Usiandike kishabiki hali ya Ngorongoro inasikitisha,inakatisha tamaa & ina huzunisha.
Ni kweli Waasai wapo ngorongoro miaka mingi wakishi na wanyama pori na mifugo yao.Wakati huo Mamlaka inaanzishwa idadi ya watu ilikuwa 8,271 na idadi ya mifugo ilikuwa 30,000.Nyumba za wamaasai zilikuwa aina ya combi
View attachment 2109828
Leo idadi ya Maasai ni 120,000 huku idadi ya mifugo yao ikifikia zaidi ya 1,000,000 na makaazi yao yakiondoka katika uasilia na kwenda kwenye usasa.Leo hii mabati msouth yamejaa Ngorongoro.Mmaasai anajenga nyumba za kisasa hadi maghorofa yamejengwa ndani ya hifadhi mgeni akitembelea Ngorongoro anakutana na Kondoo,Mbuzi na Ng'ombe kwa wingi kuliko Simba au Nyati.
Lazima Tanzania ichukue hatua kali na madhubuti kuokoa Ngorongoro.Kumezuka NGOs nyingi tena nyingine zikiasisiwa Kenya zipo pale kwaali ya kutetea ujinga na kuona Ngorongoro inakufa.Hii vita asili yake kubwa ni Kenya ambayo inaumizwa sana na uwepo wa Ngorongoro,Serengeti na Kilimanjaro.Kenya kupitia idara yake ya ujasusi inafahamu wazi ushindani wa utalii ni vivutio na wakiangalia hizo Mbuga tatu wanaona bora waiumize walau moja ambayo ni Ngorongoro.
Hizi NGOs nyingi zinawadanganya wamaasai Ngorongoro ni mali yao,serekali haina chao sasa huu ujinga ungemalizwa na vingozi wenye maamuzi mazito ikiwemo kuirejesha Ngorongoro TANAPA na kuifanya HIFADHI kama zilivyo Manyara,Serengeti,Kilimajaro au Mikumi.Wamaasai wahamishwe wote Tanzania bado ina mapori mengi.