Chacha Steven Mokiri
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 2,008
- 2,232
Habari za wakati huu, wanajamvi, poleni na majukumu na utata wa swali la tiba ya CORONA. Naamini Mungu atasaidia... Cha msingi tuwe na imani tuombe sana na tufuate maelekezo ya wataalamu wa Afya kuliko kuhojihoji hovyo.
Sasa niende kwenye hoja yangu, matumizi ya maamkizi yanaleta mkanganyiko kutegemeana na asili na makuzi ya mtu na mtu, lakini je? Namna sahihi ya kutumia maamkizi ni ipi kama taifa kwa kanuni za kiswahili ukiachana na kabila.?Tunazingatia umri tu, au nafasi na cheo cha mtu?
Naomba nitoe mifano michache ili nieleweke:
1). Kuna mtu A na mtu B. Mtu A ana miaka mingi kuliko mtu B, lakini kwa sababu za kidunia na mapenzi, huyu mtu A anaoana na mtoto wa mtu B na kumfanya mtu A awe Baba mkwe! Hiyo inamaanisha nini? Mtu A ataanza kumsalimia mtu B na kanuni ya umri itapotezewa au ni namna nyingine?
2). Kuna mtu A ambaye ni babu wa mtu B. Sasaa mtu A anapata mtoto uzeeni. Huyo mtoto anakuwa mdogo kwa mtu B, lakini nafasi yake ni Baba Mdogo. Swali linakuja - Mtu B atamsalimia huyu mtoto wa mtu A na kupuuza ishu ya umri baadala yake azingatie nafasi/cheo?
Mifano ipo mingi, lakini naamini hii michache inatosha kuanzia. Karibuni tulichambue hili.