mawaziri wa ccm sio wanasiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mawaziri wa ccm sio wanasiasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by toghocho, May 9, 2011.

 1. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  YA PROFESA MWAMFUPE NA USOMI WETU..
  Mnamo siku ya ijumaa kulikuwa na mhadhara “PUBLIC LECTURE’ ulioendeshwa na PROFESA aliyebobea katika sheria ISSA SHIVJI, bila kupunguza ukweli wala kuongeza chumvi mhadhara ule ulikuwa ni wa kuvutia na ulikuwa ni elimu na somo tosha kwetu sisi kwani tuliyokuwa hatujui,tuliyajua, tuliyodhani tunayajua ilhali hatuyajui nayo tuliyajua pia tuliyohisi hatujui ilhali tunajua tulipata uhakika ya kuwa tunayajua tena kwa ufasaha.
  Kila jambo linalofanyika lazima vioja na vijambo vijitokeze, katika mdahalo ule mambo mawili yalisikitisha naam mambo matatu yalifedhehesha, la kwanza ni la wahadhiri wa UDOM kuondoka , pili kutosikiliza na kuchangia utadhani wao hawaoni umuhimu wa suala lilimsafirisha mwenzao kutoka DAR ES SALAAM huku akiacha shughuli zake muhimu kuja kugawa darasa ambao wao hawajalitoa, na la tatu kauli yaPROFESA MWAMFUPE alipokuwa akihitimisha,kwa ufinyu wa karatasi hii naomba nisiongelee mambo mawili ya awali nijikite kwenye jambo la tatu.
  Kama tunavyojua kila mtu ana wajibu wa kujielimisha kadri awezavyo na kila mtu anao uhuru wa kutoa maoni na kusikilizwa ikiwa ni sanjari na kueleza zilizo fikira zake sahihi au sio sahihi, pia si vyema kuwabagua watu kwa itikadi wala falsafa zao, naamini PROFESA haya anayatambua, kitendo cha PROF.MWAMFUPE kutamka kuwa kuna mihadhara mingine ya namna ile itaendelea kufanyika chuoni huku akitoa angalizo kuwa baadhi ya watu tunofikiria kuwaalika hawawezi kuruhusiwa na chuo kuja kufanya mihadhara kama uliofanywa na ISSA shivji ,huku akishindwa kuwataja ni kina nani hawawezi kuruhusiwa, akili za kuambiwa siku zote changanya na zako nadhani hapa MWAMFUPE anataka kutuambia ya kuwa “akinya kuku kanya ila akinya bata atakuwa kaharisha”
  Endapo hoja ni watu kutoruhusiwa kwa kigezo kuwa wao ni wanasiasa, hebu tujiulize BENARD MEMBE ni kada wa CCM na mwenye vyeo kadha {kabla hajavuliwa gamba} aliweza kufika na kutoa mhadhara, PROF ANA TIBAIJUKA ni mwana CCM yeye naye aliruhusiwa kutoa mhadhara licha ya kuwa ni mwanasiasa hapa hawa kama ni kuku basi walikuwa wanakunya, ila bata akija ataharishaje hao ambao MWAMFUPE anachukua kipaz sauti na kusema kuwa hawawezi kuruhusiwa wanakasoro gani? Je! Huu si ukada,ubaguzi na udhalilishaji kwa watanzania wengine ambao wamejaliwa uwezo kuja kutoa mawazo yao na sisi kama jumuiya ya wasomi tuwapime!(kumbuka pia kuna maprofesa wa hapa UDOM wameenda kugombea ubunge CCM kwenye kura za maoni wametoswa Je wao si wanasiasa? )
  Popote pale duniani vyuo vikuu huheshimika kama CHEMICHEMI ya fikra pevu kupita midahalo na mihadhara yenye kugusa maisha ya watu wa chini ambao wao ni watu wanaolia ndani ya giza totoro, kwani serikali huwasikia ila haiwaoni, Rais OBAMA alipokuwa akifanya kampeni alikuwa akienda katika vyuo vikuu na kufanya midahalo na kupokea changamoto kutoka kwa wasomi, MWALIMU NYERERE alikuwa akipenda midahalo kwani mtu alikuwa akija kumtembelea alikuwa akimpeleka MLIMANI afanye mdahalo na vijana makini, mwaka 1995 katika kampeni za urais MREMA alienda MLIMANI na kubebwa huku NYERERE akiwakebehi kuwa watambeba ila watamchoka na kumwachia! Je! MWAMFUPE kwa nini asitumie busara kama hizi za NYERERE?
  Kiujumla masuala yaliyozungumzwa na shivji kama vile serikali mbovu, ugumu wa maisha, nchi kukosa dira, ubidhaifishaji na ubinafsishaji holela,matabaka ya walala hoi, walala hai, walala heri na ufisadi hivyo kuhitaji katiba mpya yanaweza kuzungumzwa na mwanafunzi wake Tundu Lisu, John Mnyika DR Slaa,Julius Mtatiro, MDEE, Hamad Rashid, John cheyo ila cha kushangaza ni kwamba mmja wapo kati ya hawa hawezi kuruhusiwa kwani yeye hawezi kunya kama waliotangulia yeye ataharisha! Huu ni ubaguzi wa kutisha, ukada, uoga,kukosa hoja na kuwa mtumwa wa fikra hili la MWAMFUPE ni changamoto kwetu wasomi. Tukumbuke kauli ya MWALIMU watu wote ni sawa na wote ni ndugu zangu na AFRIKA NI MOJA.
  Niandikie, nikosoe kupitia
  Mwitamwita77@yahoo.com
   
Loading...