Mauaji ya ccm yamepata msamiati mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya ccm yamepata msamiati mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwinukai, May 18, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hatimaye mauaji ya CCM yamepewa msamiati mwingine zaidi baada ya mbunge wa Ludewa kusema wakati akihutubia wapiga kura wake waliokwenda kumpokea kuwa

  ‘’ hata kama wakinikolimba leo wataibuka akina Zitto wengi kupinga ufisadi’’

  source habari ITV Tar. 14/5/2011 kauli hii ya mbunge wa CCM imekuja siku chache baada ya Nape Nauye kumpinga Mwenyekiti wa CHADEMA kuwa tuhuma anazotoa dhidi ya CCM kuhusika na Mauaji ni kufilisika kisiasa. sasa kama hata mbunge wa CCM anajua kuwa CCM inaua Je Nape ana usemi mwingine zaidi ya hapo?

  kutokana kuwa HORACE KOLIMBA alikuwa mbunge wa Ludewa na kifo chake kilizua maswali kilivyokua chenye utata, Je Serikali ya CCM haioni sasa ni wakati wakusimama na kutoa utata ulioibuliwa na Mbunge huyu?
   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Wakimkolimba mbunge wa Ludewa, wananchi watawakolimba 2015.
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Na hili ndilo kosa la watu wa LUDEWA licha ya CCM kukolimba mbunge wao HORACE KOLIMBA bado tumendelea kuishikilia CCM ambayo mpaka sasa inakolimba maendeleo ya Ludewa na Nchi kwa ujumla.
   
 4. Kakati

  Kakati Senior Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mbaya sana wanapowakolimba watu wa maana badala ya vihiyo. Kumbuka kihiyo na ukihiyo kama msamiati tayari haujadiliki tena. Umeota mizizi ya kutosha tangu kiongozi mmoja mbumbumbu aliposhushuliwa kwa kugushi. Kama kuna anayekumbuka msamiti mwingine wenye hadhi kama hizi atukumbushe. Kaaaaaaaaaazi kwelikweli!
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  deo's life is in danger
   
 6. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kisha nikaona mnyama akitoka baharini. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba na taji kumi kwenye pembe zake. Na kila kichwa kiliandikwa jina la kufuru. 2Huyo mnyama alifanana kama chui lakini miguu yake ilikuwa kama ya dubu na kinywa chake kama cha simba. Lile joka lilimpa mnyama huyo nguvu zake, kiti chake cha enzi na uwezo mkuu. 3Kichwa kimoja cha huyo mnyama kilione kana kama kilikwisha kuwa na jeraha lisiloweza kupona, lakini jeraha hilo lilikuwa limepona na dunia nzima ilimstaajabia huyo mnyama na kumfuata. 4 Watu waliliabudu lile joka kwa sababu lilikuwa limempa huyo mnyama uwezo wake. Pia walimwabudu huyo mnyama wakisema, ''Ni nani aliye kama huyu mnyama? Ni nani awezaye kupigana naye?''

  5 Kisha huyo mnyama akaruhusiwa kusema maneno ya kujisifu na ya kufuru na akapewa haki ya kutawala kwa muda wa miezi arobaini na miwili. 6 Alisema maneno ya kumkufuru Mungu, akilitukana jina lake na mahali aishipo, yaani, aliwatukana wale waishio mbinguni. 7Pia aliruhusiwa kuwapiga vita watu wa Mungu na kuwashinda. Alipewa uwezo juu ya watu wa kila kabila, kila ukoo, kila lugha na taifa. 8Na watu wote waishio duniani watamwabudu, yaani kila mmoja ambaye tangu kabla ya ulimwengu kuumbwa, jina lake haliku andikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo aliyechinjwa.

  9. Aliye na nia ya kusikia, asikilize kwa makini: 10. Yeyote aliyepangiwa kuchukuliwa mateka atatekwa. Mtu ye yote akiua kwa upanga atauawa kwa upanga. Na hii ndio nafasi ya watu wa
  Mnyama Kutoka Ardhini
  11Kisha nikamwona mnyama mwingine akipanda juu kutoka katika ardhi. Alikuwa na pembe mbili kama za mwana kondoo lakini aliongea kama joka. 12Naye alitumia uwezo wote wa yule mnyama wa kwanza aliyemtangulia. Akalazimisha dunia yote na wote waliomo duniani wamwabudu huyo mnyama wa kwanza aliyekuwa na jeraha la kifo lililokuwa limepona. 13Huyu mnyama wa pili akafanya miujiza ya ajabu hata kufanya moto utoke mbinguni na kushuka duniani mbele ya watu. 14Kwa njia ya miujiza aliyowezeshwa kufanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, aliwadanganya watu waishio duniani. Aliwaamuru watengeneze sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi. 15Kisha akawe zeshwa kuipatia pumzi ile sanamu ya mnyama wa kwanza hata ikaweza kuongea na kufanya wale wote ambao hawakuiabudu wauawe. 16Pia aliwalazimisha watu wote, wakubwa kwa wadogo, matajiri na mas kini, watu huru na watumwa, watiwe alama kwenye mikono yao ya kulia au kwenye vipaji vya nyuso zao. 17Hakuna mtu ye yote ambaye angeweza kununua au kuuza kitu kama hana alama ile, yaani jina la huyo mnyama au namba ya jina lake.

  18Jambo hili linahitaji hekima. Mwenye akili ya kutambua apige hesabu ya mnyama huyo kwa sababu ni namba ya mtu. Namba yake ni mia sita sitini na sita ''666''.
   
 7. B

  Bubona JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa nini alitoa hii kauli? Kuna nini nyuma ya pazia?!!
   
 8. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Alikuwa akiwahamasisha wapiga kura wake kuachana na woga katika kutetea maslahi ya Nchi, ndio akatoa kauli hiyo...
   
Loading...