Matumizi mabaya ya fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

abiko

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
692
588
DIWANI wa Kata ya Masaka, Iringa Vijijini Mathew Nganyagwa ameibua kitu kinachodhaniwa kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za halmashauri ya wilaya ya Iringa yanayohusisha mishahara ya watumishi, matumizi ya halmashauri na matumizi mengineyo.

Katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo kilichoketi katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo hivikaribuni, diwani huyo alisema matumizi hayo yenye harufu inayotia shaka ni ya kati ya Oktoba na Desemba, 2015 ambayo ni robo ya pili ya mwaka wa fedha 2016/2017.

Alisema katika kipindi hicho ripoti ya mapato na matumizi ya halmashauri hiyo inaonesha ilipanga kutumia Sh 8,258,671,300 kati yake Sh 7,341,440,800 zikiwa ni kwa ajili ya mishahara na Sh 917,230,500 kwa ajili ya matumizi mengineyo.

“Lakini matumizi yaliongezeka hadi Sh 11,451,058,440 kati yake Sh 10,701,636,634 kwa ajili ya mishahara na Sh 749,471,806 kwa ajili ya matumizi mengineyo jambo linalohitaji majibu ya kama kweli kiasi cha fedha kilichozidi kilikwenda kwenye mikono salama,” Nganyagwa alisema.

Akizungumzia shaka yake katika ongezeko la mishahara, Nganyagwa alisema katika kipindi hicho cha miezi mitatu kuna ongezeko la zaidi ya Sh Bilioni 3 jambo ambalo ni ngumu kuingia akilini kirahisi.

“Kwahiyo tungependa kujua watumishi walionufaika na fedha hizo, ni waajiriwa wapya na wangapi au wale wale tulionao na ni kwa utaratibu gani?” alisema.
Akizungumzia matumizi mengineyo, diwani huyo aliuliza sababu ya kupungua kutoka Sh 917,230,500 zilizopangwa awali hadi Sh 749,421,806.

“Pamoja na matumizi mengineyo kupungua nashindwa kuelewa matumizi hayo yanatofauti gani na matumizi ya halmashauri yenyewe kwasababu katika kipindi hicho taarifa ya halmashauri inaonesha jumla ya Sh 277,136,203.02 zilitumika kwa ajili ya matumizi ya halmashauri yenyewe,” alisema.

Akijibu madai ya diwani huyo, Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Pudenciana Kisaka alisema amezipokea hoja za diwani huyo na kuahidi kuzifanyia kazi kwa kuzingatia taratibu.

Kisaka alisema kwa utaratibu wa baraza; baraza haliwezi kutoa majibu ya maswali ya papo kwa papo yanayohusu data kama yaliyoulizwa na diwani huyo.

Akisaidia kutoa utetezi wa hoja hizo baada ya kuzuka kwa mjadala uliotaka kujua ni kanuni ipi inamzuia mkurugenzi au yoyote anayehusika kutoa majibu ya hoja zinazohusu data, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Iringa (Menejimenti ya Serikali za Mitaa),

Wilfred Myuyu alisema “Kuna hoja zinazohitaji majibu, ombi langu subirini majibu kwa utaratibu ulioelezwa na mkurugenzi maana mnaweza kufikiri kuna ulaji, matumizi mabaya ya fedha kumbe hakuna ulaji wowote.
 
Back
Top Bottom