Matukio ya aibu ya CHADEMA 2010 mpaka 2015

Matukio ya aibu ya CHADEMA 2010 mpaka 2015

Wadau nimeona leo tujikumbushje matukio ya aibu ya CHADEMA ambayo chama hicho kiliyafanya baina ya mwaka 2010 mpaka mwaka huu tulionao. Baadhi ya matukio hayo ni kama ifuatavyo;

(1) CHADEMA ilisusia hotuba ya Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati akitoa hotuba ya kufungua Bunge November 18, 2010 kwa kutoka nje ya bunge kwa madai ya kutomtambua rais, hili tukio lilikuwa la aibu kwa CHADEMA na kujidhalilisha na liliwaonyesha wananachi wa majimbo waliowachagua aina ya wabunge waliowachagua.

Tukio hilolilijidhihirisha kuwa wabunge hao ni magwiji wa uvunjifu wa sheria kwa kushindwa kuiheshimu katiba ya nchi walioahidi kuilinda wakati wakila kiapo rasmi cha kuwa wabunge . Licha ya kwamba baadaye walikuja kumuangukia Dr. Kikwete na kumtambua kuwa ni Rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

(2) Tukio lingine la aibu ni la mbunge wa chama hicho, Joseph Mbilinyi (Sugu) amabaye alitolewa nje kwa nguvu kwa kuburuzwa na askari wa Bunge baada kuanza kupiga askari hao wa bunge baada ya kukaidi amri ya Naibu Spika Ndugai kumtaka kutoka nje.

Tunaweza kuendeleza uzi huu kwa kuandika matukio tata ya chama hicho.

kuna aibu kushinda hizi ?
 
Attachments

  • attachment-14.jpeg
    attachment-14.jpeg
    10.4 KB · Views: 338
  • attachment-13.jpeg
    attachment-13.jpeg
    14.3 KB · Views: 347
  • attachment.jpeg
    attachment.jpeg
    11.3 KB · Views: 349
  • attachment-11.jpeg
    attachment-11.jpeg
    6.6 KB · Views: 346
Mtoa maada anajiita Singidadodoma, watu wa hii mikoa miwili ni wa kuhurumiwa wana mahaba sana na CCM. kwake kaona hayo ni matukio ya aibu, haoni kuwa walifanya hivyo katika kupigania haki zao!!
 
mi nafikiri mtoa mada anatoka mikoa yenye mifugo hivyo naona aende kuchunga ng'ombe mana hata elim ya 4m4 aliyopewa kata haijamsaidia kufanya uchambuz hata mwepec wa kisiasa.pole!!! kadai ada yako
 
kwani umeambiwa hayo mashangii wanapewa bure au wanapewa kwa mkopo!! think big.

Mbona alisema halitaki, halafu mwisho wa siku akaenda kulichukua kisirisiri na kuanza kulitumia?
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012

Utangulizi
Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.

Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;
a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.
b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.
c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.
d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.

Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.
2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya "Mashangingi" yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.
3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .
5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).
6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;

  • Rais
  • Makamu wa Rais
  • Waziri Mkuu
  • Spika
  • Jaji Mkuu

Mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class).

Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.

Hitimisho.

  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya "Shangingi" alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.

Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;
………………………
Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni

21 Juni 2011

Soma hapo kwenye red.
 
Shule za kata zinatoa product ambazo ni substandard kabisa.

Mungu tusaidie.

mkuu hili ni janga kuliko ata ufisadi unaotusumbua hivi sasa,vijana muda wote wanaandika propaganda tu na mambo mengine yasiyokuwa na afya kwa taifa letu.
 
Wadau nimeona leo tujikumbushje matukio ya aibu ya CHADEMA ambayo chama hicho kiliyafanya baina ya mwaka 2010 mpaka mwaka huu tulionao. Baadhi ya matukio hayo ni kama ifuatavyo;

(1) CHADEMA ilisusia hotuba ya Rais Dr. Jakaya Kikwete wakati akitoa hotuba ya kufungua Bunge November 18, 2010 kwa kutoka nje ya bunge kwa madai ya kutomtambua rais, hili tukio lilikuwa la aibu kwa CHADEMA na kujidhalilisha na liliwaonyesha wananachi wa majimbo waliowachagua aina ya wabunge waliowachagua.

Tukio hilolilijidhihirisha kuwa wabunge hao ni magwiji wa uvunjifu wa sheria kwa kushindwa kuiheshimu katiba ya nchi walioahidi kuilinda wakati wakila kiapo rasmi cha kuwa wabunge . Licha ya kwamba baadaye walikuja kumuangukia Dr. Kikwete na kumtambua kuwa ni Rais halali wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

(2) Tukio lingine la aibu ni la mbunge wa chama hicho, Joseph Mbilinyi (Sugu) amabaye alitolewa nje kwa nguvu kwa kuburuzwa na askari wa Bunge baada kuanza kupiga askari hao wa bunge baada ya kukaidi amri ya Naibu Spika Ndugai kumtaka kutoka nje.

Tunaweza kuendeleza uzi huu kwa kuandika matukio tata ya chama hicho.

kususia hotuba ya rais ndio imewaletea katiba mpya
 
Wanaotubeza tunawasamehe na kusonga mbele.2010 CHADEMA tulisusia hotuba ya JK kwa kuwa ushindi wake una utata hadi leo,ila kwa katiba ya nchi matokeo ya Urais hayahojiwi kwenye mahakama yoyote nchini.Kitendo kile kilipelekea mchakato wa katiba mpya kuanza kabla ya maccm(maharamia)kuchakachua mchakato wa katiba
Kususia hotuba ya JK lilikuwa moja ya matukio bora kabisa katika harakati za kupigania demokrasia ya kweli kwa taifa letu
 
hivi kuna kubwa kama WIZI WA ESCROW? ujangili, mauaji ya RAIA kama Mwangosi na kushamiri kwa biashara ya sembe?
 
Kama ungekuwa na akili timamu ungeelezea matukio ya aibu ya CCM kama vile kuongoza na kuwa na mawaziri wabovu kuliko wote Africa na kusababisha kubadilushwa kila mara na hata wabadilishwao nao huwa ni wabovu kama wengine. au ungeeleza matukio ya aibu ya mwenyekiti wa CCM taifa na raisi kwa kumteua Makonda kuwa DC

kitendo cha kumteua makonda kuwa dc,kinashangaza sana kinaonyeshatabia za kihuni zilizopo huko juu,hakuna kitu cha maana alichofanya huyu kijana zaidi ya kutumika kumtukana laigwanan na kumpiga mzee Warioba,anapewa udc kweli tz imekuwa ya kijinga namna hii, huyo mtu wa kutumwa kama jini leo anapata uongozi wa wilaya nzima,aibu iliyoje,kama watumwa hawa ndiyo viongozi hii nchi itapata maendeleo kweli,ujinga wa kuzindua treni ya kwenda rwanda bila reli,unafanywa na viongozi design hii.
 
Tukio Rais kusema amechoka ni bora Muda wake uishe kachunge mbuz kijijin kwao
 
Kubwa kuliko na bora la kufunga mwaka ni uteuzi wa wabunge wawili watakaohudhuria mkutano mmoja wa bunge na kulipwa mamilioni ya fedha kodi yetu wakati hosptali hakuna dawa
 
Back
Top Bottom