Matusi bungeni: wadau walaani wabunge

Matusi bungeni: wadau walaani wabunge

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Dar na Dodoma. Wakati Spika wa Bunge, Anne Makinda akitangaza kuanza kuwatoa nje ya Ukumbi wa Bunge wanaotumia lugha za matusi,baadhi ya wanasiasa, wanaharakatina wanazuoni wamesema wabungewanatumia mamilioni ya kodi za wananchi, hivyo wanatakiwa kuheshimu hilo na kujikita zaidi kuzungumzia masuala ya msingi.
Juzi Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM), Juma Nkamia na Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde aliwapiga vijembe viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakisema kwamba kuna wabunge ambao wana “mimba zisizotarajiwa bungeni.”
Kutokana na hali hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Paulina Gekul akitumia Kanuni ya 68 (7), alikilaumu kiti cha Spika kwa kukaakimya wakati wabunge hao wanatukana bungeni.
Pia Moses Machali (Kasulu Mjini-NCCR-Mageuzi) na Magdalena Sakaya (Viti Maalumu-CUF) waliomba mwongozo wa Spika wakitumia Kanuni ya 64 inayozuia lugha za kuudhi bungeni.
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti Profesa Simon Mbilinyi alisema, “Wabunge hawa wanatumia vibaya fedha za walipakodi ambao wanaishi maishaduni, hawakuchaguliwa kwa ajili ya kupigana vijembe bungeni.”
Mwenyekiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Helen-KijoBisimba alisema, “Inaonekana hawajui cha kufanya wala kilichowapeleka bungeni.”
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiel Oluoch alisema kuwa moja ya mambo yaliyotakiwa kujadiliwa na wabunge hao ni pamoja na madai ya walimu ya muda mrefu.
“Walimu wanaidai Serikali Sh25 bilioni, kuna suala la kutokuwapo kwa mitalaa, haya yote hawayaoni wanaishia kutupiana vijembe tu,” alisema Oluoch.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Nchini (MAT), Dk Rodrick Kabangila alisema tatizo siyo wabunge, bali ni Spika, Makinda.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Prosper Ngowi alisema wabunge wanatakiwa kutambua kuwa wapo bungeni kwafedha za wananchi, hivyo wanatakiwa kulipa fadhila.
“Wananchi wanawategemea wabunge wasimamie haki na usawa na kujenga hoja za kutetea masilahi yao,naona 2015 ndiyo uwe muda wa wananchi kuchagua anayewafaa ,” alisema Profesa Ngowi.
Makinda kuwaitia polisi Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema iko haja ya kuwatenga na wanaotaka kutukanane na wale wastaarabu .
Alisema kitendo cha wabunge kujadili matusi huku wengine wakishangilia, kinaonyesha ni namna gani ambavyo watu hawako makini ndani ya jengo hili. Spika Makinda alitoa kauli hiyo jana asubuhi bungeni.

CHANZO: MWANANCHI
 
“Mheshimiwa Spika, sisi ambao ni chama tawala tufanye kazi, na kipimo chetu kiwe utendaji wetu…inashangaza tunaacha kuongoza tunafanya kazi za Nape Nauye, yeye atafanya kazi gani?

“Ndiyo maana kunatokea matusi bungeni kwani badala ya sisi kufanya kazi za wananchi tunafanya kazi za watu wengine,” DEO Filikunjombe (CCM)
 
Jana tu spika mama Anne Makinda amewataka wabunge kutotoa matusi wanapochangia bungeni bwamdogo Serukamba kalimwaga kama la kaka yake Juma Nkamia na pacha wake Kibajaji @ lusinde wa mteraaaa
 
Back
Top Bottom