Matumizi ya akili za kimazoea kutatua jambo!

gkutta

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
273
168
Ni akili ndogo sana hutumika kufikiri kutatua tatizo fulani ni kutengeneza jambo kubwa au infrastructure moja kubwa kuliko zingine kusaidia hao wadogo!!..mfano ujenzi wa Reli mwendo kasi, Flyover DSM, na Kuimarisha Muhimbili!!

Tatizo linaloikumba muhimbili kwa sasa ni kigezo muhimu cha ukweli wa kosa ninalolisemea hapo juu!

Elewa kuwa ukijifanya unaipendelea Muhimbili bila kujali kuinua kiwango cha ubora na heshima ya hospitali nyinginezo za pembezoni jua kuwa akili tu itakuumbua maana hata waliopo hizo hospitali za pembezoni nao wanajua mipaka yao kiutendaji kwa mujibu wa uwezo wa hospitali hata kama wanao uwezo binafsi zaidi ya hiyo....matokeo yake Muhimbili inakwa na kitu kinaitwa aggressive feeder roads ambazo hatimaye zitaidecapacitate kiutendejai hata ufanyeje!

Kilichotakiwa hapo kilikuwa kuboresha hizo hospitali ndogo kufikia kiwango cha Muhumbili Kabla hujafikiria kuiboresha Muhimbili zaidi ya ilivyo sasa!...Simple common sense!!....Leo unajenga Flyover moja Tanzania ili magari yote yaje kupitia hapo yakikimbia adha katika vibarabara vibovu huko kwengineko...hiyo haitakuwa permanent solutinion maana itaifanya hiyo Flyover kuwa overloaded na ineffective very soon jeorpordising its own objective for construction on the fist place!
 
Alipaswa wakati ule alivyoenda Muhimbili a sort out the "whole problem" na sio yale matatizo aliyokutana nayo hapo kwa hapo.

Unakuja kununua mi ndege Dearbomba na kujenga ma flyover ya nini kwa sasa??

Bado unawaza uwaziri??

Tanzania vipaumbele vyetu ni Huduma za Afya ya Uhakika ( madawa na vifaa tiba), Elimu Bora ( Elimu na Miundombinu yake ya uhakika), Maji Safi, na Malazi Bora.
 
priorities priorities
walio juu wakiwa wana akili za ku shikiwa ndio maamuzi kama hayo, sasa watu wakiumwa wanaenda India, wakienda muhimbili jua ni magonjwa madogo madogo na wana lazwa VIP, wata mtetea lin mtu anaye lazwa mwananyamala!?
wamekazana kununua ndege, hata barabara za kuunganisha wilaya hatujamaliza, maji tu na umeme upatakinaj wake wa shida.
yaan ukifikiria mpaka unasema nchi yetu kupata hawa viongozi imelaaniwa au ni nn!?
inafika stage una waacha tu.
big up bonge ya article
 
inasikitisha sana! lakini huenda yakawa ya heri huko mbeleni hatuwezi jua!
 
Hivi mtanzania utafanyiwa jambo gani ndiyo kwako useme hili la maana na zuri

Kila linalofanywa na Serikali kwako ni baya na halifai wakati yote yanasaidia kutatua matatizo ya watanzania.

Na matatizo hayaishi Duniani na kwa nchi yoyote ile hata ufanyaje
 
Mtoa maada unaweza ukawa una pointi lakini unashindwa kung'amua umuhimu wa vitu vinavyofanyika.
Ukiwa unawaza kutatua tatizo unawaza njia ya kuanzia. Inaweza ikwa njia ya Top-bottom strategic plan problem solving au Bottom-Top strateguc plan problem solving.

Ukiimarisha muhimbili ni muhimu sana kuipa uwezo wa kuhudumia obvious magonjwa yaliyokua yanatbia nje ya nchi.Hii ni top-bottom,wakitoka hapo wanakuja kuziboresha tena hospital rufaa,mikoani,wilayani vituo vya afya hadi zahanati.Ukiangalia ndio maana juzi hapa wametangaza kugawa vitanda na bla bla hospital za chini.

Mfano tena ukija suala la elimu (kwa current situation) wanatakiwa kufanya bottom-top problem solving,yaani wanaanzia chini kwenda juu kuiboresha elimu.

Kuhusu kuimarisha miundo mbinu,hii inajulikana kabisa,serikali kuu inahusika na miundo mbinu ya kitaifa,halmashauri nazo zina mamlaka na miundo mbinu yao.Mkumbuke pia "jua huwaangazia kwanza watu waliosimama then wanafuata waliopiga magoti.Dar ni mkoa wa kwanza kuingiza pato kubwa serikalini,na hii ni sababu ya biashara kwa hivyo basi,kutatua miundo mbinu ya Dar itakusababisha upate urahisi wa kufanya biashara Dar na kupata pesa zaidi ambayo itakusaidia kuhudumia mikoa mingine km Simiyu,Singida,nk.

Tanzania ina vivutioa vingi vya asili ambazo ni nguzo kwa uchumi wetu kupitia utalii,hivi vivutio si kitu bila miundo mbinu madhubuti,usitegemee miundo mbinu ya jirani kuinua utalii wako,unatakia ujibane ujenge miundo mbinu safi ili kuvutia Wageni zaidi,jamani kupanga ni kuchagua

Niwakumbusheni tena vijana wenzangu,rais iliyepo huyu hatamaliza kila tatizo lakini ataonesha njia ya kwamba tukidhamiria tunaweza.Halafu hakuna maendeleo yanayokuja bila maumivu.Mfano,huwezi ukafaulu mtihani bila kusoma sana,kukesha na kusacrify muda wako,vivo hivyo mkulima huwezi ukavuna mazao mengj bila kufanya kazi kwa juhudi,kuamuka usiku,kugombana na shamba boy nk.

Hivyo basi,sizonje ukiacha mapungufu yake ya kibinadam,sehem aliyowekdza nguvu ya mipangi yake mingi atafanikiwa na michache atafeli.Pia akifeli sio amefeli yeye lakini tumefeli waTz wote.

Mimi naimani kidogo kidogo tutafika tu
 
Ni akili ndogo sana hutumika kufikiri kutatua tatizo fulani ni kutengeneza jambo kubwa au infrastructure moja kubwa kuliko zingine kusaidia hao wadogo!!..mfano ujenzi wa Reli mwendo kasi, Flyover DSM, na Kuimarisha Muhimbili!!

Tatizo linaloikumba muhimbili kwa sasa ni kigezo muhimu cha ukweli wa kosa ninalolisemea hapo juu!

Elewa kuwa ukijifanya unaipendelea Muhimbili bila kujali kuinua kiwango cha ubora na heshima ya hospitali nyinginezo za pembezoni jua kuwa akili tu itakuumbua maana hata waliopo hizo hospitali za pembezoni nao wanajua mipaka yao kiutendaji kwa mujibu wa uwezo wa hospitali hata kama wanao uwezo binafsi zaidi ya hiyo....matokeo yake Muhimbili inakwa na kitu kinaitwa aggressive feeder roads ambazo hatimaye zitaidecapacitate kiutendejai hata ufanyeje!

Kilichotakiwa hapo kilikuwa kuboresha hizo hospitali ndogo kufikia kiwango cha Muhumbili Kabla hujafikiria kuiboresha Muhimbili zaidi ya ilivyo sasa!...Simple common sense!!....Leo unajenga Flyover moja Tanzania ili magari yote yaje kupitia hapo yakikimbia adha katika vibarabara vibovu huko kwengineko...hiyo haitakuwa permanent solutinion maana itaifanya hiyo Flyover kuwa overloaded na ineffective very soon jeorpordising its own objective for construction on the fist place!

Sidhani kama tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye flyover tungewekeza kwenye barabara zinazochepuka ili kuondoa msongamano.

Na badala ya kuwekeza Muhimbili ni kweli bora kuwekeza kwenye hospitali za wilaya na mikoa kwanza bila kusahau dispensaries zetu ziwe kwenye standard ya kuhudumia mgonjwa na anayezidiwa anapelekwa hospitali ya Wilaya,hivyo wagonjwa wengie wataishia Hospitali ya Wilaya na Mkoa,hospitali kubwa kama Muhimbili ni wagonjwa wachache mno tena wale wahitaji zaidi maana imeshindikana kote.

Unapeleka vitanda Muhimbili wakati hakuna majengo na kuacha kupelea vitanda hospitali za Wilaya ambako vinahitajika.

Mbeya imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana,kwa maana wameweza kuboresha hospitali zao za WIlaya na dispensari na kuacha hospitali ya Meta na Rufaa kuhudumia wagonjwa wachache zaidi,wangeweza kuwekeza kwenye hospitali zaote ingesaidia sana

Hii iko Bongo tu.
 
Umeongea hekima tupu!!!
 
Back
Top Bottom