Mawakala wa Forodha Mpakani Namanga Hapatoshi,waziri Mkuu Atajwa

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Chama cha mawakala wa forodha( TAFFA) Mpakani Namanga,wilayani Longido, wamemwomba Waziri mkuu, Kassimu Majaliwa kuingilia kati mgogoro kati yao na wakala wa vipimo (WMA) unaowalazimisha kulipia tozo mpya inayotozwa kwa kila bidhaa badala ya kutumia utaratibu wa awali wa kulipia tozo kwa mzigo wote.


Wamesema hawapo tayari kufanya kazi na wakala hao hadi hapo watakapo onyeshwa hiyo sheria mpya ambayo wanalazimishwa kuitekeleza bila kuwepo kwa mwongozo wowote kutoka serikalini kitendo ambacho kinawaumiza zaidi.


Msimamo huo waliutoa Jana kwenye mkutano wao uliokuwa ukiongozwa na mwenyekiti wao, Ismail Kilas uliofanyika eneo hilo la Namanga, wilayani Longido,Mkoani hapa.


Mawakala hao walisema kuwa, walikuwa wakitumia sheria ya zamani ya mwaka 2016 ambayo walikuwa wakilipia asilimia 0.2 ya thamani ya mzigo ambapo kiwango cha chini cha malipo ilikuwa ni sh, 100,000 kwa mzigo.


Walisema wanachopinga ni wakala wa vipimo kuamua kuwatoza malipo ya shilingi laki moja kwa kila aina ya bidhaa (item ) badala ya mzigo mzima Kama sheria inavyoelekeza .


Naye Meneja wa tawi wa kampuni ya EDPAC ,Wilson Kazen alisema kuwa, kwa sasa hivi hawapo tayari tena kufanya shughuli yoyote bila kupata muongozo wa sheria mpya inayowalazimu wao kutumia utaratibu mpya wa kulipa tozo ya laki moja kwa kila bidhaa badala ya mzigo Kama utaratibu wa awali.


IMG_20190527_113912.jpeg
IMG_20190527_111022.jpeg
IMG_20190527_124013.jpeg
 
Tozo lukuki imekua kero sana hapo kuna TRA(vat) Kuna Road Toll Kuna Atomic Energy kuna TBS kuna TFDA kuna WMA kodi zote hizo mzigo wa chakula kama chumvi tuu
 
Tozo lukuki imekua kero sana hapo kuna TRA(vat) Kuna Road Toll Kuna Atomic Energy kuna TBS kuna TFDA kuna WMA kodi zote hizo mzigo wa chakula kama chumvi tuu
Hata viwanda vinatozwa hivyo, sidhani kama tutafika kwenye uchumi wa kati, ni ngumu sana, wimbo wa Tanzania ya viwanda haupo tena umekata
 
Back
Top Bottom