Mdanganywa
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 620
- 342
Sijui kama wengi mmeshagundua kwamba kuna tatizo kubwa sana la mawakili weledi hapa nchini. Wakili weledi ni yule ambaye ukimpa kesi anaielewa kiasi kwamba ukishamaliza kumpa maelezo wewe unaendelea na shughuli zako unasubiri aendelee na kesi, na huna haja kabisa ya kufika mahakamani.
Lakini mawakili wetu wako hivi. Kwanza wana tamaa ya hela hivyo wanakuwa na kesi nyingi. Hii inawasababisha wawe na summons nyingi na kesi yako inaishia kuchelewa tena wakati mwingi si kwa sababu ya hakimu, bali kwa sabababu ya wakili wako.
Mara atakuambia ana kesi High Court au Appeal court hivyo ya kwako iko katika subordinate court na hakimu akiona hivi anaahirisha hata kwa miezi miwili, wakili wako hajali. Anajali alichopata kule High Court na wewe pia kakuvuna.
Lakini jingine ni kwamba mawakili hawasomi kabisa contents za kesi yaani "substansively part" ya kesi yao. Hii ni sehemu ya msingi na ndiyo iliyokufanya ukafungua kesi, yaani hoja za kesi au malalamiko ya msingi.
Mwaka juzi nilikaa na wakili wangu na kesi ilionekana ni complicated na akawa hana muda wa kuisoma. Alichofanya na wanachofanya ikiwa hivyo, mawakili wanajikita kwenye kitu wanachoita "technicalities", yaani kuvizia makosa ya kiutaratibu ambayo adui yako ameyafanya au atayafanya mahakamani.
Hapa ndipo mawakili wanajikita karibu wote, kwa sababu kwa vile wanaingia kila siku mahakamani basi wala hahitaji maelezo yako, anajua pa kuvizia. Na kesi nyingi unazosikia mtu mlalamikaji kashindwa ni katika hili na wala si hoja za kesi.
Sasa kama mlalamikaji huna wakili basi hapa ndiyo ngoma, na ndicho wengi kinachowashinda na kuwaogopesha kwenda mahakamani.
Ukiangalia kesi ya Zitto Kabwe dhidi ya CHADEMA kuhusu kutojadili uanachama wake, Zitto si kwamba alishindwa ile kesi. Zitto alipigwa technicality kwa maana ya kwamba aliipeleka kesi kwenye registry isiyotakiwa.
Hii maana yake ni nini? Maana yake Zitto hakufikia hatua ya "substansive" yaani hakufika hatua ya kuanza kueleza malalamiko yake. Kama ingefika huenda Zitto angeshinda kwa hoja zake.
Naomba mnaokurupuka msianze kushambulia kwa matusi mkidhani mimi ni mshabiki wa Zitto, hapa ninaeleza tatizo la msingi na Zitto ni mfano mmoja public ingawa mifano ipo mingi.
Hata kesi ya "mita 200" pale wana-CHADEMA ni kama walihurumiwa tu. Kama utakumbuka yule mama Kibatala na wakili wakili wake walifungua kesi kumshtaki Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Hatupendi tu kusema sana, hili lilikuwa kosa kubwa kufanywa na wataalamu wa sheria. Siku zote anayeshtakiwa ni mtendaji wa taasisi. Mwenyekiti wa Tume si mtendaji (executive). Hivyo, naona Mahakama ilishajua serikali itashinda kesi ile na hivyo wangetumia technicality kama walivyotumia kwa Zitto, umma ungepiga kelele za ajabu ukizingatia ilikuwa imebaki wiki moja tu.
kama mnakumbuka, Kibatala (Ms.) aliambiwa arudie kuandika na amshitaki MKurugenzi wa uchaguzi. Huu tayari ulikuwa msamaha wa technicality na hata Zitto angeupata mapema msamaha huu leo hadithi ya siasa ingekuwa tofauti.
Kwa asiyejua technicality nadhani ameshajua, sasa niendelee. Ngoma ya techincality iko kama adui yako hana kosa hata moja la technicality. Hapo ndipo mawakili hudoda. KWa sababu hata kama kesi ni complicated vipi unatakiwa uisome na uielewe.
Sasa mawakili wetu kama zilivyo proffessions zingine, hawasomi na wana kesi nyingi. Tembelea sehemu za mahakama uone vituko vyao. Kesi inaanza dakika kumi zijazo utaona wakili na mteja wake eti ndiyo wanvutana pembeni na wanaandika hoja za kuelezana au kuulizana watakapoingia ndani ya courtroom!
Hivi hizi dakika kumi zitasaidia nini kujua kesi tena inayohusu process ya miaka hata mitatu?! Tena wengine si dakika kumi, bali hata dakika mbili!
Hii ni janga na balaa. Ni kutokana na mfumo wa kiuwakili kuvizia sana "technicalities" kuliko kujikita kwenye "substansive".
Mwaka jana majaji walilijadili hili na kusem ni moja ya janga linalochelewesha kesi za uchaguzi. Hebu ona hata mapingamizi mengine, mtu kasahau herufi mbili za jina lake kama pale Sengerema mtu anaweka pingamizi eti mgombea hajui kusoma wa sababua ameshidnwa kuandika hata jina lake.
Nashukuru Jaji Lubuva alitupilia mbali mapingamizi haya na hilo likawa ni somo kwa wanaovizia technicalities.
Hivyo mdau, kama una kesi, basi jikite wewe mweyewe walau kujua msingi mzima. Ukiona mambo ya techicalities unayaogopa basi weka wazi na ieleze mahakama kwamba wewe si mtaalamu wa sheria na kukosa wakili si kwamba hutapata haki. Mahakama italiona hilo. Mimi nimepata uzoefu baada ya kutembelea maonyesho ya wiki ya Sheria.
Naomba mchangie kwa ukweli tuokoe janga la kukosa haki.
Wenu mdau.