Maumivu juu ya maumivu

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,395
Reaction score
1,442
Ilikuwa ni asubuhi nikiwa nimetoka nje kuota jua na kupunga upepo uliokuwa ukipuliza vyema na kufanya hali ya hewa kuwa ya kuvutia zaidi. Nilitazama ndege jinsi wakikatiza kwenye anga na sauti zao wakiimba wimbo mzuri kufurahia uumbaji wa Mungu, sauti zao zilivutia jambo lililofanya nifurahie kuwa eneo hilo.

Siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumamosi hivyo sikwenda kwenye mihangaiko yangu ya kila siku, niliamua ni pumzike na kisha mida ya mchana mchana nilipanga kwenda kutembelea sehemu mbalimbali kufurahia weekend. Nilipanga kwenda kuonana na kipenzi changu Janeth kwani wiki nzima kutokana na ubize hatukuweza kuonana pia vilevile nilikuwa na uchu wa kukumbushia ule mchezo ambao nadhani wengi wenu mnaufahamu. Nilikuwa tayari nimejipanga kimaandalizi ni kitendo cha kuoga na kuvaa na kuondoka wakati ukifika ndo kilichobaki.

Nikachukua simu na kumpigia kipenzi changu Janeth na kumtaharifu kuwa ajiandae tukutane kwenye kamgahawa flani hapo baadae.(Sawa mpenzi wangu Hezzron)alijibu Janeth.

Muda uliwadia hatimaye niliwahi kwenye ule mgahawa tuliokubaliana kukutana. Nilimsubiri bila mafanikio na kila nikijaribu kupiga simu yake haikuwa ikipatikana. Sikukata tamaa nikaagiza soda huku nikipotezea nayo muda nikimsubiri.

Nilisubiri tangu saa tisa mchana hadi giza likaingia bila mafanikio huku nikijaribu kupiga simu yake mara kadha wa kadha ikiwa haipatikani. Kuna muda ilikuja kupatikana lakini haikuwa ikipokelewa hivyo niliandika sms za kumuuliza mbona unanifanyia hivyo nazo hazikujibiwa. Niliamua kurudi nyumbani mahali nilipokuwa ninapanga nikajilaza kitandani huku nikiwa na mawazo kedekede nikimuwaza kipenzi changu Janeth.

Nikachukua tena simu yangu ilikuwa majira ya saa mbili usiku na kumpigia tena, safari hii ilipokelewa na aliongea maneno machache na kisha kukata simu. "Acha usumbufu kapuku wewe, umeona mimi ni wa kupelekwa mgahawani. Ingia WhatsApp uone wanaume, ila sio wewe na misuruali yako." Hayo ndiyo maneno aliyoongea na kisha kukata simu bila ya mimi kujibu chochote, nikawasha data niingie WhatsApp nione yaliyojiri. Message mbalimbali zikaanza kuingia ikiwemo message za Janeth na videos kutoka kwa Janeth zikidisplay kwenye simu. Moja kwa moja nikabonyeza kwenye Jina la Janeth nikaanza kuplay akiwa analiwa mzigo live kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo bafuni, swiming pool na kwenye sita kwa sita kwenye hoteli ambayo sikuifahamu ila inaonekana ni hoteli ya bei mbaya, yani zile hoteli za bei chafu, mtu wa hali ya chini au kati kiuchumi hawezi kuingia humo. Huku alimalizia na ujumbe wa message iliyosomeka "Kati ya huyo na wewe nani mwanaume?"

Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio na kujikuta nikirusha simu pembeni na kujilaza bila hata kusoma message za watu wengine na bila hata ya kuzima data. Nilivuta usingizi bila ya mafanikio, sikukumbuka hata kula, niliumia sana. Nilitamani nilie nayo ikashindikana, nikabaki nikiwaza sana na kujiuliza sana nimemkosea nini lakini sikuwa na majibu. Niliwaza mpaka majira ya saa nane usiku ndipo usingizi uliponichukua.

Niliamka asubuhi siku ya Jumapili na kwa kuwa nilikuwa najisikia vibaya sana, sikuenda kusali siku hiyo. Baada ya mawazo ya muda mrefu nikaamua tena kumpigia simu bila ya mafanikio kwani haikupokelewa, ilizidi kuniumiza mno. Majira ya jioni saa moja usiku akanipigia video call WhatsApp nikapokea, lakini hakuongea na mimi akampa huyo njemba aongee na mimi. "Kijana mbona unamsumbua mke wangu?", Niliduwaa sikuwa nimemjibu, moyoni nilikuwa nina hasira imekuwaje Janeth kunisaliti kiasi hiki. Niliamua kukata simu na kuizima mpaka kesho yake, nikikesha na mawazo na maumivu mazito moyoni. Nilijiuliza mengi nikawaza na kuwazua lakini sikupata majibu.

Kesho yake ilikuwa ni siku ya Jumatatu nilianza tena kwenda kwenye mahangaiko yangu, sikuwa sawa kabisa kichwani, nilihisi dunia inanicheka, hata nikiona watu wamekaa wanaongelea mambo yao niliona kama wananisema mimi. Safari hii nilijikaza kiume na sikumtafuta tena Janeth ili asije akazidi kuniumiza kwa mara nyingine. Kazini watu waliniuliza Hezzron vipi leo, mbona umebadilika, walizoea kuniona mchangamfu wakati mwingine nilifanya vituko mbalimbali vilivyofanya wacheke. Lakini siku hiyo haikuwa hivyo nilikuwa nimetulia tu nikionekana nina mawazo mengi. "Hakuna tatizo, niliwajibu"

Majira ya saa saba mchana tukielekea kula nilisikia sauti ya kike ikiniita kwa nyuma na kunitaka nimsubiri. Nilisimama na kugeuka nyuma nimwone aliyeniita. Alikuwa ni Jesca rafiki yangu ambaye tulifahamiana pale pale kazini. "Vipi, nimekuona leo upo tofauti, au una kesi nini polisi?" lilikuwa swali lake la kwanza kuniuliza aliponifikia. "Hapana niko kawaida mbona." nilimjibu kwa kujiamini. "Ok, nimekufuata tukale wote" aliongezea. "Sawa"nilimjibu kisha tukaongozana kwenye mgahawa mmoja ulio karibu na maeneo tulipokuwa tunafanya kibarua chetu pale kazini.

Tukiwa tunakula pale mgahawani Jesca alijaribu kuniuliza sababu ya mimi kuwa mpole kiasi kile lakini hakufanikiwa kuupata ukweli wowote kutoka kwangu, hivyo alikata tamaa ya kuendelea kuniuliza akabaki akiniangalia tu kwa macho ya huruma. Tulimaliza kula na kurejea tena kibaruani aliniomba baadaye tukitoka tuongozane wote, maana sehemu niliyokuwa nahishi, yeye aliishi mtaa wa pili yake. Nilimkatalia na kumwambia ntaenda mwenyewe hakuna shida, lakini ni kama aligundua sipo sawa hivyo alining'ang'aniza hatimaye nikamkubalia kishingo upande baada ya yeye kung'ang'ania sana.

Mda ya kutoka kazini ulifika na Jesca akanikumbusha kuwa tunapaswa kuondoka wote, nikamkubalia kisha tukaongozana kwa mguu kwani kutoka kazini hadi ninapoishi hakuna umbali sana, vile vile kwa upande wake.

Tukiwa njiani aliniuliza sana sababu ya mimi kutokuwa na amani siku hiyo, mwisho wa siku ikabidi nimhadithie yaliyonisibu. Akanipa pole na kunitaka nisife moyo kwani ni mambo yakupita tu.

Tuliongozana mpaka nikawa nimefika maeneo ya nilipokuwa naishi kwani yeye alikuwa anaendelea mbele kidogo, nikamuaga lakini alitaka aende na mimi kwangu, niligoma goma kiaina lakini nikajiambia nisichezee bahati hivyo nikakubali. Kweli siku hiyo tulifika akapika tukala tukaanza uchokozi wa hapa na pale, (ikumbukwe kuwa hatukuwa na mahusiano yeyote yale zaidi ya urafiki wa kawaida). Basi tuliendelea hatimaye tukaangushana kitandani na kilichofanyika wengi mnakijua sitakielezea hapa. Na kwanzia siku hiyo huo ulikuwa mchezo wetu hadi tukakolea kabisa.

Siku zilizidi kusonga huku tukiendelea na Jesca tukiwa tumezana penzini na hatimaye kuendelea kumsahau Janeth siku kwa siku kwani hata namba zake nilikuwa nimefuta.

Baada ya miezi sita nilipata ujumbe wa sms kwenye simu yangu kutoka kwa mtu nisiyemfahamu akiomba tuonane. Nilimwambia kuna shida gani? Na wewe ni nani? Akaniambia naitwa Angel nilikuwa naomba tuonane kuna ndugu yangu anataka aje aombe kazi hapo unapofanyia ndo nilipewa namba zako Unipe maelezo, nakuomba sana, gharama zote nitalipa mimi za wewe kuja n kurudi na chakula. Basi nikamkubalia akanielekeza pa kukutania. Nilifika na kumtaarifu nimefika haikuchukuwa dakika tano akawa amewasili na kunigusa begani kwa nyuma. Nikageuka na kushangaa kumwona Janeth. Nikamuuliza umejuaje niko hapa. Akaniambia mimi ndo nimekudanganya naitwa Angel nimeona nikikuambia ukweli usingekuja. Nimekuja kukuomba msamaha yule jamaa aliazima gari alichukua mkopo benki akanirubuni nao mwisho wa siku akanikimbia, nimekuja kukamatwa mimi na polisi kumbe jamaa alikuwa pia mwizi, polisi wamenishikilia kwa miezi mitatu mizima wakijua nafahamu mwizi alipo, baadae walipogundua sijui lolote wakaamua kuniachia juzi juzi tu. Naomba nisamehe sana turudiane. Nikamwambia sitoweza kurudiana na wewe ila nakusamehe.

FUNZO:
Jali utu usijali maslahi.

 
Heading sasa, mods msaidieni kijanq wenu kuweka tittle inayoendana na story yake.
 
Story yako nzuri utafikiri ya kweli vile heading ndo haiendani na story
 
Maumivu juu ya maumivu. Mbona sioni maumivu ya pili kwako HEZRON wala kwa JANETH? Kichwa cha habari hakiendani na maelezo yake, badilisha. Umeumizwa J1, J3 ukatibiwa. Au inataka kusema JESCA alikuachia STDs?

Bazazi
 
Yani demu akutumie video analiwa mzigo kweli??? Anyway achana nae.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…