Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 12,037
- 24,851
Wakuu,
Kumekuwepo na ongezeko la threads(mada) humu JF hasa katika mfumo wa maswali ambazo naamini majibu yake yangeweza kupatikana kirahisi Google au kwenye search engines zingine. Wote tunajua matumizi ya google na kuna faida kadhaa za kutumia tovuti hii badala ya JF pale inapobidi; kwanza unaokoa muda wako na wa members wengine na pili unaokoa space kwenye servers za JF kwaajili ya mambo mengine ya msingi.
Mtu anaingia JF anatengeneza thread ya kuuliza lyrics za wimbo, au matokeo ya mpira, au tabia za mnyama fulani au picha ya gari, mtu au kitu fulani, na maswali kama hayo. Haya na maswali mengine mengi yangeweza kujibiwa kwa click moja tu kupitia google. Kama umeweza kuingia JF na kutunga uzi basi ungeweza kwenda google mwenyewe na kugoogle kitu husika na kuokoa nguvu na muda.
Nipende kutoa rai tuache uvivu wa kutaka kutafuniwa kila kitu na tujitahidi kutumia teknolojia iliyopo kwa mapana yake yote kurahiha maisha yetu na kupata maarifa ukizingatia karibu kila mtu ana smartphone siku hizi kuliko kujaza JF.