Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 505
- 887
Kundi la mawakili zaidi ya 13 wakiongozwa na Wakili Mwandamizi Constantine Mutalemwa, wamemwakilisha Wakili Godfrey Mjuni Martin Basasingohe katika kesi ya kikatiba dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Mashitaka ya Umma (DPP), wakipinga uhalali wa sheria ya ulinzi wa mashahidi wakidai inaleta changamoto za haki na uwazi.
Kesi hiyo Na: 22482/2025 iliyofunguliwa Oktoba 1, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Mwanza inahoji kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) pamoja na Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi za mwaka 2025.
Kwa mujibu wa hoja za upande wa walalamikaji, sheria hiyo imekuwa ikiwaficha mashahidi badala ya kuwalinda. Mathalani, wanadai kuwa mtu anaweza kutoa ushahidi mara nyingi kwa majina tofauti ilhali ni mtu mmoja.
Jopo la majaji watatu linaloundwa na Jaji Fahamu Mtulya, Jaji K.S Kamana na Jaji W.M Chuma ndilo litakalosimamia shauri hilo. Kesi imepangwa kusikilizwa Oktoba 30, 2025 kwa ajili ya amri na maelekezo ya mahakama.