Tetesi: Mauaji: Mwenyekiti wa kijiji Kimanzichana-Mkuranga auwawa kwa kupigwa risasi.

shaks001

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,246
1,070
Kwa taarifa nilizozipata kutoka chanzo kilichopo eneo husika,ni kwamba Mwenyekiti wa kijiji cha kimanzichana wilaya ya Mkuranga,amepigwa risasi na watu wasiojulikana na kujeruhi Mzee mwingine wa kijiji hicho ambaye mpaka sasa amekimbizwa Hospital ya Taifa ya Muhimbili baada ya kufikishwa hospitali ya Wilaya Mkuranga.

Tukio hili limetokea jana jioni na kwa taarifa zilizopatikana ni kwamba watu hao hawakuchukua chochote.Na inasemekana ni muendelezo wa wa viongozi wa vijiji hivyo kuvamiwa na watu wenye misimamo mikali(kidini)waliotajwa kwenye sakata la kinachoitwa "ugaidi" na "magaidi"kilichotokea miezi michache huko kimanzichana na Bupu.

Nitaendelea kuwajuza!
 
Kheeeeeee!!

Maajabu ya mwaka haya!!

Kumbe hata wala vumbi wanatandikana risasi?

Basi Tanzania haifai kabisa...wala vumbi kimbilieni Rwanda.

:D:D:D:D:D.
 
Pokea pole zangu kwa niaba ya wala vumbi wenzio.

Fanyeni mhamie Rwanda.
sawa mbeba mabox.kawasaidie wenzako kupiga box wacha wala vumbi tuisome number lakini kumbuka kwenu kuanzia jf izindiliwe hajawahi kusifia au kusema chochote kuhusu home so remember home some time

moving-house-four-men-loading-a-removals-lorry-with-cardboard-boxes-AYKN9W.jpg


swissme
 
Yaani hata kupigwa risasi nalo ni tukio linahusishwa na ugaidi? Yale mambo ya zamani mtu akiuwawa ilikuwa inahusishwa na visasi na kudhulumiana sasa mabadiliko ya tabia nchi yamehamia hata kwa binadamu. Ukiuwawa ni ugaidi., kazi ipo.
 
Back
Top Bottom