Mawakili wasomi Tanzania

Jabman

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
1,005
1,337
Napenda tuwajue mawakili wasomi kuwahi kutokea Tanzania

1. Masumbuko Lamwai

Huyu bwana ni bonge la mwanasheria kuwahi kutokea. Aliwahi kumwambia Waziri mmama mmoja kuwa ni Malaya. Yule waziri alipaniki na kuanza kutoa matusi mbele ya jaji.

Katika kuthibitisha umalaya wake, Wakili Lamwai alitoa picha za watoto wa mama yule watatu na picha za baba wa watoto wale yaani kila mtoto na babaye. Waziri alificha uso kwa aibu.

Lamwai enzi hizo alikuwa upinzani yaani NCCR-Mageuzi. Sijui kwa sasa aliko.

2. Tundu A. M. Lissu

Bwana huyu ni kiboko. Inasemekana ni mtaalamu sana wa kuwachanganya mahasimu wake kwa maswali ya mitego kiasi kwamba hasimu bila kujua anajikuta anakuwa shahidi wa Tundu.

Inasemekana hajawahi kushindwa kesi labda watumie nguvu ila hoja.

3. Peter Kibatala

Huyu ni mtaalamu wa kutafisiri sheria kiasi kwamba hata Jaji angependa kusikia sheria ikitafisiriwa na huyu Wakili ili na yeye ajifunze.

Naomba uongezee kwa kujenga siyo kubomoa.
 
Tundu A. M. Lissu....Bwana huyu ni kiboko. Inasemekana ni mtaalamu sana wa kuwachanganya mahasimu wake kwa maswali ya mitego kiasi kwamba hasimu bila kujua anajikuta anakuwa shahidi wa Tundu..

Huyu jamaa hata akiuliza swali la kawaida tu, akili ya muulizwa swali inadart huku na kule kujaribu kugundua mtego uliomo humo. Sometimes it is fun kufuatilia interrogations na cross-examinations zake.
 
Hao Mawakili Wasomi hawana tofauti na ambao hukuwataja. Isipokuwa ni kwamba, wao hao ni maarufu kupitia media. Mkuu, ni vyema ukaheshimu kila Wakili kwakuwa kila mmoja ana uwezo wake wa kipekee katika nyanja fulanifulani za uga wa sheria. Huwezi kujua vyote na huwezi kutojua chochote
 
Sahihi mawakili wanajuana wenyewe.....hao layman ...hawajui chochote zaidi ya ushabiki
 
Mimi ninachojua mawakili wore ni wasomi wazuri, tatizo wengine hutanguliza maslahi binafsi badala ya ukweli, na wengine ni wazito kutafsiri sheria zenyewe mbele za Mahakama .

Hao uliowataja ni mfano mzuri wa wakili kuwajibika kwa taaluma yao.
Neno wakili msomi lina maana gani?......au kuna na uwakili wa heshima?......
 
Neno wakili msomi lina maana gani?......au kuna na uwakili wa heshima?......
Kama nilivyosema katika hoja hii hapo juu ni kuwa mawakili wote ni wasomi na wamefuzu lakini wengine kwa maslahi binafsi wanashindwa kuonyesha ueledi wao
 
Wameandika nini? angalau maandishi ya SHIVJI, PETERMAINA, KABUDI, MWAKYEMBE, SHAHIDI, N.K Tunayaona je ! hawa hata kagazeti walichoandika sijawahi kusikia
 
Labda ndio unao wajua wewe au kwa itikadi yako lakini kuna wakongwe kina majura magafu ndyanabo kaganda nk halafu umesahau lissu alishindwa kesi ya ubunge ya wenje
 
Napenda tuwajue mawakili wasomi kuwahi kutokea Tanzania

1. Masumbuko Lamwai

Huyu bwana ni bonge la mwanasheria kuwahi kutokea. Aliwahi kumwambia Waziri mmama mmoja kuwa ni Malaya. Yule waziri alipaniki na kuanza kutoa matusi mbele ya jaji.

Katika kuthibitisha umalaya wake, Wakili Lamwai alitoa picha za watoto wa mama yule watatu na picha za baba wa watoto wale yaani kila mtoto na babaye. Waziri alificha uso kwa aibu.

Lamwai enzi hizo alikuwa upinzani yaani NCCR-Mageuzi. Sijui kwa sasa aliko.

2. Tundu A. M. Lissu

Bwana huyu ni kiboko. Inasemekana ni mtaalamu sana wa kuwachanganya mahasimu wake kwa maswali ya mitego kiasi kwamba hasimu bila kujua anajikuta anakuwa shahidi wa Tundu.

Inasemekana hajawahi kushindwa kesi labda watumie nguvu ila hoja.

3. Peter Kibatala

Huyu ni mtaalamu wa kutafisiri sheria kiasi kwamba hata Jaji angependa kusikia sheria ikitafisiriwa na huyu Wakili ili na yeye ajifunze.

Naomba uongezee kwa kujenga siyo kubomoa.

Ungesema tu kwanza mimi ni mwanachama wa Chadema naomba kuwasilisha. Yani kweli unaacha kusema wakina shivji unaanza na lisu na kibatala uliowajuavkupitia magazeti. Du huruma sana. Hata mkeo unayelala naye kila siku huwezi mwekea dhamana. Wameandika nini. Mana kila wakili ana kesi zake ngumu na za maana. We unaleta mbwembwe ahhhh please omba radhi kwa mkeo
 
Back
Top Bottom