Matunda haya bongo yapo?

Unaweza kunitajia Majina ya haya Matunda?

Mkuu matunda yote hayo yapo Tanzania na mengi hupatikana milimani na sehemu za nyanda za juu (kaskazini na kusini).

Majina yake yameandikwa kwenye hizo picha ulizobandika (bottom left corner). Au ulikuwa unataka majina yake kwa kiswahili?
 
Mkuu matunda yote hayo yapo Tanzania na mengi hupatikana milimani na sehemu za nyanda za juu (kaskazini na kusini).

Majina yake yameandikwa kwenye hizo picha ulizobandika (bottom left corner). Au ulikuwa unataka majina yake kwa kiswahili?
Mkuu Kifyatu hayo Matunda niliyoweka Picha zake hapo juu hakuna nchini Tanzania wala bara la Afrika yapo Uarabuni na Bara la Ulaya



Haya Matunda yapo huku nje na uarabuni baadhi yapo huko nyumbani kwetu.
 

Attachments

  • Mediterranean Diet Foods Fruits.jpg
    56.2 KB · Views: 427
Mboga za Majani hizooooo

 

Attachments

  • Mediterranean Diet Food Vegetables.jpg
    53.4 KB · Views: 349
Mkuu Kifyatu hayo Matunda niliyoweka Picha zake hapo juu hakuna nchini Tanzania wala bara la Afrika yapo Uarabuni na Bara la Ulaya

Mkuu, matunda ulioweka hapo juu ni hayo niliyoyaorodhesha hapa chini ukifuatilia mstari mmoja baada ya mwengine. Mimi nilitembele na kuishi sehemu za Usambaa, Tanga na ndipo nilipokutana na haya matunda. Tunda namba 5 na 7 ndio unayoyakuta kwa wingi sokoni (Tanga au DSM). Haya mengine hayalimwi kwa wingi ili kufanya biashara lakini utaikuta miti yake kwenye nyumba za zamani za wakoloni - hasa wa kiJerumani.

Unajua, Tanzania kuna climatic zones zote zilizoko duniani. Unapotoka milimani (kama usambaani) na kuteremka kwenye tambarare utakutana na climate zones kutoka temperate hadi tropical. Ukienda Dodoma utakutana na hali ya jangwa na kuna matunda mazuri tu yanayopenda ukame yanajiotea porini na wenyewe hawayauzi sokoni. Nili-enjoy sana haya matunda nilipokuwa JKT Makutupora.

Matunda ulioweka hapo juu
1 Apricot---Apricoti (utakuta miti michache ya haya matunda kwenye nyumba za zamani za wakoloni usambaani)
2 Cherry----Cheri (micheri ipo usambaani lakini matunda yake mara nyingi yanaliwa na ndege. Kuna meupe/pink pia)
3 Fig--------Tini (haya yapo zaidi sehemu za Amani Tanga lakini sijayaona sokoni)
4 Kiwi-------Kiwi (haya utayakuta kati ya Amani na Muheza - Tanga.
5 Peach-----Pichi au fyoksi (wasambaa wanayaita mafyoksi - inashabihiana na jina lake kijerumani - Pfirsich)
6 Prune-----Pruni (hutumiwa kulainisha choo kama una constipation)
7 Plum------Plamu (matunda damu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…