Matumizi mabaya ya neno Amen

chambimagaka

JF-Expert Member
Nov 17, 2017
288
338
Napenda kuchukua fursa hii kutoa mchango wangu juu ya matumizi mabaya ya neno "Ameen "

Hili neno linatokana na neno la Kiebrania "Amina" likiwa na maana ya "Na iwe hivyo."

Neno hilo lilitumika mwishoni mwa maombi kila wakati Wayahudi walipomwomba Mungu.

Neno hili lilitumika kuonyesha msisitizo katika dua na maombi yao kwamba Yehova atatenda kama walivyoomba.
Unaposema AMEN baada ya kumaliza maombi maana yake Unasema NA IWE HIVYO KM NILIVYOOMBA.

Sasa nashangaa baadhi ya ndugu zetu wanalitumia neno hili vibaya.
Utakuta mtu kapost picha za ajali za watu,
picha za waliokufa au watu wenye magonjwa ya kutisha n.k. alafu anaamuru watazamaji wa hizo posts zake kwamba kama wana moyo wa huruma watype AMEN.

Wengine wanaenda zaidi na kutishia kwamba wasipotype neno AMEN watalaaniwa.

Napenda kuwajulisha ndugu zangu kwamba unapotype neno AMEN kwa lugha nyingine unaunga mkono kwamba hao wagonjwa na watu waliopatwa na ajali mbaya waendelee na hizo hali zao mbaya.
Neno hili halipo kwa ajili ya kuonyesha huruma kama wengine wanavyodhania.
Ni vema litumike kulingana na maana yake ya asili.
Ningeomba kushauri ndugu zangu kwamba kabla ya kupost jambo lolote ni vema tufanye utafiti wa kutosha maana tunayopost yanaweza kujenga au kubomoa wengine.

FAHAMU KUWA UKISEMA [HASHTAG]#AMEN[/HASHTAG] UNASEMA NA IWE HIVYO.
NA SIYO KWAMBA [HASHTAG]#UMEOMBA[/HASHTAG] AU KUONA [HASHTAG]#HURUMA[/HASHTAG]

Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom