Natumai mko vyema, naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika,
Mimi ni mtumishi wa wajamii, najihusisha na Utabibu wa binadamu....
Natamani kuwa mjasiriamali mbali na taaluma niliyo nayo, naomba kufahamu kutoka kwa watu mbali mbali humu kuhusu soko la maua yanayotengenezwa kwa ribbon, nitaonyesha sample hapo chini..... Likoje?
Kwasababu hili wazo kwa gharama ya kuanzia baada ya kupiga hesabu ni kianzio ni kama 100000 au chini ya hapo kwasababu ribbon moja ni shilling 3500 na inauwezo wa kutoa maua hata 4-5 kwa bei ya jumla mfano ua moja shilling 2000x4=8000 kwa kila ribbon.
Mwenye experience na hivi vitu wakuu msaada tafadhali.
Youtube ina tutorial video nyingi, anzia kule, tengeneza Maua mengi ukiwa na stoo yako nyumban, yahifadhi vizur. Yakijaa then fungua fremu yako , pata lesen na anza kufanya biashara.