Habari wanajamvi,
Ninapata shida kwenye kujua matumizi ya hilo nano hapo juu "tia fora". Neno hili naamini linatumika kuelezea ufanyikaji wa kitu kupita kiasi/kupiliza. Tatizo langu ni moja hapa, neno hili linatumika katika maana hasi tu ama linaweza kutumika katika mazuri pia.
Mfano:
1. Shule ile wamefeli mpaka wametia fora.
2. Katika watu waliochelewa nyie mmetia fora.
Naomba msaada je ninaweza kutumia neno 'tia fora' kusifia? Na mifano yake ikoje.
Nawasilisha