Mawakala wa CHADEMA wapigwa stop

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Mawakala wa CHADEMA katika uchaguzi Arumeru Mashariki wamezuiwa kuingia ndani ya vituo vya kupigia kura kwa zaidi ya saa nzima.

Joshua Nassari akifanya mahojiano na Antony Joseph wa Radio WAPO saa 2:27 asb alisema "nimezunguka vituo 6 kote walikuwa wanazuiliwa hadi nilipofika. Nipo ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi naingia ili anipe maelezo kwa nini imekuwa hivi"

Source: Radio WAPO

My take: CCM nchi si yenu peke yenu.
 
Mkuu hii habari ni ya ukweli, nami nimesikia kupitia wapo radio mida ya saa 2 na kitu, ni ya kweli kabisa nasari kaojiwa na anton joseph wa wapo radion akasema anafuatilia, na kaaidi kueleza tena
 
lu-buva...lu-sinde,majina ya wanaccm huwa yanafanana hadi matendo!
 
Nmetoka kuongea na Nassari muda c mrefu anasema alikua anatania leo ni siku ya wajinga, mawakala wake wote wapo vituoni
 
Nmetoka kuongea na Nassari muda c mrefu anasema alikua anatania leo ni siku ya wajinga, mawakala wake wote wapo vituoni

usifanye upuuzi ktk vitu vinavyoamua mustakabali wa maisha ya watu.

Hata kama wewe unalipwa kwa upuuzi huu, kwingind nyamaza kimya.
 
Nmetoka kuongea na Nassari muda c mrefu anasema alikua anatania leo ni siku ya wajinga, mawakala wake wote wapo vituoni
Wewe nawe ni Mpumbavu kabisa kama huna jambo la msingi kaa kimya waachie wengine wachangie
 
nmetoka kuongea na nassari muda c mrefu anasema alikua anatania leo ni siku ya wajinga, mawakala wake wote wapo vituoni

be serious mkuu wajua aya masuala ni muhimu katika mustakabali pia atma ya maisha ya watu wa arumeru na watanzania kwa ujumla, i think you better keep quiet au peleka masiala yako uko fb wanakusubili
 
be serious mkuu wajua aya masuala ni muhimu katika mustakabali pia atma ya maisha ya watu wa arumeru na watanzania kwa ujumla, i think you better keep quiet au peleka masiala yako uko fb wanakusubili

Well said!!
 
2weni serious kidogo wadau wa JF as kwa ss 2lioko mbali twawategemeeni nyie ndio mtuhabarishe pasipo masihara wala mzaha juu ya hayo yaendeleayo uko
 
wanawazuia ili waweke mambo sawa?

Ni kweli. Kumzuia wakala hata kwa saa moja, "kura za maruhani" hata 100 zinaweza kudumbukizwa. Jambo hili ni hatari. Ni hatari kwa usalama wa wananchi, na mustakabali wa Taifa.

Akipatikana mbunge mbovu atachangia kutengeneza sheria mbovu. Tutakuwa na Taifa bovu.

CCM ni janga, Tume ya Uchaguzi ni janga zao la janga.
 
2weni serious kidogo wadau wa JF as kwa ss 2lioko mbali twawategemeeni nyie ndio mtuhabarishe pasipo masihara wala mzaha juu ya hayo yaendeleayo uko

Chumvichumvi wako watu wenye kuleta masikhara na wako watu makini. Siko katika kundi la kwanza. Wako wenye kuleta hoja za kitoto hao ndiyo wenye kuharibu ile heshima ya JF ambapo mtu ulikuwa unasema; how can a day pass without visiting JF? OR How can I live without JF?
 
Back
Top Bottom