Mauaji yakutisha yawaandama makada wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji yakutisha yawaandama makada wa CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, May 17, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Limeibuka wimbi la mauaji ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mazingira yanayoacha shaka kwamba huenda kuna mikono ya kisiasa katika vitendo hivyo.

  Wakati wakazi wa Jiji la Mwanza wapo katika simanzi kubwa ya kumpoteza Katibu wa CCM Kata ya Isamilo, Bahati Stephano (49), aliyeuawa kikatili kwa kuchomwa kisu ofisini kwake na mtuhumiwa aliyetambuliwa kwa jina la Jummane Oscar (30),

  na baadaye kifo cha mwanamke aliyekuwa ametangaza nia ya kuomba uteuzi wa kugombea ubunge katika jimbo la Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Nsega Aloyce Ntobi kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

  Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Salama A, kata ya Salama wilayani Bunda, Messo Kubuka (46), kupitia CCM naye ameuawa kinyama baada ya kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.

  Imedaiwa kuwa Mwenyekiti huyo alikutwa na mauti hayo baada ya kutoka katika mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Bunda ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.
   
 2. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Kuna katibu wa CCM wa Kata ya Isamilo ameuawa kwa kuchomwa na kisu ofisini kwake majira ya saa 6:30 mchana, muaji amekamatwa na kuhojiwa na jeshi la polisi na inasemekana ametaja waliomtuma ambao ni wapambe wa Meya wa Jiji la Mwanza.


  Mauaji ya katibu wa CCM yachukua sura mpya

  Sunday, 16 May 2010 20:04

  Frederick Katulanda, Mwanza

  SAKATA la Katibu wa Chama Cha Mapinmduzi (CCM) kata Isamilo ,Bahati Stephano (50) kuuawa kwa kuvamiwa na kuchomwa kisu limepata sura mpya baada ya kampeni meneja wa kigogo mmoja jijini hapa kukamatwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji.

  Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro alisema mbali na mtuhumiwa aliyekamatwa siku ya tukio, mpaka sasa watuhumiwa wengine wawili wamenaswa na jeshi lake.

  Wakati jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mbunge wa Nyamagana, Lawrance Masha amesema kifo cha katibu huyo sio cha mapenzi ya Mungu bali mkono wa mtu.

  Masha alisema hayo wakati wa kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa marehemu Kilimahewa jijini Mwanza kabla jana mwili wake kusafirishwa kwenda katika kijiji Busiri wilayani Ukerewe kwa mazishi.

  Masha alisema imekuwa ni mazoea katika misiba kusema ni mapenzi ya Mungu, lakini kwa msiba wa katibu huyo sio wa mapenzi ya Mungu.

  "Mara nyingi tunapokutana katika matukio kama hayahusema mapenzi ya Mungu, kifo cha bahati sio mapenzi ya Mungu ndio sababu jeshi la polisi linachunguza," alisema Masha.

  Alisema akiwa kama waziri atasimamia jeshi linawasakawauaji wote na kuwafikisha mahakamani.

  Kamanda Sirro alieleza walimkamata aliyeua na pia wamekamatwa wanaodaiwa kumtuma kufanya tendo hilo.Sirro alisema jeshi lake litatoa taarifa kamili kesho ikiwa na kubainisha chanzo cha mauaji hayo.
   
Loading...