maumivu makali yanatesa moyo wangu

maumivu makali yanatesa moyo wangu

Limbert

Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
64
Reaction score
12
katika jamii hii nimeingia tangu sasa nina maumimivu makali katka moyo wangu.kwa miezi mitano sasa toka nimpoteza mpendwa wa moyo wangu (Alifariki). sasa ninaumri 40 lakini nakili kuwa nilikuwa nikiungana na Wengi kusema nikazi ya MUNGU na baada ya muda nazoea maisha yanaendelea. Kituambacho imekuwa kinyume toka nimpoteze mpendwa wangu mpenzi wa moyo wangu nakili kuwa alikuwa mke mzuri wa tabia sura naumbo .kilicho kuwa kikivutia zaidi hakujiunga namkologo wowote; nilikuwa nikivutiwa na ngozi yake. ninapotoka kazini toka ameniacha . huingiwa nahuzuni kila mara hushindwa kutoka hata nyumbaini nashindwa kufanya kazi za ziada ijapo MAISHA LAZIMA YAENDELEE . Nitaepukanaje na hali hii.
 
pole sana na mimi ninatatizo kama lako naomba tuwasiliane ili tufalijiane niko serious nitumie namba yako au email yako pole.
 
Karibu sana JF...

Pole kwa tabu na maswaibu yote uliyoyapata, kama una watoto basi hakikisha unakuwa nao karibu.

Usiache pia kumwomba Mungu akupe faraja...
 
pole sana na upweke kaka!!

Sina ushauri wa moja kwa moja ila mtegemee sana MUNGU ili usiingie vishawishini na kama ulivyosema umri wako bado unaruhusu kuwa na mwenza mwingine ingawa anaweza asiwe sawa na yule wa mwanzo ila naamini itasaidia kidogo kuliko upweke ulio nao sasa!!

''kila la kheri mkuu''
 
Mkuu pole sana. Kama ulivosema maisha lazima yaende, na yaendelee kama zamani. Kuna mdau kakushauri kama unawatoto kuwa karibu nao, pia mi naongeza kuwa usipende kukaa peke yako na kujielekeza mawazo yako kwake, hatarudi huyo. Sali sana, jumuika na jamaa zako, fanya mazoezi sana, na usifanye kosa la kutafuta mbadala sasa, itakuumiza wewe sana.

Pole mkuu, maisha ndivyo yalivyo, maisha lazima yaendelee.
 
Kwanza nakukaribisha sana hapa kwetu nyumbani

Nahisi kweli una maumivu, mwenzi wako kukuacha wakati bado unampenda na kumhitaji...Mungu akusaidie sana, endelea kumwomba pia

Usitumie changamoto hii kujiingiza kwenye mambo mabaya uanyohisi yatakuondolea maumivu ya moyo wako..

katika jamii hii nimeingia tangu sasa nina maumimivu makali katka moyo wangu.kwa miezi mitano sasa toka nimpoteza mpendwa wa moyo wangu (Alifariki). sasa ninaumri 40 lakini nakili kuwa nilikuwa nikiungana na Wengi kusema nikazi ya MUNGU na baada ya muda nazoea maisha yanaendelea. Kituambacho imekuwa kinyume toka nimpoteze mpendwa wangu mpenzi wa moyo wangu nakili kuwa alikuwa mke mzuri wa tabia sura naumbo .kilicho kuwa kikivutia zaidi hakujiunga namkologo wowote; nilikuwa nikivutiwa na ngozi yake. ninapotoka kazini toka ameniacha . huingiwa nahuzuni kila mara hushindwa kutoka hata nyumbaini nashindwa kufanya kazi za ziada ijapo MAISHA LAZIMA YAENDELEE . Nitaepukanaje na hali hii.
 
Pole sana na karibu JF uta-enjoy sana sana ila usiende kwenye kukwaa la siasa litakuongezea stress, baki MMU na Chitchat. Utafarijika na JF itakua sehemu ya maisha yako. MUNGU akusaidie sana katika kipindi hiki
 
oooh! pole sana kaka, ila ninaamini Mwenyezi Mungu aliyemchukua mkeo kipenzi, ndio huyohuyo atakayekupa faraja na kukutia nguvu ktk kipindi chote cha maisha yako..mtumaini yeye. Pia km mlijaaliwa watoto basi kuwa nao karibu ili faraja ipztikane pia. Pole sana umenitia uchungu kiukweli!
 
Pole sana kaka Limbert :

Kitendo cha kukubaliana na wenzako kuwa ni kazi ya Mungu ni hatua ya kwanza kwenda kwenye uponyaji. Ni kawaida kabisa ukifiwa na mwenza upitie kipindi cha "grief" / 'Mourning'na ndicho unapitia sasa. Kipindi hiki huchukua muda tofauti kulingana na mazingira, ukaribu wako na mwenza aliyetangulia nk ila napenda kukushauri tu

  • Mshukuru Mungu aliyekupa muda ya kuwa na mpenzi wako (cherish the moments you had spent and thank God)
  • Kama una watoto - kuwa nao karibu ,na wasione moyo wako umekata tamaa maana wewe ndio muhumili wao daima
  • Mwambie Mola wako kweli yote kuwa unaumia na ni kwa neema tu ndio utaweza- kama kuna vikundi vya ibada/ maombi au counseling groups unaweza kuhudhuria kupata ushauri zaidi
  • Jumuika na jamii kwa kiasi : kama ulikuwa mpenzi wa mpira basi angalia au hudhuria mechi, tamasha la muziki nk
  • Kikubwa - Jiamini kuwa Mungu atakupitisha yote - maumivu kweli yapo kwakuwa tu binadamu ila kila sononi ijapo jipe moyo na jiambie nafsi yako kuwa nitaweza kuendelea mbele maana ni Lazima kipindi cha grief kipite ili uendelee mbele na maisha yako.
Nakutakia neema za Mungu tele katika kupita katika kipindi kigumu.
 
pole mkuu katika kipindi kigumu ulicho nacho. Hakuna njia mbadala zaidi ya kumtegemea Mungu na sali sana ili upate faraja ya kweli,Mungu wetu ni mwema soon hy hali itapotea maana wewe ukiwa hivyo na watoto watakuwa kwenye hali gani?
 
pole sana na mimi ninatatizo kama lako naomba tuwasiliane ili tufalijiane niko serious nitumie namba yako au email yako pole.

Mtoa mada pole sana lakini ushapata wa kukufariji huyu amejitokeza naimani utasuuzika nafsi
 
Pole sana mkuu. At that age naimagine.una maumivu kiasi gani...muhimu zingatia walichoshauri wenzangu ila niseme tu pia jichanganye na watu usikae peke yako muda mrefu...pia unaweza kuangaza angaza kama utapata wa kufarijiana naye mwenye nia ya dhati umuoe.
 
katika jamii hii nimeingia tangu sasa nina maumimivu makali katka moyo wangu.kwa miezi mitano sasa toka nimpoteza mpendwa wa moyo wangu (Alifariki). sasa ninaumri 40 lakini nakili kuwa nilikuwa nikiungana na Wengi kusema nikazi ya MUNGU na baada ya muda nazoea maisha yanaendelea. Kituambacho imekuwa kinyume toka nimpoteze mpendwa wangu mpenzi wa moyo wangu nakili kuwa alikuwa mke mzuri wa tabia sura naumbo .kilicho kuwa kikivutia zaidi hakujiunga namkologo wowote; nilikuwa nikivutiwa na ngozi yake. ninapotoka kazini toka ameniacha . huingiwa nahuzuni kila mara hushindwa kutoka hata nyumbaini nashindwa kufanya kazi za ziada ijapo MAISHA LAZIMA YAENDELEE . Nitaepukanaje na hali hii.

Tatizo lako kubwa hujiaini na kwakuwa hujiamini huwaamini binadamu wengine pia

Marehemu mpendwa wako huenda ni kweli alikuwa na sifa hizo
Hilo halimaanishi kuwa hakuna mwingine
Lakini pia hilo halimaanishi ndio ukae na huzuni kiasi hicho
Huko aliko anasikitika sana kwa kuona namna ulivyo dhaifu

Na anasikitika kuwahi kuwa na mahusiano na mtu dhaifu kama wewe
Uanaume sio kuwa na jinsia ya kiume tu
Ni pamoja na kuyaweza majaribu kama haya

Tena una umri wa miaka 40!!!!!!!!!!!!!!
Unasikitisha sana

Unadhani kuwa ulibahatisha kumpata
Hujiamini kabisa

Huamini kama kuna wanawake wazuri kama huyo
Unadhani ni vigumu sana kuwapata wa aina hiyo

hujui kwamba kuna wanawake bora sana zaidi ya huyo

Unajidanganya kuwa hayo ni mapenzi ndio yanakufanya hivyo

Ukweli ni kuwa hiyo ni hofu tu ya kupata mwingine kama huyo
Unaendelea kujidanganya kuwa kuna kama huyo

Unashindwa kujua tu kuwa hakuna kama huyo lakini kuna aliebora kuliko huyo
Hebu kua kiakili!

By the way
Pole na kuondokewa na mpendwa wako
Jambo zuri la kufanya na kumuenzi ni kukua kiakili na kuondokana na hayo mawazo!
 
Karibu sana JF...

Pole kwa tabu na maswaibu yote uliyoyapata, kama una watoto basi hakikisha unakuwa nao karibu.

Usiache pia kumwomba Mungu akupe faraja...
Inasikitisha sana mtu wa umri kama huu kuondokewa na mpendwa wake miezi mitano iliyopita halafu analialia kiasi hiki

N kibaya zaidi hata wakati mwingine ndani hatoki!!

Inakuwaje hii??????????
 
Inasikitisha sana mtu wa umri kama huu kuondokewa na mpendwa wake miezi mitano iliyopita halafu analialia kiasi hiki

N kibaya zaidi hata wakati mwingine ndani hatoki!!

Inakuwaje hii??????????

Pengine walipendana sana na walikuwa wanaambatana kwa kila jambo...kuna watu walio ndoani hupatana kama mapacha au chanda na pete
 
Inasikitisha sana mtu wa umri kama huu kuondokewa na mpendwa wake miezi mitano iliyopita halafu analialia kiasi hiki

N kibaya zaidi hata wakati mwingine ndani hatoki!!

Inakuwaje hii??????????

ujasili huopia nilikuwa nao. hivyo nashindwa kushangaa kwaswalihili nanisingependa upatejibu. inauma sana.MUNGU AWEMWEMA kwako
 
Tatizo lako kubwa hujiaini na kwakuwa hujiamini huwaamini binadamu wengine pia

Marehemu mpendwa wako huenda ni kweli alikuwa na sifa hizo
Hilo halimaanishi kuwa hakuna mwingine
Lakini pia hilo halimaanishi ndio ukae na huzuni kiasi hicho
Huko aliko anasikitika sana kwa kuona namna ulivyo dhaifu

Na anasikitika kuwahi kuwa na mahusiano na mtu dhaifu kama wewe
Uanaume sio kuwa na jinsia ya kiume tu
Ni pamoja na kuyaweza majaribu kama haya

Tena una umri wa miaka 40!!!!!!!!!!!!!!
Unasikitisha sana

Unadhani kuwa ulibahatisha kumpata
Hujiamini kabisa

Huamini kama kuna wanawake wazuri kama huyo
Unadhani ni vigumu sana kuwapata wa aina hiyo

hujui kwamba kuna wanawake bora sana zaidi ya huyo

Unajidanganya kuwa hayo ni mapenzi ndio yanakufanya hivyo

Ukweli ni kuwa hiyo ni hofu tu ya kupata mwingine kama huyo
Unaendelea kujidanganya kuwa kuna kama huyo

Unashindwa kujua tu kuwa hakuna kama huyo lakini kuna aliebora kuliko huyo
Hebu kua kiakili!

By the way
Pole na kuondokewa na mpendwa wako
Jambo zuri la kufanya na kumuenzi ni kukua kiakili na kuondokana na hayo mawazo!

Aaa nikweli ! hata mm kabula ningeweza kusema kama unavyosema lakini. ukisikia mtu anamsema mtu kuwaalibahatisha juwa huyomtu anahitaji msaada , unahitajimusaada kilashauli huwezikushauri wapo wanaoweza fatilia utajifunza. AMANI IDUM PAMOJA NAWE Kuanziasasa nazaidi.
 
Back
Top Bottom