Mauaji Kibiti Rufiji Mkuranga Busara itumike kutatua tatizo bila kuzidisha chuki

yeto

Member
Aug 23, 2010
59
40
Habari waungwana

Tushauriane busara gani itumike kukomesha mauaji ya watumishi wa serikali maeneo haya?

Kuna haja busara itumike kutafuta mzizi wa tatizo hili na suluhisho la kudumu kwani katika kanda hiyo kumekuwa na matukio ya vurugu kwa miaka karibia mitano iliyopita na mara nyingi walengwa wamekuwa watumishi wa serikali .
Kwasasa imekuwa ujambazi ikilenga watumishi hao hao wa serikali
Juhudi za polisi mara nyingi zinatuliza kwa muda tu halafu inatokea tena
Ingawa waziri ametaja maeneo hayo tu mi naona hali hiyo inafanana maeneo mengi ya ukanda huo ambapo kulikuwa na vurugu na watumishi wa serikali walishambuliwa.

Baadhi ya matukio yanayotokea kanda hiyo
Kibiti: Polisi watumia helikopta kuzima vurugu!
Vurugu Mtwara: Wabunge waangua vilio;
VURUGU TANDAHIMBA

Alichokiongea waziri




Unatakiwa ufanyike uchunguzi wa kitaalam kwa nini wananchi wa kawaida wanachukia viongozi ambao wengine wanawachagua wenyewe kama wenyekiti wa vijiji ambao pia inasemekana wanauwawa.

Pamekuwa na sababu nyingi kama Gesi ,kutolipwa korosho na kutouza mkaa nk

Nini kifanyike ili wananchi wawe na Imani na watumishi wa serikali na Jeshi la polisi kwa jumla. Kituo cha polisi kuvamiwa na polisi kuuliwa bila msaada kutoka kwa wananchi si ishara nzuri. Je kuna umhimu wa kutumia polisi jamii sehem kama hizi

Matukio ya zamani yalikuwa ni vurugu za watu wote kwa sasa zimekuwa za baadhi au kikundi cha watu ambapo inatia hofu zaidi .

Je hawa wahalifu ni wa kina nani na wanamalengo gani. Tusipotumia busara hili kundi litaongeza wafuasi ambao ni hatari kwa taifa letu



Tujikumbushe matukio mengine ya huko

Kituo cha Polisi Ukonga Stakishari chavamiwa na Majambazi



Tetesi: - Mauaji: Mwenyekiti wa kijiji Kimanzichana-Mkuranga auwawa kwa kupigwa risasi.
 
Ushirikiano haba wa Polisi na wananchi unaweza kuwa ndio chanzo cha yote hayo.
Kuna haja Polisi kuangalia upya mahusiano na wananchi ambao wengi ndio chanzo cha kufikisha taarifa za kiiteljensia.Kuna mawazo hasi hivi sasa kati ya polisi na wananchi kutokana na jeshi kuendeshwa kisiasa mno na kusahau majukumu ya msingi (shutuma za ukusanyaji mapato uliopitiliza kwa njia ya faini na kutumika kukandamiza wapinzani,shutuma na madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuua washukiwa wa ujambazi kabla ya kupelekwa mahakamani wakiwa mikononi mwao).Athari ya hayo ni kuuawa kwa ndugu, kaka na dada zetu wa waliovaa sare za jeshi la Polisi.
 
Hakuna cha ujambazi wala nini sijui? Mimi nakichukulia tukio hili ni la kigaidi na kisiasa na kwa bahati mbaya inaelekea baadhi ya wakazi wa vijiji wana support vitendo hivi vya mauuji haya ya Viongozi wa vijiji vile vile na wafanyakazi wa vyombo vya Usalama - trend hii inajirudia rudia mara kwa mara kwenye kanda hiyo ya pwani - utasikia leo Ukonga staki shari, kesho Rufiji keshokutwa Mukuranga mtondogoo Tanga na ukiangalia modus operandi ni ile ile kama inayo tumiwa na magaidi maana ni mara chache kuiba hela/fedha.

Binafsi nasikitika kusema sioni kama Wizara ya mambo ya ndani ina mikakati thabiti ya ku deal na tishio hili la uvunjifu wa amani i.e kuwabaini ni akina nani wako nyuma/finacing kundi hili hatarishi na kuwakomesha mara moja.

Alternatively Jeshi la Polisi na JWTZ washirikiane kwenye operation maalumu ya "tokomeza Ugaidi" lakini tikijidanganya na kulichukulia suala hili kama uharifu wa kawaida hatutafika mbali.
 
Back
Top Bottom