Matumizi ya Balozi Zetu kwa mwaka 2011/2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matumizi ya Balozi Zetu kwa mwaka 2011/2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Aug 1, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inaonyesha matumizi ya balozi zetu kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yatakuwa kiasi cha Shilingi za Tanzania kama ifuatavyo.

  • Ubalozi wetu Umoja wa Mataifa (New York na Geneva) pekee utatumia 5,051,259,000/-
  • Balozi zetu Ulaya ikiwemo Urusi - 12,481,913,000/-
  • Balozi kwenye nchi nne Africa Mashariki - 3,746,956,000/-
  • Balozi nyingine Afrika - 10,945,095,000/-
  • Fedha za matumizi ni nearly half of ministerial vote
  • Fedha zilizotengwa kwa mishahara ((Pensionable posts & non-pensionable) ubalozi wetu London ni 868,142,918/- (nyingi kuliko balozi zote)
  • Fedha za mishahara ubalozi wa Kigali ni 80,201,559/- (ndogo kupita balozi zote)
  Mchanganuo zaidi wa matumizi kwa kila balozi: The biggest spending Tanzanian Embassies - Budget 2011/12 | Policy Forum
   
 2. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hilo janga tena kwa taifa maana balozi zetu ukifika zinatia kinyaa hata kusema huu ndio ubalozi wangu kwa mfano ubalozi wetu China ukifika utazani kama hakuna watu wanaoishi pale mbaya zaidi ingia kwenye vyumba ndio utafikiria hata kutaka kutapika. aibu sana kwa nchi inayokamilisha miaka 50 bila kuwa na mipango ya maana balozi ni nchi ni kioo kwa hiyo sioni ajabu kama kunahela nyingi sehemu moja lakini ukweli utabaki palepale hii ni laaana wa haihitaji elimu nikuona nakujua hakuna kitu ni mitaji ya wakubwa
   
 3. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Matumizi ya ubalozi wetu Beijing kwa mwaka 2011/2012 ni sh 1,352,422,000. Ukilinganisha na uliyoyasema, haviendani.
   
 4. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Havilingani vipi? Bora ungefafanuwa! Jee fedha ni nyingi kulingana na hiyo hali ilioko au fedha zilizotengwa ni kidogo kulingana na hali iliyonayo huo ubalozi?
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Soma post ya Mwanaweja hapo juu.
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Walioko ughaibuni watuambie hali ya ofisi za balozi zetu nje,kwani pesa iliyotengwa ni kubwa sana sana.Twambieni wadau kisha tutathimini katika hali ya kawaida kuona kama kuna usambamba wa matumizi [proportionality].

  Sorry kulisemea hili,uwa sipendezwi kusikia walioko ughaibuni wakiitwa wabeba maboksi,lakini nami nisingependa kushindwa kuhalalisha ni kwanini waliamua kuwaita hivyo.Ili kuthibitisha hilo fanyeni tafiti juu ya ofisi za balozi zetu huko ughaibuni kisha mtuletee.

  Kwa watanzania ukiwauliza balozi za wenzetu tunajua hata kwa kutathimini kutoka kwa nje.Mfano ni lahisi kujua hali ya balozi ya USA kulinganisha na balozi ya nchi ya CUBA.

  Twambieni wengine tushindwe kuhalalisha walioko nje kuitwa wabeba maboksi,kwa kuwa naona binafsi pesa zilizotengwa ni nyingii sana kwa balaozi ,mafano ni ubalozi wa Uingereza ni Nyingi sana kiasi iakaribia billion moja.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi mleta thread alitarajia ku-achieve nini maana hujulikani kama unakosoa matumizi makubwa ya balozi zetu, au unadhani matumizi yanayohitajika ni makubwa kuliko makadirio yaliyopitishwa?
   
 8. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Figures alone dont mean anything...
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mwanaweja namjuwa na wewe nakujuwa . Bado swali langu nalirejesha kwako. Pengine hatujuwi lengo halisi la wewe kuposti hii thread, jee ni kuonyesha ufujaji wa fedha au kuonyesha utowaji mdogo wa fedha? Kwani hata kule mjengoni "Wanacomedi" AKA Wabunge walizungumza hali mbaya ya mgao wa fedha kwa Balozi zetu. Unapolianzisha shangwe uwe tayari na libeneka!
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kutokana na maelezo ya watumishi wengi Balozini hali ni ngumu "hata kama hizo pesa zilizotengewa Balozi zingekuwa zikitolewa angalau nusu yake"
  Ni madeni ni madeni tu kuanzia watumishi hadi huduma muhimu kama pango, fee za shule. matibabu na kadhalika. Hiyo pesa waliyotengewa kama ingekuwa kweli inawafikia basi wangelipa hayo madeni tu.
  Halafu hiyo pesa na figure zake kubwa ni pesa ya madafu ikigeuzwa kwenye pesa hasa kama dola, euro, Omani real na nyenginezo inakuwa hali ya mfuto tu!
   
 11. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280


  Wakuu nimeweka hiyo taarifa kama nilivyoikuta. Lengo langu lilikuwa kuwafahamisha matumizi ya balozi zetu kwa mwaka wa fedha ujao. Kuna ubaya wowote hapo? Whether ni makubwa au madogo sijui kwa sababu sina nyenzo za kufanya analysis. Kama alivyosema Chapakazi hapo juu figures alone don't mean anything. Ni mpaka watu wenye ufahamu na matumizi ya fedha kwenye balozi watakapotoa analysis zao ndio tutajua kama fedha zilizotengwa ni nyingi au ni chache. Na kama post ya mkuu Ngekewa inavyoashiria, hizo fedha zinazotengwa hazipelekwi hata nusu. Watu wenye data wanaweza kutufahamisha kama hizi fedha ni nyingi au chache, au hazipelekwi zote. Naamini tunao hao watu hapa JF. Hilo ndilo lilikuwa dhumuni langu.
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unajuwa ndugu yangu ulivyokuja hukutupa clue kama ulitaka mjadala hasa kutokana na maelezo ya source uliyotumia ambayo yalikwisha simama upande mmoja. Nawe kwa vile ulikaa kimya bila coment ilibidi tufikiri kuwa unakubaliana na msimamo wa source yako. Tumepoteza muda bure kukufunua msimamo wako wakati tungekuwa mbali sasa kukueleza jinsi hiyo pesa haifanyi chochote katika kuzifanya Balozi zetu ziwe na hadhi inayostahiki. Pengine laiti Wabunge wangelijuwa hali halisi ya Balozi zetu basi wangeirudisha hiyo Bajeti ya Mambo ya Nje kama ilivyofanywa ile ya umeme.
   
Loading...