha Dangote na godown la wachina baada ya hapo ni business as usual Mavunde pumzi imekwisha.
Wizara ya mazingira inayoongozwa waziri anayesemekana ni smart sana mpaka sasa hatujaona innovation yoyote kutunza mazingira na kusimamia usafi. January anatuangusha nae.
Waziri wa mambo ya ndani. Kitwanga nafikiri anashindwa tu kusema kazi imemzidi uwezo. Uhamiaji huko ni rushwa kwenda mbele. Polisi wa barabarani ni mrija wa rushwa. Yani huyu ndio mpaka namuonea huruma.
Maghembe ni mtu aliyepewa wizara ya leo wakati yeye anaishi jana. Pale zaidi ya kukamata majangili sijui ana ubunifu gani kufanya utalii utishe Tanzania na Africa kwa ujumla.
Kigwangwala na Ummy wanajitahidi japo bado wameshindwa kuri address tatizo.
Kuna huyu Makame Mbalawa namuona kama nae mfuatiliaji hivi.
Nape siasa nyingi utendaji kisoda. Mara wasanii watalipwa mpaka leo kimya. Mara bongo movies watalindiwa kazi zao na tra kimyaaa. Mara TFF watatoza kwa electronic. Huko kwenye michezo ndio sioni chochote anachofanya.
Kwa kweli mawaziri wanaotakiwa wajipange haswa. Maana Magufuli amekuwa kama one man army mawaziri nao wanamshangaa badala ya kumsaidia.
Na kuna mawaziri wanaonekana kama wana uwezo wa kufanya makubwa ila tatizo sijajua ni nini mpaka nahisi kuna kamgomo baridi au hii aina mpya ya kuongoza hawajaipenda.
Ni bora ata ya Makonda anafanana na kasi ya Magufuli.
Uccm na Uchadema pembeni wenzangu mnawaonaje awa mawaziri.