Siku mbili zilizopita mtaani kwetu hasa katika sehemu ninayoishi yaani nilipopanga niliombwa msaada wa kufungua fb account, dada kanifuata na kuniaambia tafadha naomba unifungulie facebook account kwani mimi sifahamu!, sikua na kipingamizi nikaifungua lakini katka harakati nilijikuta ninaingiza email yangu ili kuhakiki.
MAJANGA; Baada ya siku mbili hizo yaani leo hii ya alhamis nikapokea ujumbe wa kasfa na matusi kutoka kwa bwana wa dada yule jamaa akidai, kwa nini nimechukua jukumu la kumfungulia demu wake facebook? katika kujitetea jamaa alizid kuporomosha matusi juu yangu akizidi kusisitiza hakutaka demu wake awe na fb hivyo kwa nini sikumuuliza kabla? nilijaribu kumuelewesha lakin wapi ilihali mimi simfaham na wala sijui kama huyo dada alikatazwa kuwa na fb. Je kosa la nani? nisaidien mawazo.