Takwimu zilizotolewa na benki kuu ya Tanzania zinasema mauzo ya Bidhaa za viwandani kwenda nje ya nchi yameshuka kutoka dola bilioni 1.36 mpaka bilioni 1.09.
Waziri wa viwanda amesema mpomoko huo unaakisi dunia ilivyo sasa kwa upungufu wa mzunguko wa fedha uliopo. Mwijage ameendelea kusema ajenda ya Tanzania ya viwanda ipo palepale na kilichotokea ni kitu cha kawaida kwani takwimu za uuzaji bidhaa nje hupanda na kushuka kulingana na hali ya wakati huo.