Mauzo ya Nje (Export) Yaporomoka Kwa Sh. 608 Billion!!!

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
13,495
29,859
Wakati kipaumbele cha serikali iliyopo tangia wakati wa kampeni ilikuwa ni Tanzania ya Viwanda, Gazeti la The Citizen linaripoti kwamba Mauzo ya Nje yameshuka kwa Sh. 607.5 Billion; hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa Ripoti ya BoT

Pamoja na yote hayo, Gazeti la The Citizen limemnukuu Waziri wa Viwanda na Biaashara Bwana Charles Mwijage akisema hilo ni jambo la kawaida... kwamba, ni kawaida kuona mauzo ya nje yakishuka na wakati mwingine yakipanda!!

Lakini pamoja na Mwijage kusema hilo ni jambo la kawaida, takwimu zinaonesha kwamba, thamani ya bidhaa za viwandani zilizouzwa nje mwaka 2012 zilifikia $ 861million (takribani Sh. 1.1 Trillion kwa sasa), na mwaka 2012 mauzo yalikuwwa $1.037 Billion (takribani 2.2 Trillion), mwaka 2014 yalifikia $ 1.23 Billio n (2.6 Trillion), mwaka 2015 $1.36 Billion (Trillion 2.9) lakini mwaka jana yameshuka kutoka $1.36 Billion mwaka 2015 hadi $ 1.09 (Trillion 2.3)!!!

Source: The Citizen.
 
Serikali inahitaji ku boost economy ya nchi na ku stimulate njia kuu za uchumi na kuondoa vikwazo vya hovyo kwa wawekezaji na wafanyabiashara nchini wawekeze zaidi ktk kilimo kikubwa na cha kisasa lkn pia kuhimiza processesing industries
 
Msitusumbue siye tupo kwenye kujenga viwanda vya kukimbizana na wapinzani,subiri tukimalizana na wapinzani ndiyo mtuulize.

Halafu huwa sijaribiwi
 
Msitusumbue siye tupo kwenye kujenga viwanda vya kukimbizana na wapinzani,subiri tukimalizana na wapinzani ndiyo mtuulize.

Halafu huwa sijaribiwi
Mi kanichosha huyo Mwijage!! Yaani anaona kabisa from 2011 to 2015 kila mwaka export inapanda! Wao wanaingia madarakani tu; exports zinashuka hadi value equivalent na ile ya 2012 lakini anaona sawa tu!!!
 
Taarifa za mjengoni na nyumba ya takwimu uchumi unakua kwa kasi, kiasi cha kudai katika ziara moja ya mkuu wa mawaziri tuisifu awamu hii. Kwani hawakuweza kupika na hizi namba?
Yutayaona mengi miaka minne ijayo.
 
hayawezi kupanda kwa sababu hatuna mkakati madhubuti wa uchumi

tuendelee kukamata kina manji kwanza waliomuunga mkono lowassa.
 
Taarifa za mjengoni na nyumba ya takwimu uchumi unakua kwa kasi, kiasi cha kudai katika ziara moja ya mkuu wa mawaziri tuisifu awamu hii. Kwani hawakuweza kupika na hizi namba?
Yutayaona mengi miaka minne ijayo.
Ndo washahangaika sana hapo kupika imeshindikana kwahiyo solution inakuwa kutoa ripoti kimya kimya!!! Mauzo yangepanda hapo; ungekuta kuna bonge la press conference hadi kila mmoja anajua!! Na ndo bahati mbaya watu tupo busy na Makonda; nice timing!
 
Mi kanichosha huyo Mwijage!! Yaani anaona kabisa from 2011 to 2015 kila mwaka export inapanda! Wao wanaingia madarakani tu; exports zinashuka hadi value equivalent na ile ya 2012 lakini anaona sawa tu!!!
hana aibu kabisa au ndo anatetea unga wake...

hivi huyu waziri uchumi kasomea wapi jamani?!!

maana hata sisi tuliosoma kwa Mr.Evans tunaona kabisa hali mbaya

naisikitikia hii nchii!

yaani tuna viongozi wadhaifu mno wasio na uthubutu kama majoka ya kibisa
 
Hata kama awe amesomea Harvard, ameshathibitisha kwamba hamnazo!!
 
Sasa hivi sifuatilii tena habari za uchumi wa nchi hii. leo bot uchumi umeshuka kesho waziri wa fedha uchumi umeimarika.
 
hii nchi wengi wa tz ni wajinga ndo maana Leo hii unga unauzwa elf2 per kg hawalalamiki,kiroba elf37 mpk elf43 still tuko kimyaaa
Hata kama awe amesomea Harvard, ameshathibitisha kwamba hamnazo!!
work done sawa na sifuri
Kwa takwimu hizi, ina maana pesa zooooooooooote wanazodai wameziokoa huku na kule zina-compansate hapa na matokeo yake tunakuwa tumerudi pale pale!!
 
hii nchi wengi wa tz ni wajinga ndo maana Leo hii unga unauzwa elf2 per kg hawalalamiki,kiroba elf37 mpk elf43 still tuko kimyaaa

work done sawa na sifuri
Na ndio maana kuna siku nilieleza kwa urefu hapa... kwamba watu wana-take advantage baada ya kuona dunia ina wajinga wengi zaidi kuliko werevu!!!

Utashangaa pamoja na takwimu na real life kwenda kinyume nyume bado kuna watu wanaamini uchumi unakua na kila siku anashangilia!
 
Kwahiyo hoja yako hasa ni ipi manake heading na maelezo vipo wazi kwamba kilichoshuka ni exports!
Nataka kuelewa maana habari iko jumla jumla sana. Tulichopunguza kinatuhusu sasa kuna ubaya gani kukielewa?
 
Na ndio maana kuna siku nilieleza kwa urefu hapa... kwamba watu wana-take advantage baada ya kuona dunia ina wajinga wengi zaidi kuliko werevu!!!

Utashangaa pamoja na takwimu na real life kwenda kinyume nyume bado kuna watu wanaamini uchumi unakua na kila siku anashangilia!
kuna majitu kipimo cha uchumi kukua ni kitendo cha baadhi ya watu walikua 'high life'kufulia au kuyumba kiuchumi...hvyo anguko la baadhi ya watu kwao ni neema kubwa sana

nasikikitika sana nikiona hyo hali yaani mtu anashangalia kabisa eti'alikua ana gari nne sasa hivi ana moja tu"

wabongo baadhi akili zetu bwana!!
 
Nataka kuelewa maana habari iko jumla jumla sana. Tulichopunguza kinatuhusu sasa kuna ubaya gani kukielewa?
Sio kuna ubaya kuelewa tatizo ni kwamba sijaelewa concern yako ni ipi manake ingawaje umesema habari ipo jumla jumla lakini kimsingi haipo kijumla jumla!! Ipo very specific maanake imesema wazi kwamba thamani ya export imeshuka!

Kwavile kushuka ni relative term, ndo maana nikaamua kuweka hadi value of exports kwa miaka iliyopita kuonesha tulikuwa wapi back then!! Na sidhani kama kwenye export decline kuna uhusiano na maamuzi binafsi, nikijaribu kukuelewa hapo uliposema "tulichopunguza...!" As if tumeamua wenyewe kushuka by hiyo figure!!!

Ingekuwa ni decline in commodity export huenda tungehusisha na unstable world market lakini decline in manufactured goods ni ama production in manufacturing sector imeshuka or else, bidhaa zetu zimekuwa less competitive kwenye masoko ya nje!!!

Decline in export haijapata kuwa jambo jema hata siku moja unless iwe proved kwamba kuna soko la kutosha nyumbani na hivyo kutokuwa na maana yoyote ya ku-export jambo ambalo nalo linatia shaka kwa sababu, US na China pamoja na kuwa na soko kubwa ndani bado kila mmoja siku zote na wakati wote atapigana kuongeza export na kupunguza imports!
 
Back
Top Bottom