Mauaji katika ngome ya Hezbollah

Mauaji katika ngome ya Hezbollah

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,956

131119115932_blast_afp-1.jpg

​
Takriban watu 22 wameripotiwa kufariki katika milipuko miwili ambayo ililenga ubalozi wa Iran mjini Beirut, mji mkuu wa
Lebanon

131119115934_blast_afp-2.jpg

​
Afisaa mmoja mkuu katika ubalozi huo Ebrahim Ansari alikuwa miongoni mwa waliofariki. Maafisa wamesema kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka



131119115936_blast_ap-3.jpg

131119115936_blast_ap-3.jpg
Picha nyingi za mashambulizi hayo zilionyesha magari yakiteketea pamoja na miili ya watu ikiwa imetapakaa kwenye barabara za eneo hilo. Majumba pia yaliharibiwa vibaya






131119115938_blast_ap-4.jpg

​
Iran inaunga mkono kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Hezbollah ambalo limewapeleka wapiganaji nchini Syria kuunga mkono serikali ya Rais Bashar al Assad.



131119115940_blast_afp-5.jpg

​
Duru zinasema kuwa moja ya milipuko hio, ilisababishwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga, wakati shambulio la pili lilitokana na bomu lililokuwa limetegwa ndani ya gari.


 

131119115942_blast_reuters-6.jpg

​
Shirika la habari la Reuters linanukuu kituo cha televisheni cha CCTV, kikionyesha mwanamume
mmoja akikimbia kutoka katika ubalozi wa Iran na kisha kujilipua


131119115944_blast_reuters-7.jpg
Balozi wa Iran nchini Beirut alithibitisha kifo cha bwana Ansari, ingawa haijulikani ikiwa alikuwa ndani ya ubalozi au katika jengo jirani


131119115946_blast_ap-8.jpg
​
Syria imelaani vikali mashambulizi hayo. Mgogoro wa kisiasa nchini Syria umechochea kuongezeka kwa hali ya wasiwasi nchini Lebanon.











 
Back
Top Bottom