Matuta barabarani yaondolewe

Matuta barabarani yaondolewe

pembe

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
2,156
Reaction score
731
UWEZEKANO WA KUONDOA MATUTA BARABARANI

Sehemu ya barabara iliyojengwa na kampuni ya Kijerumani mkoani Tanga (Dar-Arusha) haina matuta. Kuna alama zote za barabarani zinazostahili.

Tangu ianze kutumika sijasikia ajali imetokea kwa sababu hakuna matuta.

Wataalamu wa wizara ya Ujenzi waangalie uwezekano wa kuondoa matuta barabarani kwani yanaumiza magari madogo na mgongo kwa wanaopanda mabasi!
 
Matuta ni physical measure, ni interpretation that watu hawana uwezo wa kufuata sheria bila ya shuruti. Hiyo ndiyo tafsiri ya kila mtu anapokuja Tanzania. Ni aibu kwa nchi, ni aibu kwa wananchi wake.
 
Wataalamu wa wizara ya Ujenzi waangalie uwezekano wa kuondoa matuta barabarani kwani yanaumiza magari madogo na mgongo kwa wanaopanda mabasi!
Matuta ya Bara bara ya Shinyanga - Mwanza ndio funga kazi. Usiombe uwe umepanda basi alafu umekaa siti ya nyuma. Utafika kiuno chote kikiwa kimetenguka. Matuta ya bara bara ya Singida - Dodoma, ndio matuta bora kuliko yote nchi hii. Yani tuta unaweza ukalipanda na spidi sitini bila kurushwa sana. Yana umbo zuri na ni rafiki kwa gari.
 
Back
Top Bottom