Mauaji ya mwandishi Kashoggi....Saudia Matatani.


Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Messages
2,615
Likes
2,710
Points
280
Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2017
2,615 2,710 280
Upelelezi Nchini Uturuki wabainisha kuwa Mwandishi wa Habari Mr. Jamal Khashoggi aliuliwa baada ya kuhojiwa, alipoingia Ubalozi wa Saudia Arabia kisha mwili wake ukakatwa mapande !!My take:
Hii inamaanisha saudi arabia imemuua mwanahabari huyo aliyekuwa amekimbilia nchini uturuki akihofia maisha yake kutokana na kuingia kwenye mzozo na serikali ya saudi Arabia.. mr Jamal alikuwa mkosoaji kubwa wa sera za mambo ya nje za serikali ya saudi Arabia hasa mauaji ya raia yanayofanywa na ndege vita za saudi arabia huko yemen..

Mwanahabari huyu alikuwa katika harakati za kuoa na alienda na mchumba wake katika ubalozi wa saudi arabia ili apate clearance form ambayo zitaonyesha kuwa ana vigenzo na anastahili kufunga ndoa..

Mr Jamal alienda na mchumba wake ubalozini ila akamwacha nje ya ubalozi nae akaingia ndani,mchumba wake alipoona mume wake mtarajiwa amechelewa kutoka ndipo akatoa taarifa polisi na hali hiyo ikaamsha mgogoro mpya wa diplomasia kati ya uturuki na saudi Arabia...

Uturuki inasema ina ushahidi kuwa maafisa wa ubalozi huo wakimtesa na kumuua bw khashoggi pamoja na kumkakata vipande na kuundoa mwili wake toka ubalozini ndani ya mabegi maalum.. uturuki inasema Mr Jamal alivaa saa maalumu iliyokuwa imeunganishwa na simu yake aliyoiacha ndani ya gari na ikawa inarekodi video zote ndani ya ubalozi wa saudi arabia katika kile alichokuwa anatendewa...

Duru za kijasusi ndani ya uturuki zinasema siku ya tukio maafisa wa kidiplomasia 15 wa saudi waliwasili uturuki na ndege maalumu na waliondoka na mizigo maalumu ambayo hata hivyo haikukaguliwa airport coz begi za kidiplomasia uwa hazifanyiwi ukaguzi.. uturuki inaamini maafisa hao 15 walitumika kuuondoa mwili wa Mr Jamal toka uturuki hadi saudi arabia ndani ya viroba..

Marekani imeapa itaiadhibu kwa vikwazo saudi arabia iwapo itagundulika imemuua mwanahabari huyo, nayo saudi arabia imeapa kulipiza kisasi iwapo itawekewa vikwazo na marekani au NATO..

Wadau wengi wana wasiwasi kama marekani inaweza kuiadhibi Saudi Arabia ukichulia saudi Arabia ni mteja mkubwa wa silaha za marekani hasa ndege vita na mitambo ya ulinzi wa anga..

Marekani pia ina kambi kubwa ya kijeshi pale Saudi Arabia ikilinda maslahi yake ya mafuta..
 
Proved

Proved

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
1,258
Likes
930
Points
280
Proved

Proved

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2018
1,258 930 280
Saud Arabia must learn the hard way
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
9,158
Likes
8,897
Points
280
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
9,158 8,897 280
The Custodian of the Two Holy Mosques! Ndio hao waliamrisha hayo mauwaji na kupeleka nyama zake Saudia zikiwa kwenye mabegi. Waarabu; viumbe makatili zaidi chini ya Jua huku wakihubiri dini.

Kuna mijitu kabisa itashangilia na kufurahia zawadi za tende na nyama toka Serikali ya Saudia.
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
9,924
Likes
1,503
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
9,924 1,503 280
The Custodian of the Two Holy Mosques! Ndio hao waliamrisha hayo mauwaji na kupeleka nyama zake Saudia zikiwa kwenye mabegi. Waarabu; viumbe makatili zaidi chini ya Jua huku wakihubiri dini.

Kuna mijitu kabisa itashangilia na kufurahia zawadi za tende na nyama toka Serikali ya Saudia.
Waarab na waisrael ni watu wa ajabu sana mkuu na ndio maana hiyo inayoitwa mitume ilipelekwa kwenye jamii zao.
Nalog off
 
kambagasa

kambagasa

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2014
Messages
2,012
Likes
926
Points
280
kambagasa

kambagasa

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2014
2,012 926 280
The Custodian of the Two Holy Mosques! Ndio hao waliamrisha hayo mauwaji na kupeleka nyama zake Saudia zikiwa kwenye mabegi. Waarabu; viumbe makatili zaidi chini ya Jua huku wakihubiri dini.

Kuna mijitu kabisa itashangilia na kufurahia zawadi za tende na nyama toka Serikali ya Saudia.
Asalam alekhum
 

Forum statistics

Threads 1,236,724
Members 475,218
Posts 29,267,320