comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Kwa muda mrefu Hali ya Mlima Kilimanjaro ilikuwa sio ya kuridhisha baada ya Theluji yake kuyeyeka kwa sababu ya mabadiliko ya Tabia nchi kubadilika na kuleta madhara katika kilele cha mlima huu wa Kilimanjaro.
Ni zaidi ya miaka 20 tangu Theluji ya mlima huu wa Kilimanjaro kuanza kuyeyuka kutokana na mabadiliko ya hali ya Tabia nchi..
Lakini kwanzia jana na Leo hali ya Mlima huu umeanza kuleta matumaini baada ya Theluji hiyo kuanza kuonekana inarudi katika hali yake..
Hii ni picha ya Mlima kilimanjaro iliyopigwa miaka ya 1980 ikionyesha hali halisi ya Theluji katika Mlima Kilimanjaro ilivyo kuwa hapo mwanzo..
Hii ni picha inayopigwa miaka ya 2014 ikionyesha hali ya Theluji ilivyo kuwa Mbaya katika Mlima Kilimanjaro.
Hii ni picha iliyopigwa Leo Tarehe 5 / 1 / 2017 ikionyesha hali ya Theluji ya Mlima Kilimanjaro ikianza kujaa katika kilele cha mlima huo..