neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
BAADA ya kuapishwa rasmi wakuu wa mikoa, makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu, wameahidi kila mmoja, kutekeleza ipasavyo majukumu yanayowakabili katika maeneo yao, ikiwemo kukabiliana na changamoto zinazowasumbua wananchi.
Rais John Magufuli jana aliwaapisha viongozi 21 aliowateua mwishoni mwa wiki kushika nyadhifa mbalimbali Ikulu, Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Jim Yonazi amesema, kwa kuwa mawasiliano ni uchumi, atahakikisha anashirikiana na watendaji wenzake kwenye wizara hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano salama wakati wote.
“Mawasiliano salama ni muhimu kwa uchumi wa nchi. Watu wanahitaji kuhakikishiwa usalama wao wanapofanya miamala ya kifedha kwa njia ya simu, wanapopiga simu au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa maneno; hivyo basi, kwa kushirikiana na wenzangu tutaweka juhudi za pamoja na kuwa wabunifu katika kufikia malengo hayo,” alieleza Dk Yonazi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti amesema atahakikisha tatizo la wahamiaji haramu halipati nafasi mkoani mwake licha ya mkoa huo kupakana na nchi kadhaa za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Gaguti, ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, alisema pamoja na mikakati mingine ya kimaendeleo aliyonayo, atatumia mbinu ya kiusalama aliyoitumia Kigoma ya nyumba kumi kumi katika kuwabaini wageni na wahamiaji haramu watakaojipenyeza kinyemela mkoani humo.
Amesema anatambua kwamba Mkoa wake unapakana na nchi za Uganda, Rwanda na Burundi, lakini atahakikisha Mkoa wake unabaki salama kwa kudhibiti wageni na wahamiaji haramu ambao hawafuati sheria za uhamiaji.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Kessy Maduka, amesema miongoni mwa mambo ambayo atayasimamia kwa nguvu zote ni pamoja na kusimamia ujenzi wa miundombinu itakayokidhi mahitaji ya maendeleo ya viwanda mkoani humo.
Maduka aliitaja baadhi ya miundombinu hiyo kuwa ni ujenzi wa miundombinu ya maji na barabara ambayo ni muhimu kwa ujenzi na maendeleo ya viwanda.
“Mambo mengine nitakayoyasimamia kwa karibu ni upimaji wa ardhi ili kujua aina ya udongo wa kila eneo unafaa kwa shughuli gani ya maendeleo kwa sababu tutahitaji kuanzisha kilimo cha mazao mapya ya biashara kama vile korosho, ufuta na alizeti, lakini pia nitasimamia ukusanyaji wa mapato kama Rais Magufuli alivyotuagiza,” amesema Maduka.
Kuhusu maendeleo ya mifugo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema kuwa moja ya mikakati yake ni kuhakikisha mifugo haitoroshwi nje ya nchi.
Profesa Elisante alisema kuwa Tanzania ina jumla ya ng’ombe milioni 30.5, mbuzi milioni 20, kuku wa kienyeji milioni 38.6, kuku wa kisasa milioni 36.6 na punda zaidi ya laki tano, hivyo wasiposimamiwa vizuri na wakaachwa watoroshwe nje ya nchi bila kulipiwa kodi, Serikali itakuwa inapoteza fedha nyingi.
Mambo mengine ambayo atayasimamia ni maendeleo ya viwanda vya mazao ya mifugo kama vile viwanda vya nyama, maziwa na ngozi, lakini pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wafugaji ili mifugo yao iwaletee maendeleo tofauti na ilivyo sasa.