Mauaji yanayoendelea nchini Burundi

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,041
39,993
Habari zenu wanachama wazoefu wa jukwaa la siasa,

Japo mie si mwenyeji humu ila kuna mambo huwa yanagusa na kuleta hisia kwenye maisha ya uhalisia.

Hivi hawa jirani zetu Burundi inakuweje na hii hali wanayo endanayo ya kuuana kwa kuviziana. .... hasa viongozi wa vya ma vya siasa pamoja na familia zao.
Ndo kusema vita baridi ndo imeanza? Maana hapa washaanza kulipana visasi kwa kuuana. Nimeona news VOA kuwa Hon. Ben Mkapa ni mmoja wa speakers wa peace makers ........ Je iongezwe nguvu zaidi..... peace makers speakers waongezwe?

inasikitisha kwakweli wapendwa. Kule kuna wananchi wa kawaida ambao hawako kwenye siasa ila wanaathirika na hali iliyoko huko. Dawa ni nini? Nini kifanyike waache kuuana?

Maana usipozibwa ufa utajengwa ukuta...... na mzarau mwiba guu huota tende. ....

Kasie.
 
Hawa jamaa vita imo damuni mwao, toka wanapata uhuru mpaka sasa ni mwendo wa mtutu tu.

Mizizi ya vita isipofukunyukuliwa kamwe vita haiwezi kuisha humo Burundi, nakumbuka Nyerere alihangaika nao sana hawa jamaa tangu miaka ya 70 mpaka anakufa.

Mandela ackachukua kijiti, na sasa Mkapa lakini tatizo liko pale.

Washukuru sana Tanzania ambayo huwabeba kama ndugu zao bila kuangalia inanufaika na nini kutoka kwao, siku na sisi tukianza kuangalia maslahi yetu tukaweka undugu pembeni watachinjana kama kuku hawa watu.
 
Burundi ni issue kubwa kwa sasa kasie

Zaidi ya watu 400 washauwawa,

Ukimya wa hao peacemakers nao ni utata mwingine

Ngoja tuendelee kusubiri, pengine wapo chimbo wanapiga mikakati

Pamoja ya kwamba, inatia uvivu sana kusuluhisha watu wanaolazimisha migogoro isiyo na msingi
 
My love,

Kumbe hata kwenye siasa uko vizuri enh???

Hao majamaa na jirani zao wana hobby ya kuchinjana..... tuwaombee tu kwa Mungu.
 
Ungeweka link ya VOA pia..

Burundi matatizo yao yanaanzia mbali
Nkurunzinza kaja kuongezea tu
 
Nikiangalia ni nchi ndogo tuu kati ya nchi za Afrika mashariki na kati, kwanini umoja wa afrika usiingilie kati na kuitawala hiyo nchi kama koloni walau kwa miaka 5. Wanasiasa wa nchi hiyo wadhibitiwe au wahamishwe ukimbizini nchi nyingine na familia zao.

Maana jamani raia wa nchi hiyo haki yao ya msingi ya kuishi kwa amani nchini mwao iko wapi?

Wako wapi wale watu wa haki za binadamu? Mbona hawa Wanasiasa wanakuwa wabinafsi? Chanzo ni madaraka. ..? Na wanyimwe wote.
 
My love,

Kumbe hata kwenye siasa uko vizuri enh???

Hao majamaa na jirani zao wana hobby ya kuchinjana..... tuwaombee tu kwa Mungu.

Sweetheart kuna mambo yanagusa hadi yanatia hasira. Ile hali ya ubinadamu na kujali binadamu mwenzako inapokujia huwezi kufurahia kuona binadamu wanauana tuu kisa madaraka.

Natamani itokee mamlaka iwadhibiti hao wanasiasa wa Burundi watawaliwe na umoja wa afrika hata kwa miaka 5 kisha wakikaa sawa ndo wajitawale upya.
Kinachoendelea kule si kizuri.... halafu kuna watanzania wanaishi kule. Fikiria mmoja wa walipa kisasi kakosea risasi ikamuangukia mtanzania au hata mrundi. ..... yaani hadi hasira.

Mi naona kitu lazima kifanyike wasitazamwe tuu.
 
Habari zenu wanachama wazoefu wa jukwaa la siasa,

Japo mie si mwenyeji humu ila kuna mambo huwa yanagusa na kuleta hisia kwenye maisha ya uhalisia.

Hivi hawa jirani zetu Burundi inakuweje na hii hali wanayo endanayo ya kuuana kwa kuviziana. .... hasa viongozi wa vya ma vya siasa pamoja na familia zao.
Ndo kusema vita baridi ndo imeanza? Maana hapa washaanza kulipana visasi kwa kuuana. Nimeona news VOA kuwa Hon. Ben Mkapa ni mmoja wa speakers wa peace makers ........ Je iongezwe nguvu zaidi..... peace makers speakers waongezwe?

inasikitisha kwakweli wapendwa. Kule kuna wananchi wa kawaida ambao hawako kwenye siasa ila wanaathirika na hali iliyoko huko. Dawa ni nini? Nini kifanyike waache kuuana?

Maana usipozibwa ufa utajengwa ukuta...... na mzarau mwiba guu huota tende. ....

Kasie.
Njia sahihi ni Nkurunzinza kuachia ngazi na wafanye uchaguzi upya au waunde serikali ya mpito inayoshirikisha vyama vyote.
 
Sweetheart kuna mambo yanagusa hadi yanatia hasira. Ile hali ya ubinadamu na kujali binadamu mwenzako inapokujia huwezi kufurahia kuona binadamu wanauana tuu kisa madaraka.

Natamani itokee mamlaka iwadhibiti hao wanasiasa wa Burundi watawaliwe na umoja wa afrika hata kwa miaka 5 kisha wakikaa sawa ndo wajitawale upya.
Kinachoendelea kule si kizuri.... halafu kuna watanzania wanaishi kule. Fikiria mmoja wa walipa kisasi kakosea risasi ikamuangukia mtanzania au hata mrundi. ..... yaani hadi hasira.

Mi naona kitu lazima kifanyike wasitazamwe tuu.
Hapo ndipo hujawaelewa viongozi wa Afrika.

Wana tabia moja ya kijinga. Kulindana!!
 
Ungeweka link ya VOA pia..

Burundi matatizo yao yanaanzia mbali
Nkurunzinza kaja kuongezea tu

Nimeangalia VOA kwenye TV na sio Internet, sina link ya kuweka hapa.

Ila kusema matatizo yao yameanzia mbali bado haitoshi kuwaachia wauane kama barangulu. Kunatakiwa kufanyike kitu hawa peace makers kama wameshindwa basi umoja wa afrika uingilie kati.

Hivi hasa kwanini binadamu tuuane?
Kwanini?
 
Ukiwa realistic kama mimi basi ni bora wauane sana ili attention ya kimataifa ipatikane
Vinginevyo wakiviziana kama hivi kwa kuviziana.....hawatapata attention ya kuwasaidia..

Mataifa makubwa kama Marekani wakiamua..ni jambo la siku moja tu....
 
Hapo ndipo hujawaelewa viongozi wa Afrika.

Wana tabia moja ya kijinga. Kulindana!!

Yaani nikifika hapo ndo huwa nachoka kabisa na mambo ya siasa, yaani nashindwa kuelewa...... ni mchezo gani huu unaohusisha damu? Tena ya binadamu.....

Kwa mtindo huu mpenzi, mgombea wa uraisi wa marekani alivosema waafrika hawawezi kujitawala ni watawaliwe milele alikosea? Kwa nini viongozi wetu wanashindwa kufanya maamuzi magumu?

Eeh nahisi presha inanipanda. ... Wacha niwaachie wanasiasa siasa zao chaaaa.
Njia sahihi ni Nkurunzinza kuachia ngazi na wafanye uchaguzi upya au waunde serikali ya mpito inayoshirikisha vyama vyote.

Naona tatizo ndo linaanzia hapo.... Nkurunzinza anakubali kuachika ngazi?
Je wakifanya uchaguzi upya wanae kiongozi ambaye wanamtaka na atawaongoza kwa amani?

Hapo pa serikali ya mpito naona ni kama kuunda serikali ya chamatawala na upinzani. ..... sijui kama kwenye uhalisia itakuja tokea
 
The Boss, yaani suluhisho halipatikani hadi mauaji yazidi hapo yaliyopo? Hawa raia wa kawaida haki yao ya kuishi iko wapi?

Basi watu wa haki za binadamu hawana usawa kwenye kutetea maisha na haki za binadamu.

Na hao marekani kipimo chao cha kuingilia kati na kusitisha hali ya mauaji ni hadi wake watu milioni 40?
Ngachoka kwakweli na siasa, kiukweli ndo maana siasa huwa siiwezi maana kuna vitu nataka vifanyike ambavyo kiuhalisia ndo suluhisho halafu havifanyiki kwa sababu za kisiasa.....

Link ni #VOA Burundi violence
 
Nyerere alisema mnategemea Burundi Marekani waingilie kwani kuna mafuta kule?
 
Hawa jamaa vita imo damuni mwao, toka wanapata uhuru mpaka sasa ni mwendo wa mtutu tu.

Mizizi ya vita isipofukunyukuliwa kamwe vita haiwezi kuisha humo Burundi, nakumbuka Nyerere alihangaika nao sana hawa jamaa tangu miaka ya 70 mpaka anakufa.

Mandela ackachukua kijiti, na sasa Mkapa lakini tatizo liko pale.

Washukuru sana Tanzania ambayo huwabeba kama ndugu zao bila kuangalia inanufaika na nini kutoka kwao, siku na sisi tukianza kuangalia maslahi yetu tukaweka undugu pembeni watachinjana kama kuku hawa watu.

Ni nani anatakiwa kufukunyua hiyo mizizi ya vita na kumaliza mauaji?

Siasa kwakweli mie huwa siielewi kabisa yaani kuna muda unaona mambo hayaendi sababu utaambiwa political reason..... khaaaa.
 
Yaani nikifika hapo ndo huwa nachoka kabisa na mambo ya siasa, yaani nashindwa kuelewa...... ni mchezo gani huu unaohusisha damu? Tena ya binadamu.....

Kwa mtindo huu mpenzi, mgombea wa uraisi wa marekani alivosema waafrika hawawezi kujitawala ni watawaliwe milele alikosea? Kwa nini viongozi wetu wanashindwa kufanya maamuzi magumu?

Eeh nahisi presha inanipanda. ... Wacha niwaachie wanasiasa siasa zao chaaaa.

Naona tatizo ndo linaanzia hapo.... Nkurunzinza anakubali kuachika ngazi?
Je wakifanya uchaguzi upya wanae kiongozi ambaye wanamtaka na atawaongoza kwa amani?

Hapo pa serikali ya mpito naona ni kama kuunda serikali ya chamatawala na upinzani. ..... sijui kama kwenye uhalisia itakuja tokea
Inavyoonyesha Nkurunzinza ni ngumu kuachia ngazi labda pawe na ushawishi mzito.
Vinginevyo kwake haya mauaji hayamshtui as long as anabaki kuwa rais, kwake yeye urais ni muhim kuliko usalama wa raia, tunazungukwa na majirani wa ajabu mno na wenye roho ngumu.
Jaribu ku google uone mtiririko wa kurithiana madaraka ulivyo kwao, ni kupinduana na kuuana, so hata mazungumzo ya mezani kwao sio suluhuhisho la kudum japo yaweza kuleta nafuu ya muda mfupi
 
Nyerere alisema mnategemea Burundi Marekani waingilie kwani kuna mafuta kule?
Hapo ndo nnapowaona hawa watu wa haki za binadamu hawako sawia? Kama nchi haina maslahi basi wananchi wake nao thamani inaishia hapo.

Hivi Syria napo inakuweje? Niko hakuna maslahi? Maana ile vita nayo haiishi kila leo mabomu upya.

Watoto wanakufa wamama wanalia wakimbizi wananyanyasika...... yaani ni dhiki bin shida.
 
Eastern DRC zaidi ya watu milioni 2 wamekufa..
Sanasana wazungu wanajadili namna ya kuwaokoa sokwe wa Eastern DRC...
hawana shida binaadamu akifa
 
Inavyoonyesha Nkurunzinza ni ngumu kuachia ngazi labda pawe na ushawishi mzito.
Vinginevyo kwake haya mauaji hayamshtui as long as anabaki kuwa rais, kwake yeye urais ni muhim kuliko usalama wa raia, tunazungukwa na majirani wa ajabu mno na wenye roho ngumu.
Jaribu ku google uone mtiririko wa kurithiana madaraka ulivyo kwao, ni kupinduana na kuuana, so hata mazungumzo ya mezani kwao sio suluhuhisho la kudum japo yaweza kuleta nafuu ya muda mfupi
mkuu siku Nkurunzinza akiachia hio nchi, Burundi inarudi kwenye historia yake ya mwaka 2003.

Nadhani katika historia ya Burundi, Nkurunzinza ni moja ya Marais Bora sana, kaituliza mno nchi yake pamoja na umasikini mkubwa walio nao.

Chimbua historia ya Burundi tangu inapata uhuru, utaligundua hili
 
Inavyoonyesha Nkurunzinza ni ngumu kuachia ngazi labda pawe na ushawishi mzito.
Vinginevyo kwake haya mauaji hayamshtui as long as anabaki kuwa rais, kwake yeye urais ni muhim kuliko usalama wa raia, tunazungukwa na majirani wa ajabu mno na wenye roho ngumu.
Jaribu ku google uone mtiririko wa kurithiana madaraka ulivyo kwao, ni kupinduana na kuuana, so hata mazungumzo ya mezani kwao sio suluhuhisho la kudum japo yaweza kuleta nafuu ya muda mfupi

Ndo maana nikasema kwanini umoja wa afrika usiingilie kati na kuwaondoa wanasiasa wote na kuwaacha wananchi Waishi kwa amani? Hao viongozi wote wa siasa wa Burundi wao na familia zao wapelekwe nchi za uhamishoni kuishi huko na pale waache kizazi hata cha 5 tangu kina Nkurunzinza kipite ndo wafanye uchaguzi. Hapo natumai mizizi ya mauaji na kurithishana madaraka yatakuwa yamekoma.
 
Back
Top Bottom