Matumizi ARV yapunguza uagizaji dawa

Matumizi ARV yapunguza uagizaji dawa

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
Dawa hizo zinatumika kuzuia na kutibu magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa ambao wana kinga (CD4) chini ya 350.

Aidha mpango huo, utaondoa matumizi ya vitendanishi vya kupima CD4 nchini na badala yake kwa sasa vitakuwapo vifaa vya kupimia kiwango cha virusi.

Hayo yalibainishwa jana na Daktari Mwandamizi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dk. Boniface Nguhuni, alipokuwa akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi.

“Tumeweka mashine hizi katika kanda ndiyo maana vipimo vya Kibaha vinalazimika kupelekwa Hospitali ya Jeshi ya Lugalo na inatokana na upimaji huo kuhitaji utaalamu mkubwa kwa sasa tunaongeza fedha, ili kupata hivi vifaa vya kupimia,”alisema.

Daktari huyo alisema kwa sasa kuna mpango wa kuweka vipimo hivyo katika hospitali za mikoa nchini ili kusogeza huduma karibu kwa wananchi.

Aidha alisema septrine zimekuwa zikinunuliwa kwenye kifurushi cha dawa za ARV na kwamba katika andiko la serikali lililowasilishwa Global Fund limezingatia changamoto zote za masuala ya Ukimwi.

Mbunge wa Viti Maalum, Mary Muro, alisema kuna tatizo serikali inafikiria dawa za ARV bila kujua tatizo la magonjwa nyemelezi kwa wagonjwa hao.

Alisema kuna tatizo la vipimo na kwamba wagonjwa wanalazimika kupelekwa Dar es Salaam na kutopatikana kwa vitendanishi kwenye baadhi za hospitali.

Kutokana na hali hiyo, alihoji ni kwa nini ugawaji wa Septrine usiwe sehemu ya mkakati wa kupambana na ugonjwa huo, ili kuwafanya watu wasife kwa magonjwa nyemelezi.

Naye, Mbunge wa Viti Maalum, Martha Mlatha, alisema alipokuwa mjumbe wa MSD (Bohari Kuu ya Dawa) alitembelea baadhi ya hospitali na kubaini tatizo la mgonjwa kupewa dawa ya aina moja huku akiambiwa asubiri nyingine ambayo huchelewa.

Awali akijibu hoja za wabunge, Naibu Katibu Mkuu Tamisemi, Dk. Zainab Chaula, alikiri kuwepo na changamoto katika mapambano ya Ukimwi ikiwamo ya uwajibikaji wa watendaji na uboreshaji wa huduma za afya na kwamba kwa sasa serikali imeanza kufanyia kazi.
 
Sijaelewa "siledi" ina maana septrine ni miongoni mwa dawa muhimu kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini?
 
Mimi sio daktari wala mfamasia lakini najua septrin (sulfamethoxazole and trimethoprim) ni antibiotic (dawa inayotumika kuua maambikizi ya aina fulani za bakteria)sasa sina uhakika kama matumizi endelevu ya septrin yanamanufaa gani kwa mwathirika maana sio kila ugonjwa nyemelezi unasababishwa na hao bakteria na pia septrin hazitibu kila aina ya maambukizi ya bakteria.
Viti maalumu vibadilishwe wawe wanateuliwa wataalamu wenye walau elemu ya shahada katika fani mbalimbali kama uhandisi, udaktari, ualimu na sheria badala ya kugawa kama peremende kwa hawa kinadada
 
Back
Top Bottom