Jamaa wote walikuwa ni wafanyibiashara pale kariakoo. garments. Walikuwa wankwenda nje nje kufuata mizigo yao wenyewe(they were successful) Na wote ni marafaiki na waote wanatoka Kibosho. Mengine siwezi kueleza maana ni hear say!
Ama hakika Dunia imeisha! Maana imeshuhudiwa watu wawili wakipigwa risasi live mbele ya familia za bila hata wao wenyewe wala familia zao kujitetea!!( Soma nipashe ya Jumapili). Mimi bahati niko jirani na waliouliwa! na wauaji walifyatua risasi na Shortgun zao kutishia raia wema kusogea maeneo ya tukio.
Wa kwanza aipigwa risasi sebuleni na kuvutiwa chumbabi huku damu zikichuruzika, wa pili alifumaniwa gaetini akiingia na gari lake kutoka katika shughulu zake. Matukio yote yalipishana kama 30 minutes.
Maana majirani tumebakia midomo wazi hatujui tuanzie wapi ama kumalizaia wapi. Na hii si mara ya kwanza matukio kama hayo kuripotiwa. Je yawezekana turudishe enzi za Lyatonga mrema (SUNGUSUNGU) ambapo kila ikifika saa1 jioni kila mwanaume anakuwa nje? Maan kutegemea Polisi tu naona haitoshi! Naomebeni ushauri:confused2:
Na mimi nasema usimwamini mtu ye yote kupita kiasi.1.ulinzi na usalama wa watanzania upo mikononi mwa watanzania wenyewe.....sungusungu ni muhimu.
2.Unapofanya biashara,jitahidi sana USIMDHULUMU mtu yeyote(sijasema marehemu walidhulumu)
3.Ni hatari pia kudisclose unaishi wapi kwa kila mtu,eti kisa wajue unanyumba nzuri na ni tajiri.
4.Wale watakaojua unaishi wapi si vizuri wakajua unafanya nini.
5.Kuna SUPER DEALS ambazo mtu akikudhulumu huwezi kwenda polisi,kwa mfano umedhulumiwa tani moja ya madawa ya kulevya utashitaki wapi?(sina maana wamedhulumiana)
6.Ni kosa pia kumuachia mtu kiasi kikubwa cha pesa tasilimu za biashara labda akakununulie bidhaa au akalipie malipo fulani.
tumia hundi siku zote. FIKIRIA ukifa ghafla itakuwaje?
7.Mshirikishe mungu katika biashara zako hasa kwa kutoa zaka.Kwa kufanya hivyo Mungu anakuwa mbia/share holder....na si unajua ulinzi wake mungu?
8.Mwisho usimwamini mtu yeyote,ndio i mean mtu yeyote hapa duniani.mke,mzazi,rafiki.....mchungaji,shehe...
.
HAYO NI MAWAZO YANGU.................POLENI SANA WAFIWA..
Sungusungu yawezekana Tatizo ni ku mobilse watu!!
Na mimi nasema usimwamini mtu ye yote kupita kiasi.