figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,487
Heshima kwenu wakuu,
Hii Wizara imekuwa Mwiba kwa kila Mtu alokanyaga ndani kuiongoza. Haijamuacha salama.Leo nimeona niongelee hili swala ili kuweka kumbukumbu sawa. Ntaomba michango ya WanajamiiForums, ili kuboresha Uzi huu, ntakachofanya ntaadnika kile nilicho na uhakika nacho, Ntaweka orodha ya Mawaziri na Manaibu Waziri hapa. Kisha kwa wale Wazee wetu ntaomba watuambia Changamoto alizopata kila Waziri. Je Wizara iliwaacha salama? Hii Wizara nasikia haijawahi kumuacha mtu salama.
Huo ulikuwa ni Utangulizi. Kama Mnavyojua, hii Wizara imepitia katika mabadiliko Mbalimbali ya majina yake kama ifuatavyo;
1. 1961-1963 - Iliitwa Wizara ya Biashara, Madini na Nguvu za Umeme na Waziri wake aliitwa Waziri Bw. A. H. Jamal
2. 1964-1966 - Iliitwa Wizara ya Viwanda, Madini na Nguvu za Umeme na na Kila Mwaka Mawaziri walikuwa wanabadilishwa. Waziri Bw. A. K. E. Hanga (1964), Bw. J. S. Kasambala (1964 -1965) na Bw. A. Z. Nsilo Swai (1966) na katika wote hao, ni Mwaka 1964 tu ndo kulikuwa na naibu waziri ambaye aliitwa Naibu Bw. M. R. Kundya.
3. 1970 - Iliitwa Wizara ya Maji na Nguvu za Umeme na Waziri wake Waziri Bw. I. Elinawinga.
4. 1975 - Iliitwa Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Waziri Dkt. W. K. Chagula ambaye aliiongoza kuanzia 1975 hadi 1980 huku naibu waziri akiwa Bw. Mustafa C. Nyang’anyi.
5. 1980 - Iliitwa Wizara ya Maji na Nishati na Waziri alikuwa Bw. Alnoor Kassum huku naibu Waziri akiwa Bw. Edgar Maokola Majogo.
6. 1980- Ilibadilishwa tena jina na ikaitwa Wizara ya Madini huku Waziri akiwa Bw. John Samwel Malecela(1980-1982) na Bw. Jackson Makweta (1983) na Balozi Paul Bomani (1983-1984)
7. 1984 - Iliitwa Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Mawaziri Bw. Alnoor Kassum na Pius Y. Ng’wandu
8. 1985 - Iliitwa Wizara ya Nishati na Madini na Waziri walikuwa Bw. Alnoor Kassum huku manaibu wakiwa Manaibu wakiwa; Naibu Bw. Edgar Diones Maokola Majogo (1985 -1988) na Meja Jakaya Mrisho Kikwete (1988 - 1990).
9. 1990 - 1995 Iliitwa Wizara ya Maji, Nishati na Madini na Waziri alikuwa Mhe. Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete (1990-1995) na Jackson M. Makweta (1995) huku Manaibu Waziri wakiwa; Mhe. Ernest K. Nyanda (1990 - 1991) na Mhe. Joseph F. Mbwiliza (1991-1995).
10. 1995 hadi Sasa - Iliitwa Wizara ya Nishati na Madini Waziri Dkt. Waziri Dkt. William Shija (1995 – 1996),
=> Mhe. Dkt Abdallah Omari Kigoda (1996 – 2001),
=> Mhe. Edgar Diones Maokola Majogo (2002),
Naibu Mhe. Manju Msambya (2001 – 2002)
=> Mhe. Daniel N. Yona(2002 -2006),
Naibu Waziri Dkt. Ibrahim Said Msabaha (2002-2005)
=> Mhe. Dkt. Ibrahim Said Msabaha (2006-2007),
Naibu Waziri Mhe. Lawrence Kego Masha (2006)
Naibu Waziri Mhe. Bernad C. Membe (2006)
Naibu Waziri Mhe. William Mganga Ngeleja (2007)
=> Mhe. Nazir Mustafa Karamagi (2007-2008)
Naibu Waziri Mhe. William Mganga Ngeleja
=> Mhe. William Mganga Ngeleja (2008 –2012)
Mhe. Adam Kighoma Malima (2008-2012)
=> Prof. Sospeter Muhongo (2012 -2015)
Naibu Waziri Mhe. S. Masele na Mhe. G. Simbachawene
=> George Simbachawene (2015-2016)
Naibu Waziri Charles Mwijage
=> Prof. Sospeter Muhongo(2016-2017)
Naibu Waziri Dkt. Medard Kalemani.
Mwaka huu tunategemea ateuliwe Waziri Mwingine kuchukua nafasi ya Muhongo.
Wakuu, nini hasa kisa na Mkasa hadi Hii Wizara ikawa na vituko kiasi hiki?
Karibuni Kwa Michango yenu Wakuu.