Matumizi mabaya pesa za Serikali

MillionaireMan

Senior Member
Jul 20, 2022
157
234
Hivi majuzi yapata majuma yaliyopita, Rais Samia aliwaeleza wananchi kuhusu mikopo aliyoipata kutoka Bank ya dunia na IMF ya kwamba ni mikopo ya bei nafuu.

Haitoshi, tukapata tena mikopo au niseme pesa zilizoolewa bure kwaajili ya nchi zinazoendelea zilizoathiriwa na Covid-19. Mgawanyo wa fedha hizo zilienda kwenye kujenga madarasa, sijui na kitu gani.

Jana tu, Serikali ya Rais Samia imekopa tena zaidi ya $ 1.B . Kama mtanzania wa kawaida nashangazwa na utitiri wa mikopo inayoendelea. Moja ya mikopo tajwa hapo, ilienda kujenga barabara Pemba huko, yaani inaenda nusu kwa nusu Bara na Visiwani Znz.

Mimi siamini kwamba huu ndio mfumo mzuri wa kujenga uchumi wa nchi madhubuti. Kwa mfano, tungebana matumizi na kuachana na stail au mfumo ule tuliozoea mfano, viongozi wa idara, taasisi, mashirika kuwa na madereva, mikutano ya hovyo, kamati zisizo na tija. Kwa mfano, wizara ya Habari imetoa PR kuhusu kamati itakayofanya kazi kutafuta mdundo wenye asili ya Tanzania.

Mama Samia, sijui kama unajua uchumi unavyokwenda na mimi naona hatuna nia ya dhati kweli kujitoa kwenye huu umaskini mkubwa. Watz wnataka kazi, watz wanataka maisha bora. Mimi naoma unajidhatiti na uchaguzi ujao badala ya kushughulikia hata jambo moja tu sawa once and for all.

Cheo ni dhamana, wakati wenu utapita, nchi hii itabaki milele, je watoto wetu tunawaachia nini?

Ndio maana tunataka katiba mpya kutokana na serikali kujiamulia kfanya mambo bila idhini ya Bunge wala mahakama kujua.
 
Cheo ni dhamana, wakati wenu utapita, nchi hii itabaki milele, je watoto wetu tunawaachia nini?.
☝🏾
Mmeanza kuandika mada za kutia huruma eeeh?, Twendeni taratibu tu kila kitu kitajigawa upande wake.

Achane achukue mikopo, mnapaswa kujua hii nchi haina mwenyewe kila anayeingia anaambiwa chota/chukua chako fasta wanaweza kuamka hawa japo tunawathibiti ila huwezi kujua machweo yao.

Haya hawa makamanda waliopandishwa si kwa sababu nzuri sana ila ni kwa 2025, note this.
 
Anaunda kamati za kumshauri kila siku ili kuwapa washikaji wake kupiga hela za mikopo. Eti hela inakopwa wb au imf nkopo mmoja vitu chungu mzima kupoteza maboya. Jambo enzi ya awamu ya 5 wanatumia hela za andani tu. Mama ni mbadhilifu na mpigaji sana. Ngojeni tutakuja kukubali wote.
 
Wanapenda kukopa kwa sababu ndio njia rahisi ya wepesi kupiga pesa zetu, kuliko njia ya kubuni njia zingine za kupata pesa.
 
Back
Top Bottom