Maumivu ya jino | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maumivu ya jino

Discussion in 'JF Doctor' started by Davies_007, May 16, 2011.

 1. D

  Davies_007 Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu Naumwa na Jino ile mbaya. hivi dawa ya Jino nin kama sitaki kulitoa?
   
 2. njiro

  njiro Senior Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 106
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Limetoboka hadi kwenye nerve? Kama limetoboka hakuna ujanja, labda ung'oe ama wakufanyie root canal
  Kama bado je lina usaha? Kama lina usaha jaribu kunywa antibiotics (amokslini). na make sure kuwa uwe unalisafisha kuondoa mabaki ya chakula. Pia uache kula pipi na biscuits au chokolate

  Kitu cha muhimu hapo nenda kwa Dakitari wa meno, anaweza kukupa ushauri wa kutosha kabisa. By the way ukipata dactari mzuri atakung'oa jino taratibu.
  Pole sana.
   
 3. D

  Davies_007 Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee Jino Limetoboka tu, ila naogopa kulitoa coz niliambiwa kutoa jino la juu ni Hatari sana
   
 4. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Maumivu ya Jino ni noma is better you take it off
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  May 16, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pole sana pamoja na ushauri wa mkuu hapo, kama halijawa katika hali mbaya sana jaribu pia kutengeneza dawa hii ambayo mimi niliisikia kwa Dk. Ndodi nikaitengeneza nikaitumia kwa kweli kwangu ilinisaidia mpaka sasa nina ahueni maana meno yalianza kutoboka mpaka nikaogopa nisigebaki kibogoyo.

  Niliichukua ndulele (ndula) mbili zilizokomaa vizuri na kuwa za njano zenye kubwa nikakata katikati pamoja na malimao mawili yaliyokomaa vizuri lakini yana rangi ya kijani nayo nikakata katikati kisha nikachemsha baada ya kuiva (kama dk 15) epua nikachanganyachanganya (squeeze) kwa kutumia mikono safi kisha nikachuja, halafu nikadondoshea matone matano ya mafuta ya taa nikakoroga vizuri na kijicho. Kila nimalizapo kula usiku nahakisha nimeshapiga mswaki na kuondoa mabaki yote ya vyakula kwenye meno na kuwa sitakula kitu kingine 'then' nachukua vijiko vitatu vya chakula vya hiyo dawa nasukutua kwa muda wa dk 15 - 20 kisha natema naenda kulala. nilifanya hivyo kwa muda wa siku tatu (ndio dozi) baada ya hapo nikapona hivyo bado nadunda nilisevu kwenda kung'oa. labda side effect niliyoiona ni meno kufa ganzi wakati uko kwenye dozi ila inakwisha mara baada ya kumaliza dozi. So ukipenda unaweza kujaribu au vipi muone daktari wa meno.

  Ila suala la usafi wa meno ni muhimu ni vyema kuhakisha unapiga mswaki vuzuri asubuhi na jioni kabla ya kulala najua sio rahisi kupiga mswaki kila umalizapo kula kama taratibu za afya zinavyotaka ila asubuhi na jioni ni muhimu kwa kweli.
   
 6. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60

  mmh mkuu hiyo dawa yako kiboko nina tatizo la meno kama yako ila hiyo dawa yako.. please hebu kuwa serious
   
 7. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Wahi kwa Dentist haraka iwezekanavyo..akiliona anaweza kukushauri ung'oe au la...isije ikawa ni root canal, maumivu yake si mchezo na inahitaji matibabu haraka..
   
 8. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #8
  May 20, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  INAONEKANA UNAOGOPA SANA DAWA AU UNAAMINI dAWA ZA HOSPITALI TU NDIO ZINAWEZA KUMALIZA MATATIZO YAKO.

  HIYO DAWA NI NZURI UKITUMIA HAUMEZI UNATEMA; UKIMEZA NI SUMU. MIMI NIMETUMIA NA IMENISAIDIA SIWEZI MSHAURI MTU KITU AMBACHO SIJAKITUMIA.
   
 9. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60

  sio kuwa naogopa dawa... halafu katika vitu ambavyo huwa na imani navyo ni njia mbadalay a kutibu ungonjwa... mi ni mpinzani namna moja sana wa dawa za hospital sema elimu za njia mbadala ya kutibu maradhi mbalimbali ndio zinatupita pembeni anyway nitajaribu na nikipona nitakiuja kutoa ushuhuda hapa.. thanx for the tip
   
 10. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,333
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  dah, hiyo makini sana ila mixture yake babkubwa. Are you serious rubi?
   
 11. Graca

  Graca JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hii dawa ya ukweli, mama yangu alishatumia akapona.
   
 12. blackdog

  blackdog Member

  #12
  May 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mimi nilisubuliwa na jino nilishindwa kufanya kazi kwa siku tatu nilipokwenda hospitali nilishauriwa kuliondoa lakini waliniambia ni hatari sana, rafiki yangu alinichimbia mizizi ya ndulele akanichemshia nikasukutua kwa siku mara tatu sikuamini kabisa sijaliondoa jino langu. Naamini ndulele ni dawa ya meno tofauti ni utumiaji tu.
  Jaribu kama utapenda lakini maji usimeze.
   
 13. N

  NZURI PESA JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 4,034
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Si kweli.mi nisha ng'oa meno ma 2 ya juu na 1 la chini miaka 9 iliyopita yana maumivu sawa.Na daktar aliyening'oa ni mtaalam sikuhisi maumivu tena baada tu ya kung'oa.Upo mkoa gan au wilaya gan nikupe maelekezo
   
 14. wende

  wende JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 715
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo iko sawa kabisa,,,ila wasiwasi wangu ni huo muda wa dk15-20 wa kusukutua naona kama ni muda mwingi mno!! Isn't 3minutes?? Side effect nyingine nikuwa,jiandae kutokwa na mate mengi sana mpaka kero,,,,,hii si kwa watu wote. Nina mifano hai,kuna watu wamepona kabisaaa.
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wote hapa mnaongelea kung'oa au dawa mbadala hamna alieongelea kuziba,mimi nimeziba kama manne na moja lina miaka 10 ni mbinu nzuri sana.
   
 16. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,185
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  Root cal treatment ni aina ya matibabu ya meno, ambapo jino linauliwa kwa kuondoa kiini (pulpu) na sehem ya katikati ya mzizi wa jino (canal) husafishwa, ili kuondoa infection ambayo inaweza kuwa imefika huko. Baada ya kujiridhisha kuwa maambukizi yameisha (maumivu hua yamekoma na antibiotic zaweza kutumuka) jino huzibwa kuanzia mwisho wa mzizi (apex) mpaka kujengwa sura halisi ya jino kama lilivo kuwa kabla ya kutoboka. Jino huendelea kuwepo na kutumika kama kawaida na pasipo maumivu lakini jino hilo siyo hai.Kwakweli there so many things to know in dentistry whether ua a dental practitioner or not ni muhim kujua kwan ni sehem ya afya zetu. Please fana dental check up atleast twice a year,usiende dental clinic kwa kusukumwa na maumivu kuna mengi hufanywa huko twendeni na tuwatumie ma dentist si wakati wa maumivu tu bali hata kwenye mpangilio mbaya wa meno kinywani kwani nayo huongeza chance za jino kutoboka. kukaa naugonjwa kinywani inaweza kukuingiza ktk complikeshen au kukugharim maisha.
   
 17. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #17
  May 23, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,185
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  Hiyo dawa yako mkuu inachokifanya ni kuua mishipa ya faham kwenye jino hivo maumivu huisha kwan nerves zinazofanya uhis maumivu umeziua na mawasiliano hamna,(mf. sawa na paralysis ya guu au mkono) kama jino hilo limetoboka litaendelea kupukutika mpaka liishe pasipo luleta maumivu. ANGALIZO: Kuendelea kukaa na jino lililo toboka si salama kwa afya yako ingawa halina maumivu kwan kuna mawasiliano kati ya nje na ndan kupitia hilo tundu kwny jino kwahiyo waweza kujikuta siku moja unaamka na kujikuta umevimba ingawa hukusikiamaumivu hapo awali. Kwa ufupi simshauri mtu kuitumia hiyo dawa ya Ndodi inafanya root canal isiyo rasmi hata kwa meno ambayo yangezibwa kwa njia za kawaida. alafu si kila jino linalouma litafanyiwa matibabu hayo, ndugu kuna visababishi vingi vya maumivu kinywani vivyo hivyo na matibau yake!
   
 18. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Kudondoshea mafuta ya taa si sumu hiyo Mkuu!
   
 19. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Huo muda ni sahihi kabisa maana ndio dawa inapenya kwenye jino na kuua wale wadudu sasa ukitaka mudo wako mwenyewe hutapona daina sikiliza ushauri wa daktari.
   
 20. Fredwash

  Fredwash JF-Expert Member

  #20
  May 23, 2011
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 594
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 60


  mmh veri veri resonable chalenge... but anyway its worth trying... finger crossed!
   
Loading...