Mmmh,wala si madogo,mme gombana kisa nini? yeye ndio amekukosea au wewe? na hilo kosa unahisi unastahili kufanyiwa unavyofanyiwa? au anajua kua kwake umeoza umeroa rovyo rovyo kwa penzi lake ndio mana anakufanyia vitimbi vya kusudi?
sikwambi hakufai ila jiulize mara ngapi utakua unakosa raha? kwa kosa gani ulofanya lisosamehewa? na ningekua wewe hiyo simu moja na sms ya apology 1 baada ya hapo ndio angeniona kama kituo cha Police......
Naombeni maombi yenu, mpenzi wangu nampenda sana lakini tumegombana na ni wiki ya pili saivi hatuna maelewano, nampigia simu hapokei, msg hajibu. Hapa nipo kazini nimepigia kwa simu ya ofisini baada ya kugundua ni mimi ya ofisini saiv hapokei. Naumia sana sijui kwa nini mimi tu maumivu haya yananipta.
Najiona kama sina haki ya kupendwa, Mungu nisaidie kipindi hiki kinipite salama.
Asante kwa kunitia moyo, yaani nimekua nikikosea nakuwa mwepesi kuomba msamaha ila yeye akinikosea nikimwambia hapo umenikwaza hataki anasema yeye ndo mwanaume sasa mimi naumia maana nakwazika, ameamua tuachane kwa sababu kuwa sitaki kuwa chini yake. Naumia sana basi tu
nini hasa mlichogombania? nataka kupima uzito wa kosa na adhabu anayoku punish.
ni mambo mengi, lakini kikubwa tunagombana kisa hataki tukapime afya, akikosea hataki nimrekebishe ila ikitokea kwa bahati mbaya nimekosea hata kidogo tu au msg nmemjibu tofauti basi anasema tuachane eti mimi sitaki kuwa chini yake.
Kingine yeye ni mwanaume lakini hataki sex hata nikimwambia ansema sio priority yake,nikimuliza kwa nia nzuri tu isije ukawa una tatzo. Basi ndo amezira eti nmemtukana. Yaani mpaka naihi nae kwa kuogopa badala ya kufurahi.
Pamoja na hayo yote nampenda sana naumia sana,
tatizo ni nini? kama amuna sababu ya msingi ya nyie kufanyiana hivyo ma dear just do other thing achana nae..... hivi kuchuniana inakuwaje sijawahi fanya huo mchezo aiseeeeeeee. mimi ningekuwa nimeshajichanganya na kuachana nae
Pole sana hayo ndo mapenzi.
Dont take love too serious.
Mimi nimeacha chukua mapenzi serious maana yangeniua bure wakati maisha matamu.
Watu wengine wakishajua weakness yako ni upendo kwake baaasi jua atakuwa anakusumbua tu