Maumivu ya kichwa kupitiliza

Maumivu ya kichwa kupitiliza

mugoda18

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Posts
134
Reaction score
94
Wanajukwaa naomba msaada wenu, nimekuwa nikiumwa na kichwa kwa muda mrefu ila sasa kimezidi naomba mnisaidie itakuwa shida nini???
 
Asante, ila sio mda nilienda hospital moja ya vitu nilipimwa ilikuwa presha nikaambiwa ipo normal
Ok. Kapime hospital ya maana, kichwa ni mtoa taarifa tu kuwa kuna tatizo
 
Inaweza kuwa ni migraine kuumwa kichwa mfululizo
Au pengine inaweza kuwa ni mfumo katika mishipa ya damu
Pia kama ni maumivu makali sana inaweza kuwa brain tumour ila kwa uchunguzi zaidi unahitaji ukapimwe kabla ya yote hayo
 
Kuna shida tumboni nenda kapime typhoid ukiona kichwa kinauma jua shida imeanzia tumboni
 
Nashukuru ntafanya checkup
 
Kuna shida tumboni nenda kapime typhoid ukiona kichwa kinauma jua shida imeanzia tumboni

Last month nilikutwa na UTI wakanipa dawa ambazo walisema zinatibu na typhoid !! Sijajua kama imerud
 
Wanajukwaa naomba msaada wenu, nimekuwa nikiumwa na kichwa kwa muda mrefu ila sasa kimezidi naomba mnisaidie itakuwa shida nini???

MAUMIVU YA KICHWA.jpg

KUUMWA NA KICHWA
Dalili za maumivu ya kichwa zinaweza kumsaidia daktari wako ajue nini kinachosababisha maumivu hayo hatimaye kujua matibabu yako yatakuwa vipi.
Hata hivyo, ili mhudumu wa afya aweze kutambua ni aina ipi haswa ya maumivu ya kichwa inakusumbua na aweze kutoa tiba sahihi, ni muhimu sana kwa mgonjwa kuweza kueleza kwa ufasaha na usahihi vile anavyojisikia na kujibu maswali atakayoulizwa na mtoa huduma kwa usahihi.Pia, mhudumu wa afya anahitajika kuwa na utaalamu na uzoefu wa kutosha ili aweze kutambua tatizo linalosababisha maumivu ya kichwa ya mgonjwa. Pamoja na hayo, bado inaweza kuwa ngumu kwa mhudumu wa afya kuweza kung’amua tatizo linalokusababishia haswa maumivu ya kichwa.
Maumivu ya kichwa mara nyingi huwa hakusababishwi na sababu za hatari sana au hakumaaanishi kuna ugonjwa mbaya sana unaendelea mwilini, lakini wakati mwingine kunaweza kumaanisha kuna ugonjwa wa hatari mwilini unaohitaji matibabu ya haraka. Kuuma kwa kichwa kunaweza kugawanywa katika makundi kutokana na visababishi kama ifuatavyo.

I.Maumivu ya kichwa ya awali (primary headache)
maumivu haya husababishwa na kuongezeka kwa hisia za maumivu katika viungo vinavyotaambua maumivu ndani ya ubongo. Maumivu haya ya awali hayamaanishi kuwa kuna ugonjwa unaendelea. Mfumo wa kemikali katika ubongo, mishipa ya fahamu, mishipa ya damu ya nje ya fuvu ama misuli ya shingo na kichwa huchangia katika kusababisha maumivu ya kichwa ya awali. Baadhi ya watu wamebeba vinasaba vinavyosababisha wao kupata maumivu haya maishani mwao. Aina hii ya maumivu ya kichwa nayo imegawanyika katika makundi makubwa mawili;

A:MAUMIVU YA KICHWA YA MIGRAINE (MIGRAINE HEADACHE)
-Aina hii ya maumivu ya kichwa ya awali diyo ambayo imeenea sana na watu wengi wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara huwa na tatizo hili migraine. Maumivu haya yanaweza kuwa ya upande mmoja; lakini yanaweza kuwa katika paji la uso pia na kusikika katika eneo lote la paji la uso, na shingo.

Aina hii ya maumivu ya kichwa huwa ni ya “kichwa kugonga” (throbbing pain) na huambatana na dalili kama vile kichefuchefu na/au kutapika, kizunguzungu, macho kushindwa kuona vizuri, macho kuuma yanapoangalia mwanga. Aina hii ya maumivu ya kichwa huzidishwa na kutembea au kujisogeza kwa namna yoyote, na mgonjwa hujisikia nafuu akipumzika/kulala;kwa kawaida, maumivu haya huwa makali kwa muda wa masaa 1-2, na yanaweza kuchukua kati ya masaa 4 hadi 72.Vitu ambavyo huweza

kusababisha mtu mwenye tatizo la migraine kuanza kuumwa kichwa (triggers) ni kama vile vinywaji vyenye kemikali ya caffeine au pombe (alcohol)/sigara, mawazo, uchovu/usingizi,hasira, kwa kinadada kama akiwa anakaribia siku zake, au kwenye siku zake,mwanga mkali/sauti.
Aina hii ya maumivu ya kichwa pia huwasumbua zaidi wanawake ambao wako katika umri wa kuweza kushika mimba ambao ndio wameanza kupata hedhi zao kipindi cha karibuni. Pia, migraine huweza kurithiwa kutoka kwa wazazi kwa sababu mara nyingine husababishwa na vitu ambavyo viko kwenye vinasaba (genetics) za uzao husika.

Pia, aina hii ya maumivu ya kichwa mara nyingi hutanguliwa na ‘dalili za kabla’ (aura), ambazo hutokea kwa kati ya dakika 5-20, na hudumu si zaidi ya dakika 60; dalili hizi za kabla zinaweza kuwa kizunguzungu, kichefuchefu,mwili kukosa nguvu, n.k.

B:MAUMIVU YA KICHWA YA ‘MGANDAMIZO'(TENSION HEADACHE)
Aina hii ya maumivu ya kichwa kwa kawaida huwa ni ya ‘kugandamiza/kukaza’ (pressing/tightening), na huwa yanatokea kwenye pande zote za paji la uso kuelekea utosin (frontal-occipital); na hayazidi pale mgonjwa napotembea/kujisogeza (tofauti na migraine). Aina hii ya maumivu ya kichwa yanaweza kudumu kwa kati ya dakika 30 hadi siku 7; Na hayaambatani na dalili za kichefu-chefu/kutapika/kizungu-zungu kama ilivyo kwa migraine!! Pia hakuna dalili za awali (aura).
Mara nyingi maumivu haya huanza pale mtu anapokuwa na msongo wa mawazo; na huambatana na kukosa usingizi (insomnia).

II.MAUMIVU YA KICHWA YA UPILI (SECONDARY HEADACHE)
Aina hii ya maumivu ya kichwa husababishwa na tatizo lingine amblo lipo ndani ya mwili na mgonjwa hupata maumivu haya kama matokeo ya tatizo hilo lingine mwilini. Maumivu ya kichwa ya aina hii kwa kawaida huambatana na dalili zingine ambazo nazo zimekuwa zimesababishwa na tatizo la msingi. Dalili hizo zingine ni;
-Homa,
-Kupungua uzito
-Dalili za mfumo wa fahamu (kuchanganyikiwa, kuzimia,kupungua kwa hali ya ufahamu, macho kushindwa kuona,mwili au sehemu ya mwili kupooza)
-Maumivu ya viungo/mifupa
-Kuishiwa damu
-Historia ya kuwahi kuumia kichwa/kupata ajali ya kichwa,
-Maumivu mapya ya kichwa kwa mtu mwenye umri wa miaka 50 na zaidi ambae hakuwahi kuwa na tatizo la maumivu ya kichwa.
Mara nyingi, visababishi vya maumivu ya aina hii ya kichwa huwa ni kama ifuatavyo,
-Maambukizi ya bakteria/virusi
-Saratani ya ubongo,
-Matatizo ya macho,
-Kiharusi.
-Presha ya kupanda/kushuka,
-Matatizo ya mishipa ya fahamu,
-Damu kuvilia kwenye ubongo.
-Upungufu wa maji mwilini (dehydration).
HITIMISHO
Ni muhimu pia kukumbuka kuwa; mara nyingi maumivu ya kichwa pia hutokana na aina ya maisha tunayoishi ambayo ni kinyume na kanuni za afya bora; Kama vile kutokunywa maji ya kutosha (angalau lita 1.5 kwa siku), kutopata usingizi wa kutosha (angalau masaa nane kwa siku), uchovu uliopitiliza, matumizi ya vinywaji vyenye caffeine/pombe/sigara. Hivyo basi, ni vyema kuishi kwa kufuata kanuni hizi za afya ili kujikinga na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara. Na kama unafuata kanuni hizi na bado maumivu ya kichwa yanakusumbua mara kwa mara, ni vyema ukawaona wataalamu wa afya kwa ajili ya ushauri, vipimo na matibabu
 
View attachment 1672060

Asante sana Mungu akubariki ..! Naweza kuangukia apo namba 2 maana nikiwa na mawazo tu kichwa lazima kiume [emoji32], pia maumivu kama haya yashawai nitokea nikiwa shule kipindi cha mitihani
 
Wanajukwaa naomba msaada wenu, nimekuwa nikiumwa na kichwa kwa muda mrefu ila sasa kimezidi naomba mnisaidie itakuwa shida nini???
Hivi kwann matatizo ya kiafya ambayo yanahitaji medical attention mnakuja kuleta humu?!

Wewe unaumwa, halafu jambo la kwanza unakimbilia kufanya ni kuja JF, hivi unakuwa mzima kweli kiakili?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kajaribu kupima macho pia.Unaweza shangaa kujua ndio yanasababisha hiyo hali
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom