Matusi, dharau na kelele za wapinzani ni zao la hasira ya kutodhaminiwa kwa hoja zao

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,477
2,000
Kwa muda mrefu nimekuwa mfuatiliaji wa siasa hasa za wabunge hapa Tanzania. Wakati bunge linarushwa mubashara vipindi vya jioni vilikuwa havinipiti na nilifanya jitihada kupata kila kilichojadiliwa!

Binadamu yeyote yule mahali popote pale hujisikia furaha sana pale anapothaminiwa au mchango wake kutambuliwa na waliomzunguka!(appreciation/recognition). Kinyume na hapo hujiskia huzuni na hali huwa mbaya zaidi pale anapobaguliwa kwa makusudi bila sababu za msingi.

Ukiangalia maisha ya kisiasa ya wanasiasa wa upinzani, ni maisha yaliyojaa huzuni hiyo! Muda mwingi wanapoongea, hutanguliza kabisa tahadhari ambayo msingi wake ni kwamba huenda wachoongea hakitafanyiwa kazi!

Nakumbuka wakati shangazi yangu anaolewa miaka miwili iliyopita, alisahau kutambua uwepo wa babu yetu aliyemlea (ki umri si mzee ila tunamuita babu kama cheo) wakati wa utambulisho! Babu yetu huyo anahuzuni hadi leo kila anapokumbuka wenzake walivyopigiwa vigelegele wakati wa utambulisho na jinsi kamera za siku hiyo zilivyo wang'arisha! Huyo babu, amechangia kwa kiasi kikubwa cha mafanikio aliyonayo huyo shangazi huyo.

Nimezoe kuwasikia wapinzani hasa Ndg. Zitto Kabwe, John Mnyika, Godbless Lema, Tundu Lisu, Peter Msigwa na wengine wengi wakiongea vitu vya msingi kabisa kuendeleza nchi yetu ambavyo havitamkiki na wabunge wa chama tawala. Pamoja na hayo, sina hakika sana kama serikali na viongozi wa bunge huwa wanajali sana yanayosemwa na wabunge wa upinzani! Nasema sina hakika hiyo!

Ingekuwa chama tawala kina wabunge angalau kumi wenye uthubutu wa kutumia akili na uwezo wao vizuri kama wa Mh. Hussein Bashe, ningeunga mkono kwa asilimia zote za Mh. Spika kuwafungia na kuwa - "harass" wabunge wa upinzani kama anavyofanya.

Si ungi mkono hata kidogo vitendo vya wabunge wa upinzani kutoa matusi mara kwa mara wawapo bungeni, kuonyesha dharau kwa viongozi wa bunge wala kusababisha vurugu wakati wa vipindi vya bunge! Hoja yangu ni kuangalia chanzo cha matendo hayo na kutafuta suruhu ya kudumu!

Nina uhakika kabisa kama hoja za wabunge hao zingekuwa zinathaminiwa na malalamiko yao yanatekelezwa kwa wakati na kwa usahihi kama wanavyofanyiwa wenzao vitendo vya vurugu bungeni vingeisha kabisa. Bunge letu limefikia hatua mbunge wa upinzani akisimama kutoa hoja upande wa pili wanasubiri kutafuta namna ya kumkosoa na kuitetea serikali kana kwamba wabunge wote wa chama tawala ni mawaziri!

Mimi kwa mtazamo wangu, watu wakumsaidia Spika kuwa na uamuzi sahihi katika kudumisha nidhamu bungeni ni wabunge hasa wa chama tawala kuacha kujivika u waziri na kuitetea serikali na kujiona kwamba hakuna mbunge aliyejuu ya mwenzake!

Tuwaze kwa sauti tu, hivi kwa mfano wabunge wote wa upinzani wakiungana wote kwa pamoja wakasema kwamba kwa vile hata wakiongea hoja zao zinaonekana matope na wenzao wanapoonekana kukosewa na wabunge wa chama tawala uongozi unajifanya kutosikia wala kuona japo Spika alishatamka bungeni kuwa hata mbunge akijikuna anaonekana na system
zilizowekwa, wote kwa pamoja waaachane na bunge hadi 2018 watakaporudi wenzeo waliofungiwa, hao watakao baki wataongea nini zaidi ya kubaki kusifia serikali na kuwapongeza mawaziri kwa kila kitu!??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom