Limbert
Member
- Nov 26, 2013
- 64
- 12
- Thread starter
- #21
Pole sana kaka Limbert :
Kitendo cha kukubaliana na wenzako kuwa ni kazi ya Mungu ni hatua ya kwanza kwenda kwenye uponyaji. Ni kawaida kabisa ukifiwa na mwenza upitie kipindi cha "grief" / 'Mourning'na ndicho unapitia sasa. Kipindi hiki huchukua muda tofauti kulingana na mazingira, ukaribu wako na mwenza aliyetangulia nk ila napenda kukushauri tu
Nakutakia neema za Mungu tele katika kupita katika kipindi kigumu.
- Mshukuru Mungu aliyekupa muda ya kuwa na mpenzi wako (cherish the moments you had spent and thank God)
- Kama una watoto - kuwa nao karibu ,na wasione moyo wako umekata tamaa maana wewe ndio muhumili wao daima
- Mwambie Mola wako kweli yote kuwa unaumia na ni kwa neema tu ndio utaweza- kama kuna vikundi vya ibada/ maombi au counseling groups unaweza kuhudhuria kupata ushauri zaidi
- Jumuika na jamii kwa kiasi : kama ulikuwa mpenzi wa mpira basi angalia au hudhuria mechi, tamasha la muziki nk
- Kikubwa - Jiamini kuwa Mungu atakupitisha yote - maumivu kweli yapo kwakuwa tu binadamu ila kila sononi ijapo jipe moyo na jiambie nafsi yako kuwa nitaweza kuendelea mbele maana ni Lazima kipindi cha grief kipite ili uendelee mbele na maisha yako.
mkuu ufaham wako ukojuu. maneno yako yageuke kuwa MAOMBI iwe NEEMA Kwangju.Hekima ya MUNGU iwenawewe daima.