Maumivu chini ya ubavu wa kushoto, Msaada tafadhali

nabali

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
405
526
Kwa muda wa miaka miwili sasa nimekuwa nasumbuliwa na maumivu chini kidogo ya ubavu wa kushoto, nimejaribu kwenda hospitali mara kadhaa, mara ya kwanza nikaambiwa UTI pamoja na kutumia dawa maumivu hayakuisha! Nimesharudia kupima mara 3 sina UTI tena, ila maumivu yanazidi! Kitu pekee kinacho nisaidia kupunguza maumivu ni kunywa maji mengi! Hali hii mpaka lini? Naombeni ushauri wa kitabibu wakubwa zangu!
 
Pole sana kwa maradhi yako nenda kapige XRAY kisha uje utuambie una maradhi gani? nenda Hospitali kubwa ya hapo unapoishi. Uguwa pole Ukitaka maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na mimi kwa kubonyeza hapa.Mawasiliano
 
Maumivu yapo tumboni upande wa kushoto au kwenye mbavu zenyewe.Kama ni tumboni kajaribu kufanya ULTRASOUND SCAN utafahamu ni nini.
 
POLE SANA LABDA NI VIDONDA VYA TUMBO!VINA TABIA YA KUHAMISHA MAUMIVU,JE UNAPATA CHOO VEMA,KAMA UNAPATA KAMA CHA MBUZI BASI JUA NI VIDONDA VYA TUMBO,VINAUMA UNAPO KUWA KATIKA HALI GANI ?UKIWA NA HASIRA AU UKIKAA NA NJAA MUDA MREFU AU UKILA VYAKULA VYENYE GAS?CHUNGUZA!ILA KUPATA VIPIMO NI MUHIMU PIA,NAJITAHIDI KUACHA VISABABISHI VYA KUKULETE HIYO HALI KAMA ITAKUWA VIDONDA VYA TUMBO AU GAS,KULA APPLE UNAPOHISI HIYO HALI AU TIKITI AU TANGO,IN SHA ALLAH UTAPONA,POLE SANA MAJI MUHIMU USIACHE LABDA NDIO IMESAIDIA KUONDOA ACID KWENYE TUMBO,JE USINGE YANYWA INGEKUAJE?POLE SANA
 
Back
Top Bottom