Mawakala na Wananchi kwa Ujumla popote mlipo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawakala na Wananchi kwa Ujumla popote mlipo

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwiba, Oct 30, 2010.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Usiku wa leo na mchana wa kesho ni siku ambayo CCM inapitisha na itapitisha unyama wa aina yake wa kutumia hila zao walizozitayarisha kwa ajili ya kupora uchaguzi.

  Hivyo wananchi wale wote ambao wapo karibu na maeneo ya vituo wawe macho na hali yeyote ngeni itakayojitokeza katika vituo hivyo ,kwani Zanzibar hivi sasa wamegundua mbinu mbalimbali na wamezizima ,yaani WaZanzibar hapa niandikapo onyo hili wapo macho na wanalinda vituo vyote na mpaka pale ambapo masanduku yamefikia basi wanalinda na kurekodi nyendo zote na wapo tayari kwa kumhoji yeyite yule anaeingia au kutoka katika vituo hivyo.

  Kwa upande wa Tanganyika ambako imegundulika ni rahisi walinzi kurubunika inatakiwa wawepo zaidi ya walinzi au raia wakawaida wajumuishwe katika ulinzi huo baada ya kuwaachia watu wawili au watatu kukiwakilisha Chama ,watu wachache ni rahisi kurubunia ,inasemekana laki moja au chini ya hapo inaweza kutumika kumrubuni mlinzi wa upinzani na kuwacha CCM wafanye watakavyo kwani hata Kikwete amegusia kwa mbali na kusikika akisema ni taabu kuiba lakini na mawakala nao(wenu)wasikubali kuambiwa nenda ukapate soda huku akitiliwa laki mbili mkononi eti akapate chai na baridi kumbe huwa anaondolewa kijanja ili watu wamalize kazi kwa mwendo na kasi ya ajabu.

  Ulinzi wa vituo ulitakiwa uwanze mara moja baada ya karatasi za kupigia kura kuwasili. MpoooH ,basi msije kuachwa kwenye milango mkilinda mchana kumbe kazi imefanywa usiku huu ,leo asilale mtu na ukimaliza kusoma hapa pigia simu kila kiongozi wako unaemjua umjulishe mambo na utekaji unafanyika usiku huu.:israel:
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Misururu ni mirefu wananchi wakisubiri kufunguliwa kwa vituo. baadhi ya wapiga kura wa ccm wanaonekana mifuko imetuna ,huenda ikawa ni kura zilizokwishapigwa watatumia nafasi kuzitumbukiza kwenye vituturi ,eti mpiga kura atakuwa anaonekana miguu tu !!!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Maneno ya Kikwete...."Lakini kila chama kinakuwa na wawakilishi hapo. Wakishamaliza kila chama kinaondoka na nakala yake, kabla ya msimamizi kwenda kutangaza matokeo. Baadaye msimamizi anapeleka Tume, ambayo hujumlisha na vyama vyote vinakuwapo," alisema. Kutokana na hali hiyo, alisema dawa pekee ya kudhibiti hali hiyo, ni kwa vyama vya siasa kuhakikisha vinaweka mawakala makini wasioweza kudanganywa na kutelekeza kituo na hivyo kutoa mwanya wa kura za wagombea wao kuibwa.
  "Kwamba, (wakala akaambiwa), we bwana nenda kanywe soda. Anaweza kwenda kunywa soda, huku wenzake wanachakachua," alisema Rais Kikwete na kusababisha kicheko kutoka kwa washiriki wa mdahalo huo. "Lakini haiwezekani. Labda mawakala wawe wamekubaliana kwamba, Kikwete awe mshindi. Twende pale (kwenye vituo vya kupigia kura) tukasimamie, vinginevyo tunawatia watu hofu tu," alisema.
   
Loading...